Uchaguzi wa 2020, Kukumbuka shuka kumekucha, is it too little too late kwa CHADEMA or better late than never?

-Umesahau kuwa walizuiliwa kufanya siasa?
-Umesahau kuwa wanabambikiziwa kesi kwa makusudi na hiyo hiyo serikali ya CCM?
-Kama kitetea haki za kiraia kwa watanzania ni kuwa nje ya kazi za chama cha siasa,basi naona wewe kichwani hauko sawa!
 
Mada nzuri mno ila bado inajionyesha ni jinsi gani middle class ya Tanzania inapojifanya haiishi ndani ya nchi na kujionea nini kinafanyika on the ground,tumekua waoga,mashujaa wa kwenye key boards,na wingi wa maoni yanayojionyesha tunaishi maisha ya tofauti;kuingia kwa awamu hii tumeshuhudia mkandamizo mkubwa wa kisiasa,haki za binadamu,freedom of press(bila JF hakuna chombo chochote kilicho huru),freedom of expression etc etc,sasa kuja na mada kama hii wakati tunajua kutakuwa hakuna uchaguzi mwaka huu ni kuonyesha ni jinsi gani tumepata elimu but sio elimu ya kusoma to understand;uchaguzi mwaka huu HAKUNA,(refer ule wa serikali za mitaa!!!),kuongelea uchaguzi wakati tunatambua haupo ni kulikosea heshima jukwaa hili,huwezi kuwa ni mwenyekiti wa chama cha kisiasa kinachoshiriki uchaguzi na ukajichagulia mwamuzi wako,its a bushit.
 
Kama kweli ni mfuatiliaji wa mambo ya kisiasa tangu Magufuli ameingia madarakani shughuri za kisiasa zilisitishwa kwa upande wa upinzani, upande wa CCM waliendelea kufanya siasa nchi nzima kama kawaida.

Wapinzani waliachiwa kipengere kimoja cha kufanya siasa katika maeneo walioshinda nafasi ya ubunge lakini napo walikuwa hawapewi uhuru wa kufanya mikutano katika majimbo yao.

Kwa kunyimwa kibali cha polisi, kukamatwa kwa makosa ya kubambikizwa kwa kigezo cha kwamba walikuwa wanatumia maneno ya uchochezi wakati wanahutubia mikutano yao,wakati mwingine wanazuiwa kabisa kufanya mikutano ya kwa kitu kinachosemwa taarifa za kintelejensia.

Kitu cha kusikitisha zaidi waziri mkuu akiwa bungeni alijibu kuwa kuna uhuru wa kufanya mikutano kwa wanasiasa katika maeneo yao baada ya kuulizwa swali na Mbowe, haikupita muda mrefu baada ya waziri mkuu kujibu hivyo wabunge wa upinzani katika maeneo yao walizuia kufanya mikutano.

Kinachoonekana zaidi hapa katika kuruhusu wanasiasa kufanya mikutano katika maeneo yao pia ndani yake kulikuwa na mpango wa kutumia mikutano hiyohiyo kuwapeleka wapinzani jela.

Mtego ambao wapinzani waliung'amua na wakaukwepa kwa kupunguza kufanya mikutano yao ili wasije wakaishia jela na sasa hivi wameamua kuanza mikutano kwa kuwa wanasababu moja kubwa ya kuwaeleza wabambika kesi kuwa 2020 ndo mwaka rasimi uliotangazwa na rais kuwa ni mwaka wa kufanya siasa.
 
Hizo sshughuli za kisiasa wangezifanyia ulaya? Utasema wabunge wameruhusiwa kufanya, ni mara ngapi umesikia intellegicia ya kipolisi ikikataza hata hiyo mikutano ya wabunge, na vile vile pia ishu ya kutangaza sera za chama sio za mbunge peke yake, hao waliotakiwa kuzitangaza hawaruhusiwi kusimama majukwaani huku wale wa Ccm wakiruhusiwa.

Unamkataza mpinzani wako kufanya mazoezi kabla ya pambano alafu ikifika siku ya pambano unampiga na unaanza kumkashifu kuwa alikuwa hajajiandaa na pambano alafu una toka hapo unaanza kushangilia kama
MAZUZU ya ccm
 
Ngoja wakuite MSALITI, MCHUMIA TUMBO, MSAKA VYEO(TEUZI) nahisi unawafahamu vizuri.
 
Sahihi kabisa, alafu wapumbavu wachache wanasema upinzani hawataki kutangaza sera zao wanapenda kulumbana na polisi tu.

Unashindwa kujiuliza hizo sera watazitangazia wapi
 
Chadema labda Urais wamsimamishe tena Mbowe kama wanaweza

Tofauti na hapo sioni hata wa kuchuana na yule mtu wa Chato,sioni.
Kwa muundo wa tume ya uchaguzi ulivyo, hata aje malaika kugombea dhidi ya ccm hawezi kushinda.
Refer kilichotokea zanzibar 2015
 
Nyie wasukuma ndio mlioiharibu hii nchi kwa ushamba na ukabila wenu hasa kwa kupenda sifa kuliko maiti
 
Ndugu yangu Paskali,
Kutaka kila unachoshauri kifuatwee na upinzani ni udhaifu. Hivibado hujagundua kuwa tatizo ni wewe hauaminiki tena.
Sheria/katiba ya nchi zinapovunjwa mchana, kweupe, hadharani twakuona unavyojikausha. Yawezekana ni ili kutunza tenda zako za kutangaza na kuendesha 'MAONESHO YOTE' ya kiserikali na labda uteuzi. Bunsen Burner nae alikuwa akilia kilio cha mamba hivyohivyo kama wewe.
POLE, ushauri wako watia shaka, hauhitajiki tena peleka kungine.
Amen.
 
Kwani washaruhusiwa kufanya shughuli za siasa ?
Mkuu achana na huyo mnafiki aliyepuuzwa na kila mtu humu jf , huyu anaomba kila siku chadema iuawe , sasa anapoandika upuuzi wake kuhusu Chadema watu wanamchora tu .

Huyu ni miongoni mwa watanzania watano waliofurahishwa na shambulio la Lissu , japo kwa kificho kificho , nadhani anaamini ataishi milele
 
Apo ndo naanza kumuelewa
 
Umesoma ukaelewa kilichoandikwa?,au hujasoma Kama ilivyo ada ya watanzania wavivu kusoma ,hivyo umechangia bila kusoma
Yeye nahisi yawezekana hajui au ni kama mimi ambaye nimesoma na sijaelewa anamaanisha nini , yeye sio wewe au wewe umesoma na kuelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…