GE2025 Uchaguzi wa Belarus 2020 unataka kuwa na ufanano na uchaguzi wa Tanzania 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
457
Reaction score
773
Rais wa Belarus, Alexander Lukashenko amekuwa madarakani tangu 1994. Katika Uchaguzi wa 2020 aliona kabisa angeweza kuondolewa madarakani kutokana na kukubalika kwa mpinzani wake Syarhei Tsikhanouski. Syarhei Tsikhanouski alikamatwa na kufungwa siku mbili baada ya kutangaza nia yake ya kugombea urais wa Belarus, ilikuwa wazi kuwa Rais Lukashenko hakutaka upinzani.

Mke wa Tsikhanouski, anayetambulika kama Sviatlana Tsikhanouskaya aliangalia Katiba na kuona inamruhusu hata yeye kugombea urais na kuendeleza harakati za mumewe. Rais Lukashenko Aliona mwanamke hawezi kumshinda, hata hivyo hali ilikuwa tete maana huyu mama alishinda japo mshindi alitangazwa Lukashenko. Sviatlana ilibidi aende uhamishoni Lithuania na baadae akaendelea na harakati zake nje ya Belarus, hadi sasa nchi 20 zinamtambua kama rais japo Lukashenko ameendelea kutawala Belarus.

Ikumbukwe Lukashenko ndio rais aliyekaa madarakani kwa muda mrefu kwa marais wote wa Ulaya.

Kushinda kwa Sviatlana Tsikhanouskaya kama Rais wa Belarus kulifanya watu wengi waingie matatani maana watu wengi walikuwa wakikamatwa na waliokuwa na Bahati walikimbia nchi yao kuenda Lithuania, Poland nk. Je stori hii inaweza kuwa na ufanano na stori ya uchaguzi wa Tanzania 2025?

Nawasilisha.
 
Huku Bongo ni vile tu sisi wenyewe tupo usingizi wa pono. Tungeamka kutoka usingizini na kuipinga dhuluma kwa vitendo, hakika mabadiliko ya kweli yangepatikana.
 
Rais wa Belarus, Alexander Lukashenko amekuwa madarakani tangu 1994. Katika Uchaguzi wa 2020 aliona kabisa angeweza kuondolewa madarakani kutokana na kukubalika kwa mpinzani wake Syarhei Tsikhanouski. Syarhei Tsikhanouski alikamatwa na kufungwa siku mbili baada ya kutangaza nia yake ya kugombea urais wa Belarus, ilikuwa wazi kuwa Rais Lukashenko hakutaka upinzani.

Mke wa Tsikhanouski, anayetambulika kama Sviatlana Tsikhanouskaya aliangalia Katiba na kuona inamruhusu hata yeye kugombea urais na kuendeleza harakati za mumewe. Rais Lukashenko Aliona mwanamke hawezi kumshinda, hata hivyo hali ilikuwa tete maana huyu mama alishinda japo mshindi alitangazwa Lukashenko. Sviatlana ilibidi aende uhamishoni Lithuania na baadae akaendelea na harakati zake nje ya Belarus, hadi sasa nchi 20 zinamtambua kama rais japo Lukashenko ameendelea kutawala Belarus.

Ikumbukwe Lukashenko ndio rais aliyekaa madarakani kwa muda mrefu kwa marais wote wa Ulaya.

Kushinda kwa Sviatlana Tsikhanouskaya kama Rais wa Belarus kulifanya watu wengi waingie matatani maana watu wengi walikuwa wakikamatwa na waliokuwa na Bahati walikimbia nchi yao kuenda Lithuania, Poland nk. Je stori hii inaweza kuwa na ufanano na stori ya uchaguzi wa Tanzania 2025?

Nawasilisha.

Tofauti tu ji kuwa hii Tume ya Maza haiwezi kutangaza matokeobya ukweli.

By the way, CCM haijawahi kushinda uchaguzi Tanzania tangu 2010. Wanachokifanya ni kuchakachua matokeo kwa namna wanavyofikiri kutegemea na wakati na kujitangaza.
 
Back
Top Bottom