Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Kufanyika tarehe 30/1/2021

Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Kufanyika tarehe 30/1/2021

Melubo Letema

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2020
Posts
416
Reaction score
414
Uchaguzi Mkuu wa RT unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu wa kwanza, huku nafasi ambazo zitahitajika ni nafasi ya Rais na Makamu wake pamoja na Wajumbe 6, ikiwemo moja ya Viti Maalum Mwanamke.

Fomu zitaanza kuchukuliwa Kesho (8 hadi 19, Januari), kwa ada ya shilingi laki mbili (200,000/=) kwa nafasi ya Rais na Makamu wake.

Fomu za wajumbe zitauzwa kwa shilingi laki moja (100,000/=) kwa kila mjumbe na viti maalum wanawake.

Kila mchukua Fomu Lazima arudishe yeye mwenyewe ( Physically).

Usahili utafanyika tarehe 21/1/2021, Jijini Dar es Salaam.

Wakati, Nafasi ya Katibu Mkuu na Mweka Hazina zitakuwa ni za Kuajiriwa, hivyo watatuma viambatanisho vyao.
 
Back
Top Bottom