Elections 2010 Uchahakachuaji wa Matokeo ya Slaa na Viti Maalumu

Elections 2010 Uchahakachuaji wa Matokeo ya Slaa na Viti Maalumu

Mkuu Superman,

Naona hapa hujawa superman ha haaaa!!! Inabidi usome tena somo la uraia.

Viti maalumu vya wabunge vinatokana na kura za wagombea ubunge. Viti maalum vya madiwani, vinatokana na kura za madiwani.

Kura za urais zinaingia pale tu ambapo chama hakina mgombea wa ubunge au udiwani.

Effect ya kura za Slaa kwenye mgawo wa viti maalum itakuwa ndogo sana.

Asante kwa elimu hii. Kwa maana hii basi jimbo la Arusha kutakuwa na viti maalumu vingi tu vya upinzani ( upinzani una kata 10, CCM 9) hivyo possibility ya kuunda serikali ya jiji inaangukia upinzani! Thanks Lord!
 
Asante kwa elimu hii. Kwa maana hii basi jimbo la Arusha kutakuwa na viti maalumu vingi tu vya upinzani ( upinzani una kata 10, CCM 9) hivyo possibility ya kuunda serikali ya jiji inaangukia upinzani! Thanks Lord!

Hilo jiji limechukuliwa na CHADEMA. Mbunge pia ni diwani kwahiyo hapo wanakuwa na madiwani 11 wa kuchaguliwa na CCM 9. Kisha wataongezeka madiwani wa kuteuliwa ambao kwa namba hizo CHADEMA itakuwa nao wengi kuliko CCM.

Pia miji mingine kama Moshi, huenda pia Mbeya na mwanza. Sina uhakika na Dar lakini huenda nalo limeenda CHADEMA. Yule fisadi mwuza viwanja hataweza kuuza tena kule Kinondoni.
 
Hapana, wabunge wanawake wa majimbo hawapunguzwi katika ile 30%. Asilimia hii iko fixed. Ndiyo maana wachambuzi walisema kama wanawake wakijitokeza wengi kwenye majimbo, kuna uwezekano wa kufikia asilimia 50:50.

Unaweza kuwa sahihi juu ya hili maana sina uhakika 100%. Ila kwa kuangalia bunge lililopita nafikiri wanatolewa. Kwa hoja yako, kwenye bunge lililopita kungelikuwa na wabunge wa kuteuliwa karibu 87 wakati namba inaonyesha ilikuwa 75.

Hiyo ya 50:50 ilikuwa ni hoja ya CCM ambayo haijapitishwa bado, labda mpaka 2015.
 
Nashukuru sana kwa kupata elimu hii! Thanks great thinkers!
 
Asante sana wakuu kwa kuendelea kuelimishana na kukosoana. Nilisoma kutoka katika ambacho si cha uhakika.
 
Nadhani mko sahihi, ni kura za wabunge! Isipokuwa nadhani kulikuwa na mapendekezo ya kutumia kura za Rais. Mwaka huu viti maalumu ni asilimia 40 ya wabunge wote. Wanawake walioshinda majimboni hawaondolewi kwenye hiyo asilimia, so infact tunaweza kujikuta tuna asilimia 45 ya wanawake bungeni.
 
FROM NEC WEBSITE The National Electrol Commission of Tanzania - Homepage

Tanzania has also a system of proportional representation according to votes, in the elections of Members of the Parliament for Women Special Seats. These are special seats for women which are thirty percent of the total number of elected constituency members, plus five members elected by the Zanzibar House of Representative, the Attorney General of the United Public of Tanzania (ex-officio Member of the Parliament), the Speaker and ten presidential nominees.

KWA HIYO 30% YA 239 = 72
RAIS 10
RAIS ZNZ 5
EX OFFICIO 2
TOTAL 89

CHA KUSHA CCM NA CHADEMA WAMEPELEKA MAJINA 100 NA YANAYOITAJIKA NI 72, CAN SOME BODY HELP ME ON THIS?
 
Back
Top Bottom