Uchakavu wa noti za fedha yetu Watanzania

Uchakavu wa noti za fedha yetu Watanzania

ilisha juniour

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
714
Reaction score
219
Wakuu habari?

Kwa watu walio makini wakishika fedha hasa noti mtagundua kuna tatizo sugu la uchakavu wa noti zetu hasa shilingi elfu moja, elfu mbili, pamoja na noti za elfu tano,hili kwa sisi watanzania wa kawaida tunaliona madukani, sokoni na kwenye daladala, unapotoa fedha kununua bidhaa au huduma lazima urudishiwe pesa ikiwa na hali mbaya kwa maana imechakaa, kwakuwa jamii forums ni kijiji nna imani humu watu wa Benki kuu ya Tanzania wapo,nna maswali mawili la kwanza hamna bajeti ya kuchapisha noti zenye kiwango na kuziingiza kwenye mzunguko?

Maana kwa uelewa wangu kidogo sana wa uchumi thamani ya pesa inaangalia pia durability yake(muda inaodumu kabla haijatolewa katika mzunguko kama chakavu), swali la pili kama mmeliona na kulielewa hili tatizo mnaweza litatua vipi?

Karibuni kwa maoni na michango mbalimbali atleast nipate mwanga na uelewa kwenye hili tatizo.

pic-not.jpg
 
Nadhani watumiaji wa pesa hasa za noti ya elfu moja, mbili na tano watakubali kwamba hizo noti nyingi zimechakaa mno na ni kero kwa watumiaji.

Naishauri benki kuu wachague aina ya materials ambazo haziharibiki kwa uharaka.

Ndio kuna gharama ila tupate kitu kizuri maana hii nayo ni kero nyingine.
 
Back
Top Bottom