Uchaguzi wa TFF: Wallace Karia achaguliwa kuwa rais mpya wa TFF

Kikubwa toa mawazo ya kujenga ikiwa pamoja na kuwa na sheria zinazojitosheleza maana yote haya ni kutokana na kutumia busara zaidi badala ya kanuni na sheria
 
Hakuna kureseat?
Jibu zuri ...ni kweli alipata zero ila wanasahau kwamba anaefeli form 6 ana cheti kizuri chenye credit zaidi ya tatu O-level which means huwezi kumfananisha na alieishia form 4 na D zake nne akaenda certificate
 
Kura zingepigwa kwa kutotumia hawa wajumbe wachumia tumbo Ali Mayai angeshinda maana wanamichezo wa zamani waliungana kumpigia debe Ali lakini wapiga Kura wameacha keki ya taifa wametanguliza tumbo.
Tatiz huku nje watu wanaamini kwamba kucheza soka ni kuongoza kumbe Urais wa TFF ni taasisi hivyo anahitajika mtu mwenye uzoefu wa soka letu kwa kucheza ama kutokucheza lakini pia awe na uzoefu wa kuongoza taasisi yoyote...sina shaka na Ally ila nadhani alipata promo zaidi kwa watu nje ya wapiga kura
 
Kasome vizuri Mada yote kila kitu kimewekwa kumhusu Wales, una haraka gani?
Mkuu wewe ndo ulichelewa kuingia...@Kinyungu ali-comment kabla post hawajaweka updates za wasifu...nadhani wewe uliingia wasifu wake ukiwa umepandishwa kwahiyo Kinyungu hakuwa ana haraka bali wewe ndio ulichelewa kuingia
 
Sheria haziruhusu kure-sit mtihani eti..... Hakika MBUMBUMBU ni MBUMBUMBU tu
 
hahahahaah...mnategemea mabadiliko kutoka kwa wambura??? hahahaha....kwa lipi hasa
 
Huyu Mwakalebela sasa aende akalime jamani...kwenye siasa pwaaaa, na kwenye michezo pwaaaa! Mkosi gani huu?
 
Karia na Wambura wote ni Simba damu.
Sasa matopeni chezeni mpira visingizio vya Malinzi havitakuwepo tena.

Kamati ya mashindano ilijaa watu wenu lakini kila kitu ilikuwa Malinzi hiki, Malinzi kile.


Huu ndio ukwlei, kibaya zaidi, viongozi hawachezi mpira uwanjani labda wa mezani.
labada tutegemee uhsindi mwingi wa mezani kuanzia sasa.
 
Tuwe serious wana JF wakati tunachambua masuala yenye maslahi ya Taifa. Soka letu liko ICU sasa tuwape muda hawa viongozi wapya tuone watafanya nini kulitoa soka letu ICU, kulipa uhai! Tuache kuzungumzia "watu" tuzungumzie ISSUES za mpira wa miguu wetu na namna ya kujikwamua! Huo ndio ushauri wangu au siyo!?
 
Si ndio mwanawe kakamatwa na mlungula wa kugawa chooni au sio, Tanzania bila rushwa ni kama miujiza..
HAPANA. Mtoto aliyekamatwa na TAKUKURU akiwa na pesa za kuhonga si wa Ndudgu KARIA, ni wa ndugu mwingine ambaye jina lake linafanana na la mtoto huyo. Huyo mzazi aliyemtuma mwanae ahonge wajumbe hakupata hiyo nafasi ya ujumbe. Hatutaji majina kwani yalishatajwa na TBC.
 
Huyu Rais wa TFF.. CV yake katika kazi.. Imenichanganya amewai kuwa mkurugenzi alafu sasa hivi mhasibu mkuu, mkoa wa Morogoro.. Napata shaka kuwa mkurugenzi na kuwa mhasibu katika mkoa kipi kikubwa
 
Huyu jamaa ile tuhuma ya uraia ndo imempaisha juu.vp huyu ndugu yetu Hali mayai na matembele
 
hIZO KURA 9 NDO MATEMBELE YENYEWE, AKITAKA ALE, ASIPOTAKA ASUSE
Kila mtu apewe nafasi anayo fit, kama ni uchambuzi wa Ndondo Cup, basi apewe hiyo
Wacha maneno weka soka la kisasa ...
Soka la kisasa linahitaji udhamini makini
Mmeona jinsi Leodgar Tenga alivyoweza kushawishi wadhamini makini kama 'Serengeti' na NMB
Mmeona jinsi udhamini huo ulivyofufua ari ya Taifa Stars enzi za Tenga
Hivi mnategemea Tembele angeweza kuaminikaje kwa wadhamini wakubwa na makini kama Emirates, kwa mfano tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…