Uchaguzi 2020 Uchaguzi Tarime: Jackson Kangoye afanya sherehe na wajumbe, ni mwendelezo wa kumhujumu Kembaki

Uchaguzi 2020 Uchaguzi Tarime: Jackson Kangoye afanya sherehe na wajumbe, ni mwendelezo wa kumhujumu Kembaki

Musachawenyu

Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
84
Reaction score
109
Jackson Kangoye ambaye alikuwa mshindi wa kura za maoni Tarime na baadae jina lake kukatwa na Kamati kuu na kurudisha jina la mshindi wa pili, Bwana Michael Kembaki, leo hii anafanya sherehe nyumbani kwake na kuwaalika wajumbe wa mkutano mkuu wa Wilaya na baadhi ya wagombea udiwani wa kata za Tarime mjini.

Haijaeleweka mantiki ya kufanya hayo afanyayo katika wakati huu, je ni kuonyesha wajumbe walikuwa sahihi na kamati kuu ilifanya makosa kumkata jina lake?

Au ni kuwaonyesha wajumbe yeye ni mkarimu na bora zaidi kuliko aliyepitishwa na Chama au ni kufanya hujuma kama ambavyo ililipotiwa awali kuwa hatamuunga japo baadae alijitokeza na kukanusha?

Kwa vyovyote vile vitendo anavyovifanya Jackson Kangoye Tarime havina tafsiri nzuri kwa Chama Cha Mapinduzi wala kwa mgombea aliyepitishwa na Chama, Ndugu Michael Kembaki.

Na inaonekana kuna hujuma za chini kwa chini ambazo amepanga kuzifanya ili kuhujumu ushindi wa CCM Tarime Mjini ili kutoa tafsiri kwa Chama kuwa yeye ndio alikubalika na wao walifanya makosa makubwa sana kukata jina lake.
 
sikujuwa kuwa TAARIIME NAKO KUNA WAMBEYA
 
kwaiyo hata sherehe saivi kwa mtu aliyekatwa ni kosa?
 
Back
Top Bottom