LGE2024 Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni muhimu, tukajiandikishe

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Nani kakuambia uchaguzi ndio unatoa viongozi? Hiyo kupiga kura ni kuhadaa umma na dunia kuwa kuna uchaguzi/demorasia, lakini kinachoendelea kwenye huo uchaguzi ni upuuzi kama upuuzi mwingine.
 
Hakuna Mifumo thabiti ya Utambuzi wa Watu kwenye hizi nchi zetu hizi za ki-Afrika. Suala hili limefanywa kwa makusudi na baadhi ya Watawala wahalifu ili kuweza kujinufaisha binafsi wao wenyewe wakiwa madarakani. Mathalani, watawala wamekuwa wakivuruga makusudi mifumo ya utambuzi wa Watu katika nchi zao kwa nia ovu ya kutaka kuiba kura nyakati za Uchaguzi wa siasa, ili kuendesha biashara haramu ya binadamu, magendo na uhalifu katika masuala ya utakatishaji fedha chafu, kufanikisha biashara zao za madawa ya kulevya, na kufanikisha biashara haramu za kumiliki na kuendesha Magenge ya Uhalifu. Mfano mzuri zaidi kwenye suala hili ni uendeshaji wa biashara haramu ya magenge ya Utekaji watu na kuomba "Kikombozi" kutoka kwa Wanandugu wa Mtekwaji (abductees that kept into hostage camps) inayofanywa na baadhi ya Watawala wahalifu nchini Nigeria kupitia kwa Magenge ya Wanamgambo wa Boko Haram.
NB: Nchi ya Nigeria ina idadi ya watu wapatao zaidi ya Milioni 200 ambao wanaishi nchini humo, lakini watu ambao wamesajiliwa rasmi kwenye database ya raia wakazi wa nchi hiyo hawafiki hata idadi ya watu Milioni 22 nchini kote. Aidha, hata SIM cards za simu zilizosajiliwa rasmi kwa utambulisho rasmi ulio halali hazifiki hata Milioni Kumi kwenye nchi hiyo yote kabisa.
That's why Nigeria kuna uhalifu mwingi Sana, na ni vigumu Sana kuwatambua wahalifu hao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…