Uchaguzi serikali za mitaa: Ambao hatujajiandikisha na hatuna mpango wa kujiandikisha tukutane hapa

Uchaguzi serikali za mitaa: Ambao hatujajiandikisha na hatuna mpango wa kujiandikisha tukutane hapa

2015 nilitumia zaidi ya lita 10 kufatilia kujiandikisha. Nikakaa juani. Kupiga kura nikakaa juani masaa 6 maana jina langu halikuwepo.
Afu mshenzi 1 akarudi huko huko.

Nitapiga kampeni watu wasipige kura 2020
Na mvua hizi uache kulala zako ukapange foleni ya kupiga kura ambayo kwa vyovyote tu itapuuzwa
Kura
 
Root, Hilo la kupiga kampeni unaweza kuchukuliwa hatua
 
Huku tukielezana kwa nini hatujajiandikisha. Kwa upande wangu mimi naona uvivu....hivyo tu
Wale 'wazalendo' pia karibuni
To hell hata kama wangeweka zawadi ya gunia la mkaa kwa kila anayejiandikisha nisingejiandikisha...hii ni drama matokeo yanayo tayari naninaaa!
 
mimi nilishasema sitaka nipige kura tena, toka nipigie kura yangu ya kwanza na ya mwisho 2015....,wanasiasa wote ni wanafiki tu,,,,,,,
na pia ni haki yangu ya ki demokrasia kutopiga kura,,,,,
ni ujinga kuchagua vitu vilivyopangwa tayari,,,,
kumbe tupo wengi
 
Ninapoishi na kilipo kituo cha kujiandikisha ni hatua za miguu kama 25 tu. Ila kila siku nawapita kama sijui hata wanachokifanya.
 
Sitaki tu kwenda kujiandikisha ..nikikumbuka nilivyopoteza maji yangu mwilini kwa kupigwa na jua mwaka 2015,alafu mambo yakawa shaghalabaghala..sitaki Tena kupoteza energy.
 
Habari za kusumbuana na kuandikishana majina sitakagi me, kwanza sikai sehemu moja popote kambi me
 
Habari za kusumbuana na kuandikishana majina sitakagi me, kwanza sikai sehemu moja popote kambi me
 
To hell hata kama wangeweka zawadi ya gunia la mkaa kwa kila anayejiandikisha nisingejiandikisha...hii ni drama matokeo yanayo tayari naninaaa!
[emoji23][emoji23][emoji23] ngoja ufuatwe na mtutu
 
Mimi sioni sababu ya kujiandikisha kama washindi wameshajulikana
 
Back
Top Bottom