Pre GE2025 Uchaguzi Mkuu wa mwakani ufutwe ili kuokoa gharama

Pre GE2025 Uchaguzi Mkuu wa mwakani ufutwe ili kuokoa gharama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Nyarupala

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2024
Posts
494
Reaction score
856
Japo itaonekana ni kuvunja katiba lakini kuna sababu za msingi za kufanya hivyo.

Hivi bunge halioni kujadili hili suala na hatimae mahakama kupitia mwanasheria mkuu wa serikal naye akashirikishwa na hatimaye ikapitishwa kwa kauli moja ya kwamba uchaguzi wa Rais na Wabunge usiwepo kwaajili ya kuokoa gharama?

Binafsi ningeomba chama tawala kipeleke ombi mahakamani la kuondoa uchaguzi na mahakama iridhie hiki kitu kwa chama tawala kutoa sababu za msingi za kuahirisha huo uchaguzi kama;

-Kuokoa gaharama za uchaguzi ili kisudi zile pesa ambazo zingetumika kwaajili ya maandalizi ya uchaguzi zipelekwe kwenye miradi mingine.

-Hakuna chama kinachoweza kushindana na CCM kwa sasa,kwasababu vyama vya upinzani havina hoja za msingi za kuwashawishi wananchi au wapiga kura kiasi cha kuwanyima kura CCM hapi mwakani.

Ya kwangu ni hayo tu.
Maoni yaheshimiwe.
 
Back
Top Bottom