Uchambuzi: Hali ya Usalama Duniani chini ya Rais Donald Trump. Ukraine imeambiwa ili kuwe na Amani isahau Crimea na je Dunia imejiandaa vipi

Richard

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
15,692
Reaction score
23,038
Baada ya raisi Donald Trump kushinda uchaguzi mkuu nchini Marekani na kuwa raisi mtarajiwa wa 47 wa taifa hilo kubwa Duniani, nchi kadhaa duniani zimeanza kujiweka sawa.

Baadhi ya nchi hizo ni Russia, Ukraine, Iran na Israeli. Nchi zingine ni pamoja na Nigeria, Eritrea,Sudan na Tanzania.

Nchi nyingi hususan za bara la Ulaya zimekumbwa na sintofahamu kubwa huku viongozi wa nchi hizo wakikutana mjini Budapest nchini Hungary ambapo waziri mkuu wa nchi hiyo Victor Orban ambae ni mmoja wa watu wanomhusudu Donald Trump ametoa kauli ya kumkaribisha kiongozi huyo. Viongozi hao wa Jumuiya ya nchi 27 za Ulaya na NATO wamekutana kwa siku mbili za Alhamisi na Ijumaa (AP Hungary's leader Orbán predicts Trump will end support for Ukraine in comments before EU summit) linaripoti kujadili changamoto watazokutana nazo pale watapoanza kufanya kazi na raisi Trump.

Jana Ijumaa waziri mkuu wa Hungary Victor Orban akatoa kauli kwamba Donald Trump atasitisha kuendelea kutoa msaada kwa Ukraine kwenye vita yake na Russia na kwamba ni lazima viongozi wa Ulaya wafikirie upya juu ya msaada wao wa kijeshi kwa Ukraine.

Mapema leo mshauri mwandamizi wa raisi Donald Trump bwana Bryan Lanza amesema kuwa jitihada kubwa za Marekani katika kutatua mgogoro wa Russia na Ukraine mkazo wake mkubwa utakuwa ni kufatuta amani. Katika mahojiano yake na BBC leo, Trump campaign adviser says Ukraine focus must be peace, not territory, Lanza ambae pia ni mwana stratejia wa chama cha Republican amesema utawala wa Marekani utamuuliza raisi wa Ukraine Volodymyr Zelensky mtazamo wake halisi wa kufikia amani.

Bwana Lanza akaendelea kusema, ikiwa Zelensky atakuja na kauli kwamba kutakuwa na amani tu endapo Russia itarudisha Ukraine basi hiyo itaonyesha Zelensky aleta mzaha. Lanza akamalizia kwa kusema "Crimea imeishakwenda" akimaanisha kwamba Russia imeishaichukua Crimea.

Russia ilitwaa Crimea iliyoko mashariki mwa Ukraine kuwa chini ya himaya yake mwaka 2014. Chama cha Democrats tayari kimetoa shutuma kwa raisi mtarajiwa Donald Trump kwa kuonyesha kuwa tayari kukubali mahitaji ya raisi Vladimir Putin. Mapema mwezi Octoba raisi Zelensky aliwasilisha mpango alouita "Victory Plan" kwenye Bunge la Ukraine mpango alodai unasisitiza Ukraine kutokuwa tayari kuachia majimbo yalochukuliwa na Russia pamoja na kulinda uhuru wake.

Russia kwa upande wake imetoa kauli kuashiria kuwa tayari kuzungumza na kumsikiliza Donald Trump atakuja na mapendekezo yapi, wanaripoti AP. Naibu waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergei Lyabkov amesema Washington na Moscow wamekuwa wakibadishana mawasiliano (Communication Channels).

Nalo Jarida la Wall Street Journal laandika kuwa washauri wa raisi mtarajiwa Donald Trump wamekuwa wakihangaikia ahadi aloitoa bwana Trump kwamba atawarudisha kwenye nchi wanazotoka wale raia wote ambao hawana vibali halali vya kuishi nchini Marekani, https://www.wsj.com/politics/policy/trump-mass-deportation-immigrants-plan-348eaa91?st=56N5g1.

Moja ya nchi kadhaa zingine ambazo zimekuwa