The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Chuo kikuu cha Dar es Salaam kupitia shule kuu ya uandishi wa habari na mawasiliano kwa umma (SJMC) kwa miaka kadhaa kimekuwa kikitekeleza mradi unaojulikana kama 'Yearbook' ukiwa ni utafiti kuhusu “Ubora wa Maudhui ya Vyombo vya Habari Tanzania. Katika mwaka 2024 utafiti huo ulichunguza uripoti wa vyombo vya habari kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Kwa kutumia vigezo mahsusi, utafiti huu ulivichunguza vituo 35 vya redio kutoka pande zote nchini Tanzania ukijumuisha vituo vya redio vya ndani vyenye leseni za mikoa, wilaya na redio za jamii pamoja na kituo cha Utangazaji cha Taifa (TBC Taifa).
Pia soma Matukio ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kila Mkoa Tanzania Bara: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Utafiti huo unabainisha kuwa vyombo vya Habari vilishindwa kufanya tathmini na kuripoti mafanikio na kushindwa kwa wagombea waliokuwa madarakani, kutekeleza majukumu yao.
Uchunguzi kuhusu mafanikio ya wagombea uliripotiwa kwa kiwango cha chini (10%) na uchunguzi wa kina wa wagombea waliokuwa madarakani kuhusu kushindwa kutekeleza majukumu yao ni kama haukuwepo kabisa (1%).
Kwenye kampeni za uchaguzi, kuyataja mafanikio ya mgombea wakati akiwa madarakani kunawawezesha wapiga kura kufahamu kuhusu uwezo wa wagombea wanaogombea nyadhifa mbalimbali na hivyo kuwawezesha wapiga kura kuwachagua wagombea kwa usahihi. Mwaka 2024, ni 8% tu ya kazi zilizochunguzwa ndizo zilizoripoti mafanikio ya wagombea wakati wakiwa madarakani. Zaidi ya asilimia 90% ya kazi zilizohusu wagombea hazikuripoti kuhusu mafanikio yao.
Vyombo vya habari kuripoti kuhusu kutofanikiwa kwa mgombea fulani ni jambo muhimu mno kwani linawawezesha wapiga kura kuuelewa udhaifu wa mgombea husika. Mwaka 2024, ni kazi tatu tu (3) ndizo zilizoripoti japo kwa kidogo kuhusu kutofanikiwa kwa wagombea. Hii ina maanisha kwamba, wakati wa uripoti wake, vyombo vya habari havikuwachunguza wagombea kwa kina.
Kwa kuzingatia umuhimu mkubwa wa vyombo vya habari kwenye nyakati za uchaguzi, udhaifu huu uliojitokeza ni mkubwa mno; vyombo vya habari vinapaswa kuchunguza kwa kina mafanikio na kushindwa kwa wagombea ili kuwawezesha wapiga kura kufanya maamuzi sahihi ya uchaguzi.
Chanzo: Yearbook on Media Quality in Tanzania 2024