GE2025 Uchaguzi wa Udiwani Mzinga waahirishwa baada ya kifo cha Mgombea wa CUF

GE2025 Uchaguzi wa Udiwani Mzinga waahirishwa baada ya kifo cha Mgombea wa CUF

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Wagombea muombeane heri!. Maana hivi vifo vinazidi sana. Na kunagharama mtu alishazifanya za kampeni na mambo mengine so uchaguzi unapoharishwa kuna mambo yanabadilika kabisa!
===============
Uchaguzi wa Udiwani katika Kata ya Mzinga, Jimbo la Kivule, jijini Dar es Salaam, umeahirishwa kufuatia kifo cha aliyekuwa Mgombea kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Rashid Abdallah Nandonde.

Taarifa iliyotolewa leo na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jiji la Dar es Salaam, Jimbo la Kivule, imesema kuwa kusitishwa kwa uchaguzi huo kunazingatia masharti ya Kifungu cha 71(1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na.1 ya Mwaka 2024.

Soma Pia: Uchaguzi wa Ubunge Fuoni na Udiwani Chamwino, Mbagala Kuu utafanyika Desemba 30, 2025

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) itatoa notisi mpya kupitia Gazeti la Serikali kuhusu tarehe nyingine ya uteuzi wa wagombea, na taratibu zote za uchaguzi katika Kata ya Mzinga zitaanza upya.

Aidha, taarifa imeeleza zaidi kuwa wagombea wengine walioteuliwa kihalali wataendelea kubaki kwenye nafasi zao, isipokuwa kama mgombea atajitoa mwenyewe. Pia, kampeni zote za uchaguzi katika kata hiyo zimesitishwa hadi hapo uteuzi mpya utakapokamilika.
Screenshot 2025-10-20 174357.png
 
Back
Top Bottom