Kuna nafasi aliipata Mzize akiwa na golikipa mbele yake! Angekuwa ile nafasi ameipata Azizi Kii au Pacome (kama angecheza), basi lilikuwa ni goli la wazi kabisa.
Halafu kuna nafasi nyingine aliipata Kennedy Musonda! Na yeye angekuwa na kasi kama ya Mzize, au utulivu kama wa Pacome; na lenyewe lingekuwa goli kwa Yanga.
All in all, jana Yanga walitengeneza nafasi nyingi za magoli ukilinganisha na hao Mamelodi waliopewa nafasi kubwa ya kushinda kabla ya mchezo! Ni vile tu walikosa utulivu, na pia maamuzi sahihi. Naamini mechi ya marudiano nayo itakuwa ni ngumu sana kwa pande zote mbili.
Na kama Mamelodi Sundowns walifikiri wamepewa mpinzani rahisi na mwepesi, basi watakuwa wamekosea sana. Maana lolote linaweza kutokea kwao kwenye huo mchezo wa marudiano.