Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Masoko ya chakula nchini yamekuwa katika hali ya uchakavu na uchafu hivyo kuhatarisha afya za watumiaji wa huduma za masoko hayo hususani wanawake ambao ndio watumiaji wakubwa wa huduma hii. Hii ni kinyume na Sheria ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa ya mwaka 1982 (kama iliyorekebiswa) inayozipa Mamlaka ya Serikali za Mitaa jukumu la kusimamia na kuboresha Afya ya Jamii.
Sababu zinazopelekea uchafu na uchakavu katika masoko hayo ni kama ifuatavyo:
i. Agizo la Ofisi ya Rais – TAMISEMI, linataka kila Halmashauri kutenga asilimia 15 ya mapato yanayopatikana kutoka katika masoko ili kutekeleza shughuli za maendeleo, marekebisho na usafi katika masoko hayo. Hata hivyo, Halmashauri 8 zilishindwa kutenga asilimia 15 ya kiasi cha fedha kinachokusanywa kama mapato kutoka katika masoko ili kugharamia usafi wa masoko hayo.
Mfano, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ilitenga asilimia 5, wakati Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Mbeya, Manispaa za Kigoma Ujiji na Temeke na Wilaya za Korogwe, Mbarali na Sengerema hazikutenga kiasi chochote cha fedha kwa ajili hiyo katika kipindi cha miaka minne (2016/17 – 2019/20) kama inavyoonekana katika kielelezo Na. 2.
ii. Katika ukaguzi huo, CAG alibaini masoko 8 kati ya masoko 20 yaliyotembelewa, hayakuwa na watoa huduma waliosajiliwa kutoa huduma mbalimbali ikiwemo huduma za kuondoa takataka na kufanya usafi katika maeneo ya soko. Vilevile, CAG alibaini kuwepo kwa idadi kubwa ya wafanyabiashara katika masoko zaidi ya uwezo wa masoko hayo
iii. CAG alibaini kulikuwa na udhaifu katika usimamizi wa uendeshaji wa masoko ambapo kati ya Halmashauri 10 zilizokaguliwa, Halmashauri 5 hazikuwa na sheria ndogondogo za usimamizi wa usafi wa masoko. Pia, Halmashauri 7 kati ya 10 hazikuwa na miongozo ya kusimamia kamati za usimamizi wa masoko kwenye masuala ya usafi. Masoko 14 kati ya 25 yaliyokaguliwa hayakuwa na kamati za usimamizi wa masoko pamoja na kutokuwa na uongozi wa masoko yaliyokuwepo.