Uchaguzi Serikali za Mitaa: Ni huzuni, aibu, fedheha na si afya kwa Chama cha Mapinduzi(CCM)

sasa nyie mnatka mmebwe na nini
si mmesusa mkajua uchaguzi hauta fanyika
 

Uko sahihi kwa utetezi wako, sasa twende pamoja, lengo la kujaza fomu ni ili kupata wagombea kwenye uchaguzi na sio umahiri wa kujaza fomu. Sehemu zote zenye nia njema unapojaza fomu kisha ukakosea, hupewa nyingine ujaze kwa usahihi na sio kuenguliwa kwani hapo haukuwa mtihani wa kujaza fomu bali lengo ni uchaguzi. Makosa ya ujazaji fomu yako kuanzia bank, fomu za NIDA, nk, lakini kote huko hakuna aliyefukuzwa kwa kukosea kujaza, bali hupewa fomu nyingine ili kujaza kwa usahihi kwani lengo sio kukomoa bali kupata huduma husika.

Hilo hapo juu ni moja, huenda kweli walikosea kujaza kama mnavyolazimisha japo ni jambo lisilowezekana kwa idadi hiyo. Je ni kipi kilikuwa kinafanya hao wasimamizi wagome kutoa ushirikiano kwa wagombea wa upinzani na hujuma nyingine za wazi kwenye huo mchakato? Ni dhahiri hapa rais ndio anayeagiza huo ubakaji wa box la kura, hasa ukizingatia kile kinachoendelea kwenye huo mchakato.
 
Unaposema form za wagombea wa CCM zilikuwa na kasoro ndogo lakini wao hawakufuatilia. Ni nani hao ambao hawakufuatilia? Ebu fafanua hapo.
 
Hata mtoto wangu Wa darasa la pili hawezi kukuamini,wagombea wote Wa upinzani hawajui kujaza form,hii inatokea mwaka huu,tulijua hamwezi kukosa sababu,sasa basi malengo yenu yametimia kama mlivyotaka,fanyeni sherehe kwa kushinda kwa kishindo,pili ninaamini wapinzani ndo walikuwa wanawaletea watz umaskini kwa sasa uchumi utapaa kwa double digit,huduma za jamii asilimia 100 maisha bora kwa kila mtanzania
 
Hata mbuyu ulianza kama mchicha ! Machafuko huanza kwanza kwa kudharau mambo madogo kama haya but mwisho wa siku watakaoumia ni wapiga kura na ambao hawapigi kura
 
Unaposema form za wagombea wa CCM zilikuwa na kasoro ndogo lakini wao hawakufuatilia. Ni nani hao ambao hawakufuatilia? Ebu fafanua hapo.
Wapinzani hawakufuatilia ili kuwawekea pingamizi kama walivyo wenzao was ccm
 
Jamani eeeee!!!!!!! Katafute riziki,mambo ya siasa ya nchi hii muda mwingine inabidi kuziba pua.
 
Tukubali kushindwa kama hatukujipanga kwa wakati huu

Demokrasia ina mambo mengi ukizidiwa mbinu unarudi nyuma kusahihisha makosa
ahsante kwa kuunga mkono siasa za hila zinazolindwa kwa nguvu zote!!!!!!!
Anyway ushindi ni ushindi kaza mwendo mkuu
 
Tukubali kushindwa kama hatukujipanga kwa wakati huu

Demokrasia ina mambo mengi ukizidiwa mbinu unarudi nyuma kusahihisha makosa
Tuelezee aina za demokrasia unazozifahamu ili tujue hii imeangukia wapi? Hiki kituko ulishakisikia wapi duniani kama siyo hapa Tanzania? Tumejitahidi kuitangaza nchi yetu lakini sasa inafika wakati tutasema sisi siyo watanzania bali ni wakenya kwa kuogopa kashfa. Hata wakati wa mwalimu tulikuwa tunapigia jembe na nyumba au ndiyo na hapana na hakuna mtu alikuwa anakuwa disqualified sababu kulikuwa na wasaidizi kukuongoza kukosoa ulipokosea.
 
