Uchaguzi vyuo vikuu

Wangooto

Member
Joined
Feb 1, 2013
Posts
20
Reaction score
5
Ndani ya wiki kama mbili zilizopita vyuo vingi vya elimu ya juu nchini vimekuwa vikifanya chaguzi mbalimbali ili kujipatia viongozi watakao waongoza kwa misingi ya sheria na utawala bora katika serikali za wanafunzi. katika chaguzi hizi vijana huanza kuonekana nyota zao kisiasa kwani umaarufu wao huanza kupatikana katika kipindi hiki ambacho wao huwa vyuoni.
Habari hii imejiegemeza katika Chuo Kikuu cha Dodoma ambapo zoezi hili limemalizika jana na washindi kutangazwa na tume ya uchaguzi ya chuo hicho mida ya saa tatu na nusu usiku. Chuo Kikuu cha Dodoma kina college 6 ambazo ni college of Education, college of Humanities and Social Science, college of Informatics and Virtual Education, college of natural sciences and mathematics, college of mines and petroleum engineering na college of health and allied sciences.
lakini miongoni mwa hizo college zote college iliyokaa kisiasa zaidi ni SOCIAL SCIENCES AND HUMANITIES. ambapo democrasia na ukomavu wa kisiasa huonekana mara kwa mara katika chaguzi zao. mwaka huu umekuwa wa kihistiria baada Mr. Bernard, Janus kushinda kwa kishindo na chaguzi huo uliogubikwa na fitina, majungu na uhasama wa hali ya juu dhidi yake lakini kupitia sera zake amawashawishi mamia ya wanafunzi katika kitivo hicho kujitokeza na kupiga kura kwa wingi. Na kuwa dhihirishia wapinzani wake kuwa yeye ni mkomavu wa siasa na anakubalika. mamia ya wanafunzi skuli ya sanaa na lugha walikesha wakishangili ushindi wake kwakishindo. nina mtakia mujumu mema katika serikali yake.
 
Nani kashinda?

MaCCM hayajaleta mnuso?
 
Nasikia ,masisiem yamemwaga 2 milion...nani kashinda mkuu???
 
Mkuu Wangooto,


Nasikia kulikuwa na itikadi za vyama (CCM & CDM) Huyo aliyeshinda alikuwa upande gani?
 
Je Haki imeshinda dhidi ya Dhuluma , au Ufisadi wa Mil 2 umetamalaki ?
 
Kuna habari nimezipata kuna dogo mmoja hapo udom anaitwa kiringo yeye ni bingwa wa siasa za udini hapo chuo kuna jamaa yangu anafanya kazi hapo amenitonya kuwa yeye na mgombea wake walipewa na shehe mkuu wa mkoa wa dodoma laki 6 ili ziwasaidie katika ujinga wao ni kweli haya?
 
ukiona hivyo ujue magamba wametumia mwanya huo wa udini,halafu baadae wanapiga vijembe CDM.
 
Acha ujinga dogo naomba mtupe sababu za kuwaengua PHILIPO MERCY, KALANDA GILBERT.M.,CHAMA WILLIAM ktk nafasi ya urais na baada ya wao kuamua kumuunga mkono mgombea JAPHARY OTIENO KHATEMBO nae mkamuengua asubuhi jana siku ya uchaguzi ili kufanikisha malengo yenu ya waliowatuma chini ya usimamizi wa dharimu NZAMBA NASSA kama mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kupandikiza mashushu (bernard janus na mwenzake william denis aliyewekwa kama kiini macho)
 
Mkuu Wangooto,


Nasikia kulikuwa na itikadi za vyama (CCM & CDM) Huyo aliyeshinda alikuwa upande gani?
Ni gamba makamanda wote walienguliwa kwa nguvu na wengine kuzuiwa kushiriki kabisa kampeni na NZAMBA NASSA mwenyekiti wa tume ambaye pia ni kada mzuri na kiongozi wa CCM anayejipambanua kama mtu mwenye nguvu nyingi za watawala, kijana mmoja mwenye jeuri hivi isyokuwa na mashiko yoyote
 

