Pre GE2025 Uchaguzi wa BAWACHA nafasi ya Mwenyekiti kurudiwa baada ya wagombea wote kushindwa kufikia asilimia 50 ya kura zilizopigwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Uchaguzi wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) kwa nafasi ya Mwenyekiti unatarajiwa kurudiwa baada ya wagombea wote kushindwa kufikia asilimia 50 ya kura zilizopigwa.

Kulingana na kanuni za uchaguzi wa chama hicho, wagombea wawili wa juu watachuana tena katika duru ya pili ili kumpata mshindi.

Soma Pia: Uzi maalumu wa matokeo Uchaguzi wa Baraza la Vijana (BAVICHA) na Baraza la Wazee (BAZECHA) na wanawake (BAWACHA) CHADEMA Taifa 2025

Taarifa za awali tulizonazo ni kwamba katika kinyang'anyiro hicho Sharifa Suleiman anaongoza kwa kura 164 akifuatiwa na Celestine Simba aliyepata kura 116 kisha Suzan Kiwanga. Hata hivyo wote hawakufikisha asilimia 50

Kwa mujibu wa taratibu za CHADEMA, wagombea wawili walioongoza kwa kura ndio watakaopambana kwenye awamu ya pili, ambapo mshindi atapatikana kwa wingi wa kura.
 
Uchaguzi wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) kwa nafasi ya Mwenyekiti unatarajiwa kurudiwa baada ya wagombea wote kushindwa kufikia asilimia 50 ya kura zilizopigwa.

Kulingana na kanuni za uchaguzi wa chama hicho, wagombea wawili wa juu watachuana tena katika duru ya pili ili kumpata mshindi.

Taarifa za awali tulizonazo ni kwamba katika kinyang'anyiro hicho Sharifa Suleiman anaongoza kwa kura 164 akifuatiwa na Celestine Simba aliyepata kura 116 kisha Suzan Kiwanga. Hata hivyo wote hawakufikisha asilimia 50

Kwa mujibu wa taratibu za CHADEMA, wagombea wawili walioongoza kwa kura ndio watakaopambana kwenye awamu ya pili, ambapo mshindi atapatikana kwa wingi wa kura.
Hapo Bi Sharifa kashashinda!! Huyo Celestine Simba u team Lissu umemponza!! Nilimheshimu sana huyu mama lkn kitendo chake cha kushabikia wahuni nimemdharau sana!
 
Ningejiunga nanyi ningepata asilimia 90+ zinge baki za wagombea tu.

😅😅😅
 
Wakuu,

1737148103825.png

Uchaguzi wa nafasi ya uenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) na Makamu Mwenyekiti bara unarudiwa.

Hatua hiyo ni baada ya kukosekana mgombea aliyepata asilimia 50 au zaidi ya kura zote.

Wagombea wa nafasi ya uenyekiti ni Sharifa Suleiman aliyepata kura 167, Celestine Simba 116, huku Suzan Kiwanga akipata kura 100.

Kwa sababu hiyo, Sharifa na Celestine,watapigiwa tena kura na wajumbe.

Kwa upande wa makamu mwenyekiti Bara, wagombea walikuwa Moza Ally, Agnes Chilulumo, Elizabeth Mwakimomo, Marietha Chenyenge, Naomi Ndigile, Rose Mkonyi na Salma Kasanzu.

Wanaorudia kupigiwa kura ni Salma na Elizabeth.
 
Hapo Bi Sharifa kashashinda!! Huyo Celestine Simba u team Lissu umemponza!! Nilimheshimu sana huyu mama lkn kitendo chake cha kushabikia wahuni nimemdharau sana!
Kwani we nani? Machawa wa ccm ndio haohao machawa wa mbowe.
Lazima tuchukue hatua kuokoa chama chetu
 
Wakuu,

Uchaguzi wa nafasi ya uenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) na Makamu Mwenyekiti bara unarudiwa.

Hatua hiyo ni baada ya kukosekana mgombea aliyepata asilimia 50 au zaidi ya kura zote.

Wagombea wa nafasi ya uenyekiti ni Sharifa Suleiman aliyepata kura 167, Celestine Simba 116, huku Suzan Kiwanga akipata kura 100.

Kwa sababu hiyo, Sharifa na Celestine,watapigiwa tena kura na wajumbe.

Kwa upande wa makamu mwenyekiti Bara, wagombea walikuwa Moza Ally, Agnes Chilulumo, Elizabeth Mwakimomo, Marietha Chenyenge, Naomi Ndigile, Rose Mkonyi na Salma Kasanzu.

Wanaorudia kupigiwa kura ni Salma na Elizabeth.
Ili kubalance dini na ukanda wajumbe mpeni kura bi Sharifa!! Walau kaonesha ukomavu na busara!
 
Back
Top Bottom