Elections 2015 Uchaguzi wa Marejeo Zanzibar ni Huru na Haki! Tuyasubiri Matokeo, Tuyakubali!

Ha ha ha. Mzee Mohamed Said katika ubora wake.
Chaza,
Wakati wetu hivi ndivyi vitabu tukisomeshwa tukijifunza lugha.
Huyu Alice alimuoma sungura wa ajabu akaamua kumkimbiza.

Sungura akaingia katika shimo na Alice akamfuata kwenye shimo.
Hapo ndipo mikasa ya Alice ilipoanza.

Unaonaje mikasa ya CCM Zanzibar?
Wako kwenye kura peke yao wanasema watashinda kwa kishindo.

Wakifanya uchaguzi na watu saizi yao wanafuta uchaguzi baada ya
kupigwa mwereka.

Huu ni mwanzo.
Hii movie itakuwa na ''sequel.''

We subiri.
 
Kilichofanyika Zanzibar ni kama sensa, Sensa ya wana CCM, ili chama kijue kina washabiki wangapi baasi, lakini ule siyo uchaguzi wa hadhi ya uchaguzi!. Pasco haupo sahihi katika hili hata kama ulichukia CUF kutokufuata ushauri wako wa kwenda mahakamani wakati unajua majaji wa kule Zanzibar wanateuliwa na nani,na wana muelekeo gani katika maamuzi.
Wakati mwingine kwenda mahakamani ni mtego wa wababe kukudhulumu haki yako "kisheria"
 
Pasco,ni.masuala gani ya msingi yaliyotokea 25 Dec.2015 ambayo yalifanya uchaguzi urudiwe kwa upande wa Rais wa Zanzibar tu na si kwa upande wa pili wa Rais wa Muungano?
 
Eti ZEC ni impartial and balanced system! Usiwe una download na kupaste usivyovielewa.
Pasco ni askofu anayepigania kuwa mchawi ili apate hela zaidi ya sadaka!
 


Nani kaupinga sio wa haki?
 
Ndio maana nilianzisha uzi nikashauri waandishi wa habari wasipewa nafasi za uteuzi.
kwa sababu wanaitumia taaluma yao vibaya kumpamba mtu fulani au chama fulani na kumponda mtu fulani wa chama fulani ili wakumbukwe ktk teuzi za raisi. mf. mzuri ni e. buhohela wa itv now anakula shavu ikulu, same as pasco, kakengeuka sana huyu jamaa wa ppr!
 
Aliye na macho hambiwi ona. Wengi hawajaelewa post nadhani lugha shida. Kimsingi mwandishi anasema viegezo vya chaguzi huru na wa haki havijatimizwa / havikutimia.
 
 

Attachments

  • Zanzibar.jpg
    9.4 KB · Views: 54
  • Zanzibar.jpg
    9.4 KB · Views: 55
  • Zanzibar1.jpg
    34.9 KB · Views: 57
buhohela ni nani ikulu kwani
 
Mkuu Gamba la Nyoka, mtu ukifungua shauri mahakamani, kitu cha kwanza kinachoangaliwa ni vifungu vya sheria vinasemaje!.
1. Kwanza kabisa, Jee Jecha yeye kama Jecha, anayomamlaka ya kujigeuza ZEC na kutoa maamuzi kwa niaba ya ZEC?!- Hapa mahakama ingemtwanga Jecha kuwa hakuna kipengele chochote cha sheria kinachompa mamlaka Mwenyekiti wa ZEC kujigeuza yeye ndio ZEC!. Kama uamuzi ule ungekuwa ni uamuzi wa ZEC kama ZEC, then angalau ungekuwa na nguvu kidogo ya kisheria.

2. Jee kuna kipengele chochote cha sheria kinachoiuhusu ZEC kufuta matokeo yote ya uchaguzi mzima kwa sababu tuu ya kasoro kidogo mahali. Hapa mahakama kuu ingekuta hakuna kipengele chochote cha sheria kinachoruhusu hili kufanyika!.

