GE2025 Uchaguzi Tanzania 2025: Kampeni za mwaka huu hazina mvuto ukilinganisha na miaka iliyopita

GE2025 Uchaguzi Tanzania 2025: Kampeni za mwaka huu hazina mvuto ukilinganisha na miaka iliyopita

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Kampeni za mwaka huu hazina mvuto ukilinganisha na miaka iliyopita," anasema mchambuzi wa siasa za ndani, Mohamed Issa, akieleza hali ya kisiasa inavyoendelea nchini Tanzania mwezi mmoja tangu kuanza rasmi kwa kampeni za uchaguzi mkuu Agosti 28, 2025.

Kwa sasa, picha kubwa inayoonekana ni chama tawala CCM kutawala anga la kisiasa kwa nguvu kubwa, likijaza viwanja vya mikutano na kuonekana peke yake katika sehemu nyingi za nchi.

Vyama vingine vidogo vya upinzani vinavyoendelea na kampeni vimekosa rasilimali, nguvu na hata ufanisi wa kushawishi umma kama ilivyokuwa katika chaguzi zilizopita.

Katika muendelezo wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 29, Mgombea Makamu wa Rais kupitia C.webp


Chama kikuu cha upinzani, Chadema, kilitangaza mapema kuwa hakitashiriki uchaguzi huu, hatua iliyosababisha pengo kubwa na kuondoa mvuto uliokuwa ukionekana miaka iliyopita.

Kwa upande wa chama kingine cha upinzani chenye ukubwa, mgombea wake urais Dk. Luhaga Mpina bado hajaanza kampeni kutokana na kuenguliwa kwake na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), kesi yake ikiendelea Mahakamani kupinga hatua hiyo.

Kwa mujibu wa rekodi za INEC, kati ya vyama 19 vilivyosajiliwa nchini, ni Chadema pekee kimeamua kutoshiriki uchaguzi wa mwaka huu, huku vyama vingine 18 vikijitosa, 17 vikisimamisha wagombea urais.

Hali hii inafanya uchaguzi huu wa Oktoba 29 kuwa wa kipekee tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka1992 na uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi 1995, kwani ni mara ya kwanza chama kikuu cha upinzani kinajitoa kabisa kushiriki uchaguzi mkuu.

"Hakuna upinzani imara"
Mchambuzi Mohamed Issa anabainisha zaidi hali hii:

"Hakuna chama chenye mizizi imara kwa upande wa upinzani kuweza kukabiliana na CCM. Hata mikutano ya vyama vinavyoendelea na kampeni haionekani kuleta shamrashamra kama miaka ya nyuma."

Katika chaguzi za miaka iliyopita, vyama kama Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi au hata TLP vilikuwa na nafasi ya kuibua mijadala mikali na kushindana vikali na chama tawala. Mikutano ya kampeni ya upinzani mara nyingi ilikuwa na umati mkubwa wa watu, ikionyesha hisia za kisiasa zilizogawanyika zaidi miongoni mwa wananchi.

chaummaaa.png


Lakini mwaka huu hali hiyo haipo. Badala yake, CCM imeonekana kutawala kabisa uwanja wa kampeni, ikifanya mikutano mikubwa inayojaza maelfu ya wananchi huku wapinzani wakijikongoja na mikutano midogo isiyokuwa na uhamasishaji mkubwa.

Hata hivyo, sio kila mchambuzi anayeona hali hii kama ishara ya udhaifu wa demokrasia. John Ngwandu, mchambuzi wa masuala ya siasa aliyezungumza na Crown Media, anatoa mtazamo tofauti:

"Tunakwenda vizuri, vyama vyote vinavyoshiriki vinapambana kwa kadri vilivyojipanga." Aligusia hayo alipohojiwa na Crown Media.

Kwa mujibu wake, hali ya kampeni sasa inaonyesha ushindani unaolingana na nguvu, maandalizi na rasilimali za kila chama. Anasisitiza kuwa, japo vyama vya upinzani havina ukubwa sawa, bado vinajitahidi kuweka ajenda zao mbele ya wapiga kura.


Katika muendelezo wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 29, Mgombea Makamu wa Rais kupitia...webp



Sauti za wananchi zinaonyesha mtazamo unaofanana kwa kiasi kikubwa na ule wa wachambuzi, hasa kuhusu ukosefu wa mvuto kwenye kampeni za mwaka huu.

Selemani Pacal, mkazi wa Dar es Salaam, anaona taswira ya kampeni kwa mtazamo wa matokeo:

"Uchaguzi ni kama umemalizika. Huoni ni kwanini CCM isishinde kwa kishindo kama utaangalia kampeni zilivyo?"

Mwananchi mwingine Naomi Metusela, anahisi kwamba kukosekana kwa Chadema kumeondoa ladha ya uchaguzi:

"Chadema kutokuwepo kumepunguza ladha ya uchaguzi. Ni kama uchaguzi hakuna. Mimi nimetembea Dar es Salaam hata bango moja la mgombea urais wa upinzani sijaona, naona CCM tu."

