Uchaguzi wa Tanzania kwa Jicho la Rohoni ni Uchaguzi wa Msimu dhidi ya Msimu

Uchaguzi wa Tanzania kwa Jicho la Rohoni ni Uchaguzi wa Msimu dhidi ya Msimu

mwakibete

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2009
Posts
3,068
Reaction score
2,299
Awali ya yote naomba kuweka interest zangu mbele, Mimi ni muumini wa mambo ya Kiroho. Ninaamini juu ya uwepo wa ulimwengu wa Kiroho. Nina amini kuwa, kabla ya mambo kuwa vile yanavyoonekana kuwa katika ulimwengu wa Kimwili, mchakato wake huwa unakuwa ulianzia Rohoni na baadaye kujidhihirisha kwenye macho ya damu na nyama.

Sasa basi, baada ya kusema hayo, nawiwa kusema machache juu ya Uchaguzi wa Tanzania wa mwaka 2020 unaotarajiwa kufanyika Tarehe 28/10/2020.

Kwanza natamani waTanzania tujue kama tupo kwenye MSIMU mpya. Katika msimu mpya, kisiasa, HATOCHAGULIWA mtu kwa sababu ya yale amefanya. Kwa sababu hata angefanya mazuri kiasi gani kwa WaTanzania bado MSIMU ungemkataa. Kila msimu mpya unapokuja, huwa unakuja na vitu vyake na taratibu zake.

Kwa hivyo basi, ushindani tunaouona haujaanzia machoni petu bali umekuja kujidhihirisha machoni petu baada ya kwenye ulimwengu wa KIROHO kuwa vile tunavyouona. Ni ushindani baina ya MSIMU na MSIMU (Msimu Mpya na Msimu wa Zamani). Hakuna namna msimu wa zamani unaweza kuzuia msimu mpya kutokea.

Kibiblia, “40” ni namba ya utimilifu. Ukisoma Biblia, utagundua utimilifu wake. Nitatoa mifano michache juu ya huo utimilifu kutoka katika Biblia kwa kuangalia nyanja ya utawala.

Watumishi kama Mussa> Sauli > Daudi> Suleiman na wengineo wengi, Soma Biblia kujiridhisha, kila mmoja kwa majira na msimu wake walitawala kwa takribani miaka 40. Na tunaona baadhi ya sehemu ambavyo haikuwa rahisi kwa mfano, Sauli kuachia mamlaka kwa Daudi baada ya kipindi chake kuisha, na tunajua nini kilimpata Sauli alipopambana na MSIMU mpya wa Daudi.

Kwa wajuvi wa hesabu na historia, tutafakari hili pamoja; "Kijani" ilizaliwa miaka ya 1977. Ukijumlisha na namba ya utimilifu "40" utapata "2017". Kimsingi kabisa, 2017 ilikuwa iwe ni ukomo wa Kijani kwa nchi ya Tanzania, kwa maana kwamba haya yanayoonekana sasa ni matokeo yaliyotokea mwaka 2017 katika ulimwengu wa KIROHO. Kwa sababu ya ratiba ya katiba yetu ililazimu isubiri sasa 2020. Na hivyo basi, hali ya uchaguzi wa 2015 ilikuwa ni vuguvugu ya 2017 kuelekea 2020

Kwa hivyo basi, natamani watawala wajue kuwa si "NI YEYE" anayesababisha haya mambo kuwa yalivyo, bali ni MSIMU umeamua kumtumia katika kuhakikisha waTanzana tunaenda na kasi ya msimu Mpya.

Msimu mpya unahitaji vitu vipya kabisa. Ni wakati wa kusimama kidete kupambana na ukosefu wa haki za msingi za binadamu, mmomonyoko wa kanuni na maadili na utu wema wenye mvuto na mashiko.

Marko 2:22​

Wala watu hawatii divai mpya katika viriba vikuukuu. Kama wakifanya hivyo, divai itavipasua hivyo viriba, nayo divai pamoja na hivyo viriba vitaharibika. Divai mpya hutiwa katika viriba vipya!”

Luka 5:38​

Divai mpya hutiwa katika viriba vipya.


KUJIANDAA KISAIKOLOJIA NI MUHIMU KWA MSIMU MPYA.
ASIKIAYE NA AFAHAMU.
 
Vote for His Excellency President Magufuli, He is among powerful leader in the world
 
Eeeh Mungu matendo yako ni makuu sana.

Ahsante kwa kuwa kijani inaenda kufutika tz
 
Hujambo lakini mheshimiwa askofu Mwamakula? Naona wewe na mchungaji mwenzio Gwajima mmeamua kujitosa kwenye siasa directly and indirectly respectively! Peace Sana jombaa wasalimieni waumini huko makanisani kwenu!
 
Back
Top Bottom