Uchaguzi wa Wabunge wa EALA 2022

Uchaguzi wa Wabunge wa EALA 2022

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,611
Nashauri upatikanaji wa Wabunge wa EALA Tz tuzingatie umakini, haki na weledi.

Tukiendekeza tabia za wajumbe tumepata hasara.

Sasa hivi desturi ya dunia hii ni kunyang'anyana fursa.

Kama tutapeleka Wabunge wasio na sifa za weledi hakika tutapoteza.

Sasa hivi baada ya uchaguzi wa Kenya kumuingiza Raila Odinga ikulu, ni dhahiri kwamba sasa Tz tumezungukwa na metric brains kotekote kwenye EAC.

Napendekeza utaratibu wa kuwapata Waheshimiwa hawa usiwe ule wa kupitia vyama vya siasa na Bungeni bali waombe kwa mfumo wa kuomba ajira/kazi ambapo watakaofanikiwa wapewe malengo na matarajio ya taifa kwao ambapo ima faima wabanwe kuyafikia malengo na matarajio hayo. Serikali isilegee katika hili.

Bill Clinton alisema Arusha ni Geneva ya Afrika, mimi nasema Kenya ni USA ya EAC na Maziwa Makuu.

Bitter Truth!
 
ukweli ni kwamba katika uteuzi na uchaguzi wa wajumbe wa baraza la wa wajumbe la EALA ; Tanzania uwakilishi wetu umekuwa unazingatia siasa na sio weledi wa wajumbe tanaowapeka kutuwakilisha! Matokeo yake we are not effectively represented kama majirani zetu! Tubadilike.
 
Utawala wa sasa umeamua kulegeza kamba kwenye mambo muhimu ya kitaifa.

Badala ya kupigania maslahi yetu tumewekeza zaidi kwenye kuhakikisha tunawafurahisha majirani zetu ambao ni washindani kiuchumi.
 
Haya maneno yako ninaya-frame na kuyaweka ukutani ofisini kwangu.
 
sasa humu unadhani kuna mtu anaehusika atakae upokea ushauri wako...jamani enh tujifunzeni japo kuzitembelea ofisi husika...na tutumie barua japo kwa anuani zao za posta...humu ni sawa na kurenga jiwe gizani...linaweza lisimpate mtu
 
Utawala wa sasa umeamua kulegeza kamba kwenye mambo muhimu ya kitaifa.

Badala ya kupigania maslahi yetu tumewekeza zaidi kwenye kuhakikisha tunawafurahisha majirani zetu ambao ni washindani kiuchumi.
Nyie mliopigania maslahi ya Nchi mliwanufaisha vipi Watzn?
 
sasa humu unadhani kuna mtu anaehusika atakae upokea ushauri wako...jamani enh tujifunzeni japo kuzitembelea ofisi husika...na tutumie barua japo kwa anuani zao za posta...humu ni sawa na kurenga jiwe gizani...linaweza lisimpate mtu
Ukitaka kujuwa kwamba wanafuatilia ona haya:-
1. Kwanini watu humu wanaficha majina yao?
2. Kwanini mtandao umesajiliwa kwao huko serikalini?
3. Mtandao unalipa ada wapi kama siyo kwao?
4. Weka maudhui yasiyotakiwa humu uone kama wewe na Mods mtakuwa salama.
5. ........................................
6. ........................................
7. ........................................
 
Nashauri upatikanaji wa Wabunge wa EALA Tz tuzingatie umakini, haki na weledi.

Tukiendekeza tabia za wajumbe tumepata hasara.

Sasa hivi desturi ya dunia hii ni kunyang'anyana fursa.

Kama tutapeleka Wabunge wasio na sifa za weledi hakika tutapoteza.

Sasa hivi baada ya uchaguzi wa Kenya kumuingiza Raila Odinga ikulu, ni dhahiri kwamba sasa Tz tumezungukwa na metric brains kotekote.

Bill Clinton alisema Arusha ni Geneva ya Afrika, mimi nasema Kenya ni USA ya EAC na Maziwa Makuu.

Bitter Truth!
Akili na exposure tanzania ni sifuri is was there hadi aibu
 
Akili na exposure tanzania ni sifuri is was there hadi aibu
Napendekeza utaratibu wa kuwapata Waheshimiwa hawa usiwe ule wa kupitia vyama vya siasa na Bungeni bali waombe kwa mfumo wa kuomba ajira/kazi ambapo watakaofanikiwa wapewe malengo na matarajio ya taifa kwao ambapo ima faima wabanwe kuyafikia malengo na matarajio hayo. Serikali isilegee katika hili.
 
As long as you acknowledge that they were from me!
Napendekeza utaratibu wa kuwapata Waheshimiwa hawa usiwe ule wa kupitia vyama vya siasa na Bungeni bali waombe kwa mfumo wa kuomba ajira/kazi ambapo watakaofanikiwa wapewe malengo na matarajio ya taifa kwao ambapo ima faima wabanwe kuyafikia malengo na matarajio hayo. Serikali isilegee katika hili.
 
Wanatokea ndani ya vyama kwenda kupigiwa kura bungeni. Kule bungeni kuna ushabiki wa vyama usioangalia maslahi mapana ya nchi.
Na sasa wajumbe (wabunge) wa kupiga hizo kura ili kuwapata hao wawakilishi wetu katika bunge la EALA, ni hao wa CCM. Hawa watu wa chama hiki hata utoe mawazo mazuri kiasi gani, wao CCM ni mbele kwanza kabla ya nchi. Tena kubwa zaidi ni ubinafsi kuwekwa mbele kuliko huo wanaouita au aliouita mwendazake "UZALENDO"

Kitakachotawala kwenye huo "uchaguzi" wa wabunge wa EALA ni "mwenzetu" zaidi kuliko uweledi wa mtu.
 
sasa humu unadhani kuna mtu anaehusika atakae upokea ushauri wako...jamani enh tujifunzeni japo kuzitembelea ofisi husika...na tutumie barua japo kwa anuani zao za posta...humu ni sawa na kurenga jiwe gizani...linaweza lisimpate mtu
Asingeleta hapa wewe pia usingepata hicho ulichokipata. Acha watu wamwage kila sehemu watu tupate na kuchangia mawazo kama hivi wanavyochangia, kwa sababu hata huko unakosema kunastahili, yakipelekwa hayatafanyiwa kazi na wewe hutajua.
 
Na sasa wajumbe (wabunge) wa kupiga hizo kura ili kuwapata hao wawakilishi wetu katika bunge la EALA, ni hao wa CCM. Hawa watu wa chama hiki hata utoe mawazo mazuri kiasi gani, wao CCM ni mbele kwanza kabla ya nchi. Tena kubwa zaidi ni ubinafsi kuwekwa mbele kuliko huo wanaouita au aliouita mwendazake "UZALENDO"

Kitakachotawala kwenye huo "uchaguzi" wa wabunge wa EALA ni "mwenzetu" zaidi kuliko uweledi wa mtu.
Nijuavyo (niko tayari kusahihishwa) ni kwamba chama kinachounda serikali ndicho kinachopeleka Wabunge wa Tz EALA (umewahi kusikia kambi ya upinzani imetoa Mbunge?).

Kama serikali ni ya mseto basi upinzani unaoshiriki kuunda mseto nao utapewa nafasi.

Ila kwa minajili ya kuondoa kero za muungano, GoT inatoa baadhi ya nafasi kwa SMZ pia.

Wewe kaa mkao wa kula siku siyo nyingi kipenga kitapulizwa!
 
Back
Top Bottom