Uchaguzi wa CWT wilaya ya Butiama utazamwe na TAKUKURU
Kuna tetesi kuwa mchakato wa uchaguzi wa CWT katika wilaya hiyo umegubikwa na visa vingi vinavyokiuka taratibu za uchaguzi.
Mojawapo ya visa hivyo ni pamoja na usambaji wa fomu kwa wagombea ngazi ya matawi unaoambatana na kupewa kiasi fulani cha pesa.
Tunaiomba TAKUKURU imulike uchaguzi huo.
Walimu walipaswa kuonesha mfano halisi wa demokrasia. Badala yake mwenyekiti na team yake wanafanya mambo yasiyoeleweka. Mambo ni pamoja utoaji wa hongo kwa wawakilishi wa matawi, matumizi mabaya ya fedha za chama na rasilimali nyingine.
Moderator tafafdhali naomba hii thread msiifiche.