Uchaguzi 2020 Uchaguzi Mkuu wa kwanza CCM kukiwa kumepooza, wapinzani wachangamka dakika za majeruhi

Uchaguzi 2020 Uchaguzi Mkuu wa kwanza CCM kukiwa kumepooza, wapinzani wachangamka dakika za majeruhi

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,475
Miaka yote ya Uchaguzi Mkuu CCM huwa ni full list,full mashamsham,umoja,mshikamano na kuaminiana.

Lakini hii Ni kwa Mara ya kwanza CCM inaingia kwenye uchaguzi wakiwa na pengo la Hon BW Mkapa.

BK Membe akiwa sio mmoja wao.

Abdalaman kinana akiwa mpole kabisa.

Nape Nnauye sio yule wa 2010 na 2015.

January Makamba hajulikani alipo.

Mwigulu Nchemba kapooza.

Paulo Makonda akiwa Hana mamlaka yoyote.

Na wengine wengi hawajulikani walipo.

Wapinzani wakubwa wa CCM bara CDM waliokua wako kifungoni,kifungoni Cha kisiasa wanaonekana kupata nguvu kipindi Cha lala salama,au mda wa majeruhi,hii ni baada ya Ruturn Of Tundu Lissu.
Tundu Lissu anaonekana Ni Game Changer

Mkongwe Pekee anaetegemewa kuipigania CCM kwa jasho na damu Ni JM Kikwete.

Huyu Mzee anaetegemewa kubeba mikoba ya BW Mkapa.

Mkapa aliipigania CCM kwa jasho na damu,tunakumbuka hotuba zake za ama kufungua kampeni ama kufunga kampeni alivyokua akitoa hotuba za kuchoma wapinzani.
Je JM Kikwete ataweza kuvaa viatu vya Mkapa?

Mkapa aliitetea CCM kwa nguvu zake zote,kuanzia Zanzibar kwa Mzee Sheni Hadi Mwanza Jimbo la Nyamagana.
JM Kikwete ndio Rais mstaafu pekee mwenye ushawishi ndani ya CCM baada ya Mkapa.
Je ataweza kuziba pengo la Mkapa kipindi Cha kampeni,siku ya Uchaguzi na hata kufikia mda wa kutangaza matokeo?
 
Kikwete hawezi maana ana ndugu yake Membe kwaiyo atapoa ila kimoyomoyo anapenda membe achukue nchi Magufuli afeli
 
CCM wanaenda kukamilisha utaratibu tu ila kiuhalisia wameshashinda wala tusijidanganye hapa! Lissu tangia arudi kashatoa matamko Kama 70 Huku hakuna ata hoja moja iliyokaa ata kwenye vichwa vya washabiki wake zaidi ya nyimbo zisizo saidia taifa..
 
Kwa speed na mwenendo wa Lisu ni Big Ben,Kinana, Nape na Junuary yuleee sio huyu ndio watawezana kwenye siasa za majukwaani, unless mzee wa Msoga anakibarua kizito sana.
 
CCM wanaenda kukamilisha utaratibu tu ila kiuhalisia wameshashinda wala tusijidanganye hapa! Lissu tangia arudi kashatoa matamko Kama 70 Huku hakuna ata hoja moja iliyokaa ata kwenye vichwa vya washabiki wake zaidi ya nyimbo zisizo saidia taifa..
Umepata mpaka nafasi ya kuyahesabu!?

Mahaba yaliyoje.
 
Mbuyu haukumbatiw endeleen kujitekenya wenywe na kucheka wenyewe pengne vilembwe wa vilembwe vyenu ndio wanaweza walau kuota kutawala nchi hii lakini kwa nyie msahau kabisa hata mkiweka wagombea 100 wapambane na Jpm bado atawashinda utendaj wake ni kampeni tosha .Hana haja ya kufanya kampeni mwaka huu kazi zinaongea.
 
Upinzani bongo ni shida tupu...mnaokoteza sana mambo....Jakaya Kikwete hana undugu na huyo Maembe
 
Back
Top Bottom