Uchaguzi wa kumpata Naibu Spika kufanyika Februari 11, 2022. Vyama vyakaribishwa kuwasilisha majina ya Wagombea

Anakula uteuzi chap kwa haraka🏃🏃
Nafasi za Rais kuteua wabunge (hasa wa kiume) zimeshakwisha mzee.
Ameshateua watano kama ifuatavyo:-

1. Dr. Bashiru Ally Kakurwa
2. Humfrey Polepole
3. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk
4. Dr. Leonard Chamuriho
5. Prof. Shukran Manya

Orodha nzima inawajumuisha pia:-
6. Riziki Lulida
7. Dr. Dorothy Gwajima
8. Dr. Stergomena Tax
9. Balozi Liberata Mulamula.
10. Nafasi hii ni kwa ajili ya mwanamke
 
10. Anjella Kairuki

Ni swala la muda tu!
 
Spika sio lazima awe mbunge, angeweza kuwa hata Mwijaku.

Naibu spika ni lazima awe mbunge, ndio maana masharti yanasomeka hivyo.
Sasa naona waki tumiwa kina Mdee kuonyesha demokrasia komavu iliyoko Tanzania.
Yaani vituko haviishi...
Ccm watafika mbinguni wakiwa wamechoka sana
 
Kila chama chenye uwakilishi bungeni!!! Hivi wale wa TLP juzi walikuwa na wawakilishi bungeni??
Tuna hitaji KATIBA MPYA!!!
Kwa nafasi ya Spika nadhani kanuni zake ni tofauti na hii ya unaibu spika.
 
Haya brother Pascal Mayala tutabirie tena hapa kama ulivyo tutabiria kwa Tulia ambae alikua Naibu Spika kua atakua Spika!? Mziko uko nani atakua Naibu wake!?
 

Bunge lafungua milango kwa nafasi ya Naibu Spika​



=====
Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi ametangaza nafasi ya Naibu Spika wa Bunge kuwa wazi akivitaka vyama vyenye uwakilishi bungeni kuteua wagombea watakaowania nafasi hiyo.

Hatua hiyo inakuja kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson aliyeteuliwa na CCM kugombea nafasi ya uspika na baadaye kushinda uchaguzi wa kuongoza mhimili huo.

Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano cha bunge leo Februari 3 imesema Wabunge watafanya uchaguzi wa nafasi hiyo Ijumaa Februari 11, 2022 na kwamba vyama vyenye uwakilishi bungeni vinatakiwa kutuma majina ya wagombea wao kwa Katibu wa Bunge kabla ya saa 10 jioni ya Februari 10, 2022.

Katibu wa Bunge amesema katika taarifa hiyo kuwa, Dk Tulia alijiuzulu kwa mujibu wa ibara ya 149 (I) (C) na (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Ibara ya 85 (3) (b) na 86 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema, uchaguzi utafanyika haraka iwezekanavyo mara kiti hicho kitakapokuwa wazi," inasema taarifa hiyo.

Chaguzi zote katika mhimili huo zinakuja kufuatia kujihuzuru kwa aliyekuwa Spika wa Bunge Job Ndugai Januari 6, 2022 na mchakato ukaanza kwenye vyama vya siasa.

Tofauti na uchaguzi wa Spika ambao anaweza kugombea mtu kutoka nje ya bunge, sheria inaelekeza nafasi ya Naibu Spika lazima itokane na mmoja wa wabunge.
 
Hii Nafasi ya unaibu spika ilikuwa wazi siku nyingi sana. Hii nafasi kutangazwa sasa ni kuanika ujinga wetu hadhari.
 
Hii Nafasi ya unaibu spika ilikuwa wazi siku nyingi sana. Hii nafasi kutangazwa sasa ni kuanika ujinga wetu hadharani.

Hii nchi kuendelea itachukua miaka mingi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…