Uchaguzi serikali za mitaa: Ambao hatujajiandikisha na hatuna mpango wa kujiandikisha tukutane hapa

Nimejiandikisha kwasabau muandikishaji alikua dada mzuri nikataka kupiga nae stori mbili tatu na kubadilishana mawazo tu, Kwenda kupiga kura bado natafakari, Mama mstaafu jirani yangu anagombea kwa tiketi ya chama pendwa na kaniomba na kunisihi sana nisimuangushe kama jirani yake. Huenda nikamsapoti jirani
 
[emoji23][emoji23][emoji23] hatari sana labda wameshajiandikisha huo mtaa
Unajua nn..hamna serikali iloharibu maana kamili ya upigaji kura kama hii ya sasa.

Watu wamechoka, ma walichoshwa na tabia zilizotokea za chaguzi ndogondogo zilizopita hapo nyuma.

Watu hawaoni maana tena, maana wapige wasipige, ..hamna mtu atakayetangaza matokeo yasomfurahisha mkuu wa wilaya,wamkoa, Rais.

Nifanyeje sasa?????
 
Yaani napata wapi ujasiri na ndevu zangu kwenda kuandika jina langu eti nikapige kura??? Nikaangalie pambano ambalo mmoja kafungwa kamba mikoni na mmoja anapiga tu eti tunalazimishwa kumshangilia huyu mshindi wa kupangwa.
Kwenye hili Rais ajue yeye ndio chanzo na hatutajitokeza hata watangaze mpaka usku wa manane sisi hatutaenda na hata watufungulie mashtaka hatutaenda.
 
pumbavu wote wanaosema hawatopiga kura

Mkuu kwa watu wenye akili timamu na wanao penda justice and democracy kwa siasa zilivyo sasa huwezi kwenda kupiga kura.
Na hata kwaka ujao ni wachache sana watapiga kura.

Hii iwe fundisho kwa watawala kuwa na justice pia waheshimu mawazo ya wananchi . Haiwezekani uwaambie wananchi waombe msamaha kwa kuchagua upinzani au mtu mwingine usie mtaka wewe kiongoz pia uminywaji wa democracy unaoendelea ni vema tu ili kusiwe na vita vya kuchukiana kuumizana tuamue kurudisha utawala wa chama kimoja maana nadhani hii ya vyama vingi ukweli imetushinda.

Mkuu mbaga jr, siasa sio uhasama ila nikupata platform ya wananchi kuelezea hisia zao kwanini wamemchagua huyu na wamemwacha huyu ili itusaidie ku learn theough mistakes lakini inapogeuka kuwa vita na kuumizana na kutoana uhai hapo tunadhani ni vema waungwana kutothubutu hata kusogea kujiandikisha.
 
Naona uvivu hata nikijiandikisha sidhani kama kura yangu itasaidia maana matokeo yameshapangwa. kwanza kura zitapigwa siku moja kabla ya wengine siwezi piga kura
 
Mimi sitajisumbua tena maana nina Passport na NaID
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…