3. Mahakama ingetoa kitu kinachoitwa "executive orders" ambazo kwa hapa ziko tatu, "prohibition, certiorari na mandamus" lakini kwa wenzetu ziko 6, hizi ni amri ambazo mahakama inazo kuiamuru serikali kufanya jambo fulani kwa lazima, serikali itake au isitake. Kinachotakiwa ni lazima kuwatumia manguli kwelikweli wa sheria, ambao manguli wa level hiyo CUF inao, yuko Prof. Safari, kule Zenj yuko Aboubakar Khamis Bakari, sijui walishikwa na kigugumizi gani!.

4. Tume ya Uchaguzi Zanzibar, ingeamuliwa kwanza kutangaza matokeo yote halali ya uchaguzi wa Zanzibar, kisa kuthibitisha maeneo yenye kasoro, kasoro hizo kama ni kubwa sana za kuathiri matokeo, then ni majimbo tuu yenye kasoro ndipo uchaguzi ungerudiwa!.

Amri hizo ni hizi
  • certiorari an order by a higher court directing a lower court to send the record in a given case for review;
  • habeas corpus demands that a prisoner be taken before the court to determine whether there is lawful authority to detain the person;
  • mandamus an order issued by higher court to compel or to direct a lower court or a government officer to perform mandatory duties correctly;
  • prohibition directing a subordinate to stop doing something the law prohibits;
  • procedendo sends a case from an appellate court to a lower court with an order to proceed to judgment;
  • quo warranto requiring a person to show by what authority they exercise a power;
Prof. Issa Gullamhusein Shivji akishirikiana na Prof. Gamalieli Mgongo Fimbo mara kibao wameitumia mahakama kuilazimisha serikali kufanya jambo fulani au kuizuia kufanya jambo fulani.

Huu uamuzi wa CUF kukwepa kutumia njia rasmi za kutafutia haki, ndio unaoniogopesha, kuwa kuna kitu CUF wanachokitegemea. Hawawezi kususa tuu ili kususa for nothing!, there is something!, yaani the motive behind kususa kwao inajulikana, ni kupinga huo ubakaji, lakini jee wamesusa ili iweje?!, what are they trying to achieve!, sio nothing!. Uchaguzi umefanyika, CUF got nothing!, jee mambo sasa ndio yameishia hapa?!.

Pasco


 
Mkuu UngaUnga, Pasco ni yule yule juzi, jana na leo, tatizo ni viwango tuu vya uelewa!.

Pasco sio miongoni mwa wale waandishi wa kujikombakomba kwa yeyote kwa lolote, wala hategemei kukumbukwa na yeyote kwa sababu aliishaachana na kutumwa siku nyingi, hivyo hawezi kuejea tena utumwani, kwa kutumwa na rais au na yeyote!, yeye ni mtu wa kujituma tuu!.

Magufuli akifanya mazuri, tunamsifu kama hapa
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata
Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simp

Lakini akiboronga tunambonda tuu kama tunavyowabonda waborongaji humu!.
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ..
Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki ...
Amri ya Rais Kuifuta Siku ya Uhuru Haijataja Usafi!. Jee Usafi n

Ukizisoma thread hizo, utagundua Pasco sio mtu wa kunjikomba kwa yoyote wala kwa lolote!.

Pasco
 
Hayo unayoyasema ni kweli na ndivyo inavyopaswa iwe! , lakini Aliyemteua Jecha ndiye aliyeteua hao majaji.
Kama aliamuriwa avunje sheria ya Zec kwa kufuta matokeo unilaterally with impunity, usishangae na hao wengine pamoja na kuujua ukweli wakashinikizwa wa rule otherwise, na kwa gharama yoyote!

Historia iko wazi, kwa matokeo ya kesi ya mgombea binafsi, jinsi ilivyohukumiwa ni somo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…