Uchaguzi Serikali za Mitaa: Ni huzuni, aibu, fedheha na si afya kwa Chama cha Mapinduzi(CCM)

Ukiangalia mchakato mzima na mambo yaliyotokea kuhusiana na uchaguzi wa serikali za mitaa, ni wazi kwamba ushindi wa uchaguzi wa serikali za mitaa ni ushindi ambao mwanachama yeyote wa CCM mwenye akili timamu na busara atapaswa kuuonea aibu badala ya kuushangilia.Na hata zaidi, kuna maeneo ya uchaguzi ambayo ushindi huo unapaswa kukemewa na wanaCCM wenyewe kabla ya watu wengine.

Sasa swali la kujiuliza ni kwamba, kuna wanachama wangapi wa CCM ambao ni watu wenye akili timamu na busara? Sasa hilo litakuwa wazi matokeo ya uchaguzi yatakapotangazwa
 
wewe maiti,hivi hujui kuwa wapinzani hawaruhusiwi kufanya mkusanyiko wowote either wa ndani au nje na je nani amewazuia?
 
Wapinzani hawakufuatilia ili kuwawekea pingamizi kama walivyo wenzao was ccm
Unamaanisha kinachotafutwa ni makosa ya kujaza form, na sio sera wala malengo ya mgombea? Vipi taasisi nyingine kama bank, NIDA, vyuo vya elimu nk. wakifuata mfumo mnaoutumia ninyi kuchuja waombaji?
 


Hahaha! I say hawa jamaa mapoyoyo kweli. Yaani mtu ambae hawezi hata kuandika kiswahili ndie wakamchukua ku assess form? Angalia badala ya kusema "kutoainisha" akasema "kutoiwaisha". Afadhali hata angesema kutoainisha!

Kwanza kutoiwaisnisha sehemu sahihi anakoishi ndio kiswahili gani? Inaonyesha uduni wa elimu ya huyu mtu - yaleyale ya watu wenye akili ndogo kupewa mamlaka makubwa!
 
Raha ya ushindi ni kushindana, lakini ushindi wa kupewa ama kubebwa hauna raha yeyote. Hi aibu ni ya kiwango cha lami.
 
Wewe kweli mwehu, kwahiyo watendaji kukimbia ofisi na yenyewe ilikuwa ni maelekezo ya kwenye form?
Eti tukaenda kuangalia, ulikwenda kuangalia kama nani?
Mnazidi kujitia uchizi tu, na kuwatia hasira wananchi. Haya mmeshinda jiapisheni basi.
 
Hivi kweli hata Wenyeviti waliomaliza muda wao hawajui kujaza fomu!? Kweli now ni mene mene na tekeli!
 
Dr. Bashiru aitoe CCM kwenye uchaguzi huu, ibaki CUF na T ELO P.
Bashiru pamoja na kuwepo kwenye chama chenye uchafu mwingi, anajitahidi kutotumbukia mzimankama alivyotumbukia Polepole.

Siamini kama Bashiru atakuwa alishiriki kwenye huu ujinga uliotokea. Kwa kiasi kikubwa hii ni mipango iliyomhusisha mwenyekiti, mwenezi, bashite na jafo.
 
Unaonekana ni mtu mwenye kupenda kufuata misingi ya Haki. Naamini una elimu nzuri ndani yako.
Unanifanya niamini si ccm wote waliooza
 
Inasemekana IDD Amin Aliwahi kununua ndege 69 ndani ya miaka 9 hivi ni Kweli?
 
Post bora kama hivi wale praise team wanazipita kama hawazioni na kikubwa zaidi na cha muhimu kabisa.. Umetanguliza maslahi yako wazi kabisa kuwa wewe si mpinzani ni mwana CCM
 
Vijana wanao anza kuonja asli ndiyo chanzo kikubwa cha haya yanayo jiri leo. Busara na hekma za wazee zilitupwa kando saana. Wazee na washauri wote wameonekana kama hawana nafasi na walipo jaribu kushauri waliambiwa wakae kimya na haya ndiyo matokeo.
 
Mleta mada unapoitaka CCM yako iondoe dosari hujuwi kuwa unataka wamuondoe rais mahana ndiye dosari yenyewe. Magu ndiye mvurugaji mwandamizi wa chaguzi za marudio na wa serekali za mitaa.
 
Unawaonea hao watendaji walikuwa wanatekeleza maagizo mahsusi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…