Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Uchaguzi wa kihistoria wa Tanzania utakao fanyika mapema oct.2025, utafanyika kwa uhuru, haki na uwazi kwa mujibu wa katiba na sheria za Taifa letu, na sio kwa makelele na upotoshaji wa wanasiasa wa vyama mbalimbali vya siasa nchini kwa niaba ya mabwenyenye ya Magharibi kupitia vibaraka wao eti kuielekeza Tanzania namna ya kuendesha uchaguzi.
Uchaguzi wa Tanzania utafanyika kwa salama na amani, na ni wito wangu kama mdau wa siasa nchini, kuwasihii waTanzania wenzangu kupuuza makelele, uzushi na uchochezi wa aina mbalimbali unaofanywa na wanasiasa wenye nia ovu dhidi ya umoja, amani na utangamano miongoni mwetu, huku familia na maslahi yao yakiwa ughaibuni kwa wanao wafadhili.
Hayupo mTanzania wa kudanganywa na kibaka wa siasa,
Ni muhimu wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa wingi zaidi, na kujitokeza kwa mamilioni yetu kupiga kura, ili hatimae tupate fursa ya kulidhibiti mdimo na makelele ya laghai na kibaraka wa ukoloni mambo leo kwenye sanduku la kura, Oktoba 2025.
Mungu Ibariki Tanzania