Uchaguzi TLS: Ni Mwabukusi vs Nkuba. Serikali imeshatia Mguu

Uchaguzi TLS: Ni Mwabukusi vs Nkuba. Serikali imeshatia Mguu

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Salaam Wakuu,

Pamoja na kwanza Mawakili hasa wa kujitegemea na Wananchi wote wanampenda Mwabukusi, lakini Serikali imeshatia Mguu, Mawakili wote wa Serikali wamelipiwa kwenda Dodoma kupiga Kura.

Na wapo kikazi kwani wamepewa Maelekezo kwamba Nkuba ashindwe.

Kwa siasa za TLS, na Mawakili wanaomuunga mkono Mwabukusi ni wale wa kujitegemea.

Serikali inajua akishinda Mwabukusi, Mafisadi wa Mikataba ya Nchi ndo itakuwa Mwisho wao kwani wengi ndo hao Wanasheria.

Hii ni kutoka na na Msimamo wa Mwabukusu kutaka Mikataba iwe inapelekwa Bungeni kabla ya kusianiwa na kutaka mikata yote iwe wazi kila Mwananchi kuisoma.

Rais Samia alikuwa aende kufungua Mkutanano wa Chama cha Wanasheria lakini baada ya Mwakubukusi kushinda Rufaa Mahakamani akaahilisha na kumtuma Naibu Waziri Mkuu Biteko.

Sasa hivi Mawakili wanaomuunga Mkono Mwabukusi wamenuna na kuanza kulalamika kwamba Serikali inawaua chama cha TLS.

Wanasema hata kama Mwabukusi asiposhinda, ndo rais wao wa Moyoni.

Taasisi zote za Serikali zimepewa Maelekezo Mawakili wote wa Serikalini wakapige kura. Wengine walikuwa wanalalamika kwamba wameambiwa waje hawajapewa per diem. Serikali imeelekeza Per diem watapewa wakirudi kwani limekuwa swala la gafla. Wameambiwa kumpigia Mwabukusi ni kusaliti Serikali.wamelipiwa kila kitu.

Hii pia iliyokea kwa aliyekuwa Hosseah aliyekuwa rais wa TLS.. Serkali ilimtaka wakalipia mawakili wake ambao walilipiwa na akashinda.

Hadi sasa Mwabukusi kushinda ni 69 kwa 51.

Huwezi kushindana na Serikali kwenye Nchi isiyo tenda haki.

Kura zimeanza kupigwa leo saa 12 asubuhi zoezi linaenda hadi saa nne. Wafuasi wa Mwabukusi bado wamelala, sijui jana walilewa?

Mimi namuunga mkono Kapteni.

Pumzika kwa amani Wakili uliyekufa baada ya mkutano kufunguliwa.
 
Mawakili wa serikali si wana umoja wao sijajua kama walisha chagua Rais wao.sasa iweje waingilie na TLS . Mifumo ya Tz ni ya hovyo
 
Mawakili wa serikali si wana umoja wao sijajua kama walisha chagua Rais wao.sasa iweje waingilie na TLS . Mifumo ya Tz ni ya hovyo
Mwenyekiti wao ndo katoa maelezo. Na wot walioenda kupiga kura wanalipiwa na Serikali. Mawakili wa Serikali hawataki Sera, wanataka mtu wao ashinde na kwa wingi huu, wamekuja na nguvu moja.
 
Kitakachotokea ni G z waache waendelee kulindana kwa kuiba mali za Umma..
 
Ndugu figganigga umekwisha jiuliza motive behind ya Mwabukusi kushinda RUFAA Kwa majudge Hawa Hawa wapokea maelekezo?

Kuna move isiyoonekana inafanya KAZI underground.

Tusubiri.
 
Serikali inajua akishinda Mwabukusi, Mafisadi wa Mikataba ya Nchi ndo itakuwa Mwisho wao kwani wengi ndo hao Wanasheria.

Hii ni kutoka na na Msimamo wa Mwabukusu kutaka Mikataba iwe inapelekwa Bungeni kabla ya kusianiwa na kutaka mikata yote iwe wazi kila Mwananchi kuisoma.

.
Kuna ujumbe mzito sana hapa,
 
Kwamba mawakili wa Serikali watamsaliti Nkuba na kumpigia kura Mwabukusi?
ujiulize tu, kwamba mawakili wa serikali walioomba kuungwa kwenye kesi ya mwabukusu dsm hao hao wampigie kura mwabukusu.
 
ujiulize tu, kwamba mawakili wa serikali walioomba kuungwa kwenye kesi ya mwabukusu dsm hao hao wampigie kura mwabukusu.
Naamini serikalinwatashangazwa!!

Hii ni kura ya Utanganyika wetu vs uporaji wa raslimali zetu.
 
Serikali inajua akishinda Mwabukusi, Mafisadi wa Mikataba ya Nchi ndo itakuwa Mwisho wao kwani wengi ndo hao Wanasheria.
Aaah mkuu....Mwabukusi akishinda huko TLS atawafunga jela hao mafisadi ?....
 
NABII mwabukusi ni threat Kwa waovu.
ninaamini wala sio threat kihivyo, ashinde yeye au asishinde yeye, ila rules zibadilishwe mawakili wa serikali wasipige kura, waachwe mawakili wa kujitegemea wapige kura wachague rais wao awe mzuri au mbaya awe wa kwao. mbona mawakili wa serikali wana rais wao? lini mawakili wa kujitegemea wameenda kupiga kura kwa rais wa mawakili wa serikali?
 
Kura wapige wote ndio HAKI.

Muhimu RUSHWA na mashinikizo yasiwepo.
 
Back
Top Bottom