Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Kwenye uchaguzi unaoendelea nchi nzima huko CCM, mambo yanayotendwa ni mazito kuliko mnavyosikia, ni hatari na balaa kubwa, hali iliyoko huko kwenye chaguzi za Mikoa inatengeneza uhasama wa Milele, watu wanasingiziana hadi Ukimwi hadharani.
Huko Kilimanjaro, Mmoja wa Wagombea wa Uenyekiti wa Mkoa, ndugu Alphonce Temba wakati wa kujieleza , alikumbana na swali la Mjumbe 'aliyepangwa' ambaye alimuuliza kwamba kwanini anagombea uenyekiti wa Mkoa wakati mwaka 2018 alitangazwa kuwa ni Kichaa? Swali hilo la uongo lilizua taharuki, huku msimamizi wa Uchaguzi huo aliyejulikana kwa jina la Mrindoko, akimzuia Temba kujibu kwa madai kwamba hilo siyo swali (mbinu ya kum disqualify), kuzuiwa huku kwa mchongo kulifanya Wajumbe waamini kwamba Temba ni kichaa na hivyo kumnyima kura.
Sasa unaweza kuona mambo yanayofanyika kwenye chaguzi hizo, kuna wagombea wamesingiziwa mpaka Ukimwi ukumbini , wengine wametajiwa hadi idadi ya wanaume waliotembea nao na majina yao kwenye mikutano ya uchaguzi ili kuaminisha Wajumbe wasichague Malaya, kama hali ya ccm imefikia hapo ni wazi sasa WATANZANIA ANZENI KUPIGA VIGEREGERE, maana wameanza kutafunana wenyewe.
Nukuu: WANACCM HAWAACHIANI MAJI YA KUNYWA MEZANI - KIKWETE