Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Hii ni fundisho kwa viongozi wote kwamba Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu,na sauti ya umma si yenye kudharauliwa hata kidogo,ni wakati umefika sasa kwa viongozi wengine kujifunza haya yalitokea Chadema
Jana nilikuwa nafuatilia matangazo ya Television ya uchaguzi wa Chadema,nilivutiwa na mchambuzi wa maswala ya siasa bwana Buberwa,alisema hivi nanukuu " Ukiona kiongozi umekaa miongo mitatu madarakani mpaka vizazi vipya vimekukuta na wewe upo tu basi ni wakati wa kukaa pembeni"
Na wataalamu hao wa mambo ya siasa walisema hata Mwalimu na baba wa taifa Julias Nyerere watu walimchoka pamoja na kuanza kumuita mchonga meno na mambo kama hayo,hii inaonyesha kwamba inafika kipindi kama kiongozi inabidi ujitathimini na kufanya maamuzi sahihi
Mheshimiwa Mbowe bahati mbaya sana hakuliona hilo na kibaya zaidi alidharau sauti ya umma na mwisho wa siku tumeyaona yaliyo tokea,amejifunza in a hard way,badala ya kustaafu kwa heshima baada ya kukijenga chama kwa mda mrefu matokeo yake amestaafu kama loser
Tunaelekea katika Uchaguzi mwaka huu na hapana shaka mama yetu kipenzi Samia Suluhu Hassan atapeperusha bendera ya Tanzania tena kama raisi wetu,kuna maneno maneno mengi yanasemwa kwamba huenda mama yetu kipenzi akagombea tena mwaka 2030
Basi ni busara sana kwa washauri wake walione hili mapema ili mama yetu amalize ngwe yake kwa heshima na kumkabidhi mtu mwingine kijiti ili asipate kuchafua heshima aliyojiwekea,naamini chama chetu cha ccm kina azina kubwa ya wanasiasa wenye busara na maono makubwa
Nimalizie kwa kusema kwamba kwa upande wa Chadema imetuonyesha demokrasia kwa upande mwingine wa shilingi kwa uchaguzi kufanyika kwa haki,na wajumbe kwa nyakati tofauti walijipambanua wazi wazi kwamba wanamuunga mkono mgombea fulani,hakika wameonyesha uthubutu na ukomavu wa kisiasa,kongole kwao
Mungu ibariki Afrika na Mungu ibariki Tanzania
Ni hayo tu!