niliomba kusimamia uchaguzi katika kituo fulani ivi, jina langu likatoka, likapelekwa halmashauri, walipoona kuwa nimejiandika kuwa mimi ni mwanafunzi wa chuo, wakalikata. hii ni bahati mbaya, nilikuwa naenda sio kwamba nikapate hala yao, bali nikalinde kura kwani niliomba usimamizi mkuu wa kituo. my waifu amepata na ananipa data zote wanavyofanya huko na wanavyoambiwa wafanye, vitisho wanavyopata na kila aina ya ushetani wa ccm. hakika yake nchi hii inaonewa sana na ccm. na kama kungekuwa na uchaguzi wa huru na haki, sisiemu isingekuja kupata kiti.
elimu yangu ni ya juu sana, lakinni ili nipate niliweka cheti cha degree yangu yakwanza kabisa, kumbe hilo likawa kosa. wao walikuwa wanachagua watu ambao watawapendelea wao, wasomi wamewazuia kabisa, wamewachagua mambumbumbu wa form four ambao watasikiliza maelekezo yao yote kwa hofu. majina hayajaonekana kwenye vituo vingi, na yale ya wasimamizi wakuu na wasiaidizi, yamechakachuliwa yote wakawekwa makada..TUME HURU YA UCHAGUZI TUTAIPATA LINI hapa tz? Ee Mungu tuokoe na ccm hii.