Uchaguzi wa 2020, Kukumbuka shuka kumekucha, is it too little too late kwa CHADEMA or better late than never?

Uharo tu huu. Tunataka mazingira sawa ya kufanya siasa ndipo uandike uharo huu na utakuwa na substance. Chama miaka 5 hakijafanya siasa, then unaadika uharo huu!
 
Uharo tu huu. Tunataka mazingira sawa ya kufanya siasa ndipo uandike uharo huu na utakuwa na substance. Chama miaka 5 hakijafanya siasa, then unaadika uharo huu!
Basi basi pole kama amekuudhi msamehe labda anaishi nje ya nchi
 
-Umesahau kuwa walizuiliwa kufanya siasa?
-Umesahau kuwa wanabambikiziwa kesi kwa makusudi na hiyo hiyo serikali ya CCM?
-Kama kitetea haki za kiraia kwa watanzania ni kuwa nje ya kazi za chama cha siasa,basi naona wewe kichwani hauko sawa!
Nisawa na Mzazi aliyebize na kazi na kutafuta pesa, halafu anasahu kufuatilia maendeleo ya wanawe shuleni. Hayo yote uliyoyataja yamewazuia kumtafuta na kumuaanda mashindani wa magufuli. Wangegawana kazi/majukumu na kila idara ingekuwa na nguvu.
 
Kugawana majukumu ndio ufanisi wa kila kitu. Chama kama kiliyafahamu hayo yote na hakijatafuta mbinu mbadala ya kutangaza sera zake basi kunashida sana. Mapema sana kingeanza mchakato wa kupata mgombea wao leo hii tungemfahamu, kuna magazeti, radio, tv na mitandao ya jamii, yote hii inatosha Watanzania kupata taarifa.
Sababu hata mkutano wa hadhara ukifanyika Kigoma mimi niliye Lindi napata taarifa kupitia hizo media. Kwahiyo kuzuia mikutano ya siasa sio sababu ya kujitetea, wakati iunafamu kabisa kuwa mikutano imezuiwa.
 
Unaandika kana kwamba ujui kinachoendelea hapa Tanzania

Na nikwanini mmoja aachiwe uhuru wa kuzunguka na kutangaza sera yake na mwingine imlazimu kutafuta njia mmbadala?

Katibu wenu kasema wao wanatumia dola kulinda maslahi yao na kuhakikisha hakuna mpinzani anayefurukuta kwa namna yoyote ile, hizo mbinu mbadala ambazo dola ingeziacha chadema wazitumie sijui ni zipi
 
Huku kwenye siasa ni mweupe kichwani.We sikiliza tu unayoambiwa hapo WCB uje utuletee nondo kule Jukwaa la Celebrity ila huku unapotea.Au hata kama WCB wote ni ccm ila sasa ndo maana huoni wanajadili kwa uwazi mambo ya Kuipinga CDM au ACT
Siumesikia mwenyekiti wa chadema atampokea Membe akija chadema hapa inaonesha hiki chama hakina future

Sent using Jamii Forums mobile app
 

..huko mahakamani wanajipeleka wenyewe?

..au wanapelekwa na vyombo vya dola ambavyo Dr.Bashiru alisema ni mali ya ccm?
 
Ccm imeshindwa kuua chadema na imeshangaa kuona chadema.bado hai hai 2020.

Wamepaniki wanaanza kuhaha wakati kumekucha sijui tutatumia dola kushinda..

Chama kizee kama ccm kitategemeaje kupita kwa mbeleko ya pilice na vyombo vingine vya dola?

Bashiru anatakiwa kuwaomba radhi wote ambao wanahusika na dola kwa sababu chama kizee kama ccm kilitakiwa kishinde kwa sera na utekelezaji wake.


Hadi march 2020 bado wanatumia police kuvuruga mikutano ya wabunge wa hadema

Chadema hata bila mbowe kipo imara sana.

Vijana tupo na chadema

Chadema mpango wa Mungu.

Kama hupendi chadema, usitukane , tafuta maji ya suma JKT glass moja utajiridhisha.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila ccm na Magufuli yani na kutetea kote huku Kwa ndugu yetu paskal mpaka anajitoa akili anakuwa kama zuzu lakini bado Magufuli hamteuwi tu.Hivi makada wa CCM hapo Lumumba ambao kila siku wapo humu kuandika upupu lakini wanambania pascal nafasi wanapewa kina polepole wakati kuna mropokaji huku.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chukua koja hapo nitalipia.. umeongea point sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukumbuke hata hao wambunge walipokua wakihutubia kwenye majimbo yao waliletewa fujo na mikutano kuzuiwa kwa kisingizio hofu ya kuhatarisha aman, hata mwenyekit juz kafanya mkutano jimbon kwake mkutano umekuja kuvurugwa na polisi, hata mikutano ya ndan ya chama imekua haiwezekan au kufanyika kwa mbinde. Taifa linakosa mwelekeo, taifa la vyama ving lakin kimoja tu ndo kinaruhusiwa kufanya siasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo una mawazo kuwa wapinzani ni viongozi wa upinzani

Wapinzani ni sisi wananchi, kama sio mpinzani basi wewe ni ccm.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na pia sera nyingi za chadema zimetekelezwa kimya kimya na ccm wakiogopa wanachedena ambao ni wengi kuliko wana ccm.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata maeneno waliyoshinda ilikua ni marufuku. Umeona ile clip heche akikataliwa na police kuto fanya mkutano na wananchi wake.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema ilipoteza mwelekeo tangu DR. Slaa aondoke chadema.
DR. SLaa alikuwa katibu makini kuliko, ambaye alikiimarisha chama kila idara, baaada ya hapo chadema ilipoteza dira hadi sasa.... Ndio wanakbuka shuka jua la utosi!!!
 
Najua mkuu unapenda sana kuchomekea chomekea na kiingereza kidogo. But nadhani ungeachana nacho ili tudumishe kiswahili tu.

"This is a good, hatimay chadema......"
Hiki ni kiingereza kibovu.huwa naona mara nyingi kwenye mabandiko yako.mi nadhani si lazima sana kutumia english.tupe michapo kwa kiswahili chetu watanzania.tutakuelewa vizuri.

Natumaini ombi langu litakubaliwa.

Wako katika ujenzi wa Taifa
Komeo lachuma.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…