Watoto wa udom mnamambo ndio maana tunasema chuo chenu ni cha kata hata wanafunzi akili zenu zimekaa kikata kata tu nasikia hao madogo wengine walifoji g.p.a ili waweze kugombea na pia sio kilaunayemtaka lazima apite hata kama hana vigezo mimi nimeumia sana kusikia huyo mzanzibar kiringo mtoto wa yule jamaa wa zanzibar mwenye skendo chafu kuwa ni bingwa wa udini juzi nilikuwa nimekuja dodoma kwenye majumuisho ya wizara yangu jamaa angu akawa ananippa habari yeye anafanya kazi hapo dogo lengo lake lilikuwa atawale mwisilamu na yeye ndio aliomba pesa kwa shehe wa mkoa nasikia hata huko wanakoswalia alikuwa anaendeleza kura za udini
 
Yaani akishinda mtu wa ccm ni kosa? mbona hatupendi kukubali maamuzi ya wengi? Kama ameenguliwa basi msipige kura ili ijulikane kuwa dhuluma imeleta utata uchaguzi uanze upya. Tuana lalamika huku tunapiga kura. Tujenge tabia ya kukubali uhalisia. Ooooh je ni ccm au kamanda? hili swali ni la kitoto sana tena linafaaa kuleklee kwa kina mheshimiwa naniliuuuu.
 

Katika swala la udini hassan kilingo ni kiongozi wao,amejaa fitina na ujinga,yuko mwaka wa tatu sheria lakini hana chochote anachojua zaidi ya quran na kuwaita wenzake makafiri,mjinga sana huyu
 

Tume ya uchaguzi imejaa watu wababe,wakiongozwa na NZAMBA NASSA na DAVID MUYA wote wanasheria mwaka wa nne,kuna watu walitishwa mpaka wakajiengua wenyewe,kila aliyegusia udhaifu wa utawala ktk kampeni alinyofolowa,tulikuwa na imani kubwa na tume ila kikwazo ni kuongozwa na kada wa CCM NZAMBA NASSA..
 
Katika swala la udini hassan kilingo ni kiongozi wao,amejaa fitina na ujinga,yuko mwaka wa tatu sheria lakini hana chochote anachojua zaidi ya quran na kuwaita wenzake makafiri,mjinga sana huyu
Nilipopata hii habari nilisikitika sana hapo ndipo mnapokiuwa chuo chenu kijana kama huyo ni kirusi kwenye jamii anasoma sheria ama sharia? mngeunganika kwa pamoja mkapopoa hata mawe sisi enzi zetu wakati nipo pale univeristy of khartoom japo nchi ile waislamu wengi lakini mambo haya hayakuwepo kabisa
Maana jamaa aliniambia kuwa yeye ukiwa mkristo ni adui yake na wajinga mnaolubali kumfuata huyo mtoto wa mzee kilingo wa zenji like fathet like son
 

Mkuu sula la kufojiGPA ni uongo wa NZAMBA NASSA na mwenzake DAVID MUYA hawa maparal legal ndio walioeneza hizo habari baada ya kuona kila mtu UDOM anawazungumzia vibaya na kuwalaani sasa ikawa ni ground ya kutaka kujishafisha tu mbele ya macho ya watu. Ila ukweli ni kwamba wameletewa mapesa na sisiem wahakikishe kwa gharama yoyote ile wanapitisha CCM ndio maana walipoona kijana anaitwa OTTIENO ampata nguvu baada ya kuungwa mkono na wale walioondolewa kwa hila naye wakamwondoa jpili asubuhi siku ya uchaguzi
 
hivi mpaka viranja eti siasa za udini au vyama!!! hahahaah!!!!! tena afadhali hata vyuo vya umma, vingine rais huna cha kuhoji kuhusu mambo nyeti...........poleni watu wa chuo fulani Arusha maana uongozi wenu hauna tija labda uwe unahudhuria chapel tu.
 

vigezo vya kugombea urais kwa udom vipi? na je walioenguliwa walitimiza mbona hutuambii kwa uwazi dogo?
 
Tume ile ile imetangaza nafasi ya uspika na naibu spika leo! Kazi inakwenda
 
Huyu jamaa anaonekana huwa hajihusishi na siasa ndani ya chuo kwani hajawahi onekana kwenye vikao vya chama chochote ila ni mwanaharakati kwelikweli na anajua kujenga hoja ndio maana amekubalika wapinzani wake walipoona anawashinda kwa hoja wakaanza kumchafua kwa kutumia neno ati ni kada wa chama cha mapinduzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…