Tukubali kushindwa kama hatukujipanga kwa wakati huu

Demokrasia ina mambo mengi ukizidiwa mbinu unarudi nyuma kusahihisha makosa

Tumekuwa na nakisi kubwa ya uongozi katika zama hizi. Watu mbilikimo katika uongozi hawawezi kujua umuhimu wa seriali za mitaa. Kumbe huu ndio uongozi muhimu kabisa kuna unakuwa maisha ya kila siku ya wananchì. Ifahamike kuwa katika ngazi hizi za chini kabisa wananchì huwa hawachagui vyama vya siasa bali "individuals" wanaokidhi vigezo vinavyotumika kwenye jamii husika kumtambulisha mtu mwenye karama ya uongozi; siyo chama. Hata kama ingekuwa kweli kuwa wagombea wa vyama shindani wamefanya makosa kwenye fomu za kugombea bado busara ingetumika kuona kuwa hayo makosa hayaathiri uchaguzi wenye ushindani. Ukiona tu zaidi ya nusu wagombea wanakwenda kuenguliwa ujue tayari uchaguzi umevurugika na siyo busara kuendelea. Kwa hili la uchaguzi wa serikali za mitaa nchi ya Nyerere imenajisiwa kupita maelezo. Itoshe tu kusema: com, the ball is in your court.
 
Jafo umechemka sana bro.; kuna watu eti walikuwa wanatoa chepuo kwamba unafaa URAIS 2025, sasa uchaguzi huu mdogo umekushinda huo urais upi utaweza, labda kuongeza wake hadi wafike 4 hilo sipingi.
 
Ati ccm members wao walijaza 100% perfectly huu ushenzi anaweza kuuamini Jaffo tu.
 
Wapinzani hawakufuatilia ili kuwawekea pingamizi kama walivyo wenzao was ccm
Bado sijaelewa labda mimi ni kilaza nivumilie tu. Ninachotaka kijua hapa ni hivi, kila ngombea alijaza form yake na baada ya kujaza inapelekwa kwa hao watendaji. Sasa hizo form kila mgombea alikuwa na uhuru wa kukagua form za wenzake upande wa upinzani ajue kama kakosea kujaza? Au niweke swali langu hivi, hao wagombea wa CCM walijuaje kwamba wapinzani wao wamekosea kujaza form? Au form baada ya kujazwa zilibandikwa kwenye ubao/ukutani?
 
Tukubali kushindwa kama hatukujipanga kwa wakati huu

Demokrasia ina mambo mengi ukizidiwa mbinu unarudi nyuma kusahihisha makosa
Ccm siyo chama cha siasa tena ni genge la magaidi wavaa kijani, waabudu mungu wao mwenge Nyamrunda.
 
Wewe kweli kiongozi mzuri. Sasa kama hizo fomu zilitakiwa umakini mkubwa, waliotakiwa kuwafunza namna ya kujaza ni viongozi wa vyama au huyo huyo mwenye kuziandaa?? Kutakuwa na kosa gani kusema kuwa; Jafo ni CCM, akaandaa fomo (CCM), akaweka kamtego kadogo kumpata kosa mjazaji, halafu akauonesha mtego kwa wanaye (CCM) huku akiuficha mtego wake kwa wasio wana(Wapinzani) ili tu washindwe??
Mshauri Jafo kuwa; Asituteulie viongozi halafu aseme tuwachague aliokwisha wateua. Huo ni uhuni na hatutaki kuitwa wahuni.
Ushauri; Asogeze mbele uchaguzi tuletewe wapinzani wa kutupinga ili watu wanaotupenda ambao kwa kweli ni wengi watuchague.
 
Ngoja tuendelee kusifu na kuabudu

Binafsi naishukuru sana sana serikali ya awamu ya tano kwa kututengenezea ardhi, mito(rivers), maziwa(lakes), wanyamapori, misitu ya asili, Bahari pamoja na mlima Kilimanjaro. Lakini pia naishukuru serikali kwa kutuondolea joto na kutuletea mawingu na mvua katika jiji letu la Dar kwa siku ya leo.

mungu ibariki serikali yetu ya awamu ya tano [emoji1431][emoji120][emoji1431][emoji120][emoji2536][emoji120][emoji120][emoji2536][emoji1431][emoji120]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…