Asha Ommary
Member
- Sep 1, 2020
- 97
- 90
Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wakiwa katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, makao makuu ya chama, Dodoma
Kijiti cha uenyekiti kukabidhiwa rasmi leo.
Chama cha Mapinduzi(CCM) kinafanya Mkutano Mkuu Maalumwa kumchagua Mwenyekiti wake wa taifa jijini Dodoma katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Makao Makuu ya Chama.
Wajumbe wengi wapo ukumbini
UPDATES:
Rais Samia apata kura zote 1862 (100%)
MKUTANO Mkuu Maalum wa Chama cha Mapinduzi CCM ulioketi leo jijini Dodoma umempitisha Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mwenyekiti wa Sita wa chama hicho akipata kura za ndiyo kwa asilimia 100.
Akitangaza matokeo hayo, Mwenyekiti wa uchaguzi huo ambaye pia ni Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema kura zilizopigwa ni 1,862 ambapo kura za Ndiyo zilikua zote 1,862 ikiwa ni Asilimia 100 ya kura zote.
Rais Samia: Asanteni sana wana CCM wenzangu kwa kunichagua mimi kuwa mwenyekiti wa chama chetu najua jukumu mlilonipa ni kubwa lakini naamini nitaweza, naamini nitaweza kwanza chama chetu kinaongozwa na katiba na kanuni, kazi hii si yangu pekee yangu bali ni yetu sote.
Rais Samia: Nafahamu kuwa nachukua jukumu la kukiongoza Chama hiki (CCM) kikiwa kina baadhi ya changamoto ikiwemo uhaba wa vitendea kazi, kuna baadhi ya Mikoa na Wilaya Viongozi hawana usafiri, changamoto nyingine ni maslahi duni kwa Watumishi wa Chama.
Rais Samia: Nafahamu kuwa kuna malimbikizo ya madai ya stahiki zikiwemo za uhamisho na kustaafu, nawaahidi nitashirikiana na nyinyi kuzitatua changamoto zilizopo kwenye CCM nilizozitaja na ambazo sijazitaja.
Rais Samia: Ninafahamu kuna changamoto za uhaba wa vitendea kazi kama usafiri kwenye Wilaya zetu na Mikoa yetu jambo ambalo linalofifisha utendaji kazi wa kukijenga chama chetu na Nchi yetu kwa ujumla
Rais Samia: Changamoto nyingine ni maslahi duni kwa watendaji wetu pamoja na malimbikizo ya madai ya stahiki ikiwemo ya uhamisho na kustaafu, niwaahidi nitashirikiana nanyi katika kutatua changamoto hizo kwa pamoja, "
Idadi ya wajumbe yapungua kutoka 1,909 hadi 1,876
Naibu katibu mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo amesema wajumbe wanaotakiwa kuhudhuria mkutano mkuu wa chama hicho ni 1,909 lakini waliowasili katika ukumbi wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma ni 1,862.
Amesema idadi wa wajumbe imepungua kutoka 1,909 hadi 1,876 na kwamba watu 33 hawajafika kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo vifo na kwamba waliohudhuria ndio watakaopiga kura.
Amesema CCM imekuja na kauli mbiu ya ‘chama imara, Serikali madhubuti, kazi inaendelea’
Lazaro Nyalandu arejea Chama cha Mapinduzi (CCM)
Lazaro Nyalandu ametangaza rasmi kurejea CCM mbele ya Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Samia Suluhu kupitia Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Dodoma leo akitokea CHADEMA, Nyalandu alitangaza kujiondoa CCM mwaka 2017.
Nyalandu: Kupitia Mkutano huu Maalum wa CCM naomba kukushukuru Mwenyekiti (Rais Samia) kwa kukubali Kunipokea, kunisamehe na kuniruhusu kurejea nyumbani (CCM), hakuna furaha inayozidi furaha ya Mtoto arejeapo nyumbani
Nyalandu: Katika Nchi ya ugenini wimbo hauimbiki, Mzee Lowasa, Mzee Sumaye, Mzee Slaa hawa ni Mashuhuda wachache kati ya wengi wa kwanini wimbo wa Bwana hauimbiki katika Nchi ya ugenini
Nyalandu: Watanzania wameiona nyota yako Rais Samia, wameguswa kwa kuinuliwa kwako kwakuwa Mungu alikuandaa kuwa Kiongozi wa Taifa hili, Mungu akuongoze katika safari, uwepo wangu kwenye Mkutano huu ni kielelezo tosha cha wewe kuungwa mkono na Watanzania wote
Nyalandu: Kazi iendelee, Rais wetu (Samia Suluhu), Mama yetu, Mwenyekiti wa Chama chetu (CCM), Mama tuma neno lako likaponye wote walioumia, ukaitwe heri na shujaa wa mioyo ya Watanzania, ukaongeze Tabasamu katika nyuso za Watanzania wote
Uteuzi wa viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM):
1. Katibu Mkuu- Daniel Chongolo
2. Naibu Katibu Mkuu (Bara)- Christina Mndeme
3. Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi- Shaka Hamdu Shaka
4. Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar) - Juma Sadala