Chadema yenyewe inasema kinachoendelea ni kiini macho, na huo ndiyo msingi wa kutoshiriki kwa uchaguzi wa mwaka huu, mpaka mifumo ua uchaguzi itakaporekebishwa ili kuwa na uchaguzi huru na wa waki na wenye ushindani.

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduz.jpg


Lakini si wote wanaojadili uchaguzi kwa mtazamo mmoja. Katika mazungumzo ya vijiweni, mijadala imegawanyika kati ya wanaozungumzia kampeni na uchaguzi wa Oktoba 29, na wale wanaojikita zaidi kwenye maandamano yaliyotangazwa kufanyika siku hiyo hiyo. Wapo wanaoona mjadala wa kura umepoteza mvuto na badala yake maandamano yanaibua hisia mpya za kisiasa.

Mchambuzi Issa anabainisha zaidi:

"Wakati fulani mikutano ya kampeni ilikuwa kivutio chenyewe. Vyama vya upinzani vilivyokuwa na nguvu kama CUF na Chadema vilileta hamasa kubwa. Lakini mwaka huu uchaguzi umedorora kiasi fulani tofauti na miaka ya nyuma."

Kwa upande wa chama tawala, CCM, kwao uchaguzi huu umezingatia vigezo na utaratibu wote na ushahidi ni uwepo wa vyama 18 vinavyoshiriki kasoro Chadema. Kwa mantiki hiyo uchaguzi wa mwaka huu usiichukuliwe kirahisi hata kama upinzani hauna nguvu kubwa.

Mgombea wake, Rais Samia Suluhu Hassan, aliwajibu wanaohoji kwanini chama chake kinatumia nguvu kubwa licha ya upinzani kuonekana dhaifu:

"Waswahili wanasema anayedharau mwiba ukimchoma mguu unaota tende. Sasa usisubiri mpaka uchomwe na msumari, hata mwiba lazima uushughulikie."

Kauli hii inatoa picha kwamba CCM bado inaliona jukumu la kampeni kwa wananchi kama jambo la msingi, bila kujali ukubwa au udogo wa changamoto kutoka kwa wapinzani.

Source: BBC Swahili
 
Kwa hiyo kina nape, kitila na vigogo wengine wameamua kukaza kwa nguvu zote kutokudharau upinzani hata kama haupo! Chaguzi za zamani hata UDP ilikuwa na vibe. Huyu Cheyo miaka hiyo alitisha kwa sera yake ya kujaza mapesa mifukoni wananchi mpaka akaitwa mzee wa mapesa. CCM kwenye kampeni za mwaka huu inajijazia nyomi kimkakati halafu inasema wananchi wamejaza uwanja, wanahamasishana wanachama wake kuanzia mashinani wahudhurie kampeni na ndicho watakachofanya kwenye kupiga kura mabalozi watafanya kazi ya kuhamasisha wanachama wao kila nyumba wakapige kura. Ina maana ccm ina uhakika wa kupata kura milioni kumi na tatu za wanachama wake tayari ziko kibindoni, wanachotafuta ni kura za nyongeza tu. Washindani wao kwa ujumla wao hawana nguvu za kupata kura nyingi kwani kuna vyama havijulikani kwa wananchi, huibuka wakati wa uchaguzi tu na havina mashina
 
Ni maajabu makubwa kama wapinzani hawa watapata mbunge hata mmoja! Ni zito tu ndiye anaonekana mpinzani kule kigoma mjini. Kuna miji mabango ya wagombea uraisi wa upinzani hayaonekani kabisa achilia mbali ya ubunge na udiwani. Hizi ni kampeni za aina yake ccm inajitwalia majimbo na kata bila shughuli pevu ila inatumia nguvu nyingi na mbinu nyingi wakati hakuna upinzani. Mwenyekiti wake mstaafu kasema huko kwao pwani hawatachanganya pumba na mchele na kupelekea mikoa mingine nayo kuitikia kauli hiyo nao kusema hawatachanganya pumba na mchele. Sasa hapa hivi vyama shikizi visivyo na upinzani vitapepetewa mbali bila huruma visipate hata diwani ikiwa kauli ya mwenyekiti mstaafu itafanyiwa kazi nchi nzima
 
Mwaka huu kwa mara ya kwanza tunashuhudia ujinga uliokithiri, na maigizo ya Bongo muvi kutamalaki kwenye hicho kitu kinachoitwa uchaguzi.
 
Mwenyewe asiena mpinzani yupo raha kabisa anafurahia hali hii
Anajitekenya na kucheka mwenyewe ila hataakajipitisha kuwa raisi atapata tabu sana kuendesha nchi isiyo na umoja atapata upinzani mkubwa ndani na nnje ya serikali yake.
Ufusadi utakuwa mkubwa sana maana nchi inaongozwa na kikundi cha watu na wengi wanao muunga mkono wanamuunga mkono kwa masrahi yao binafsi.
Tutarajie matajiri kujilimbikizia mali na umaskini kuongezeka kwa kasi yaajabu.
 
Back
Top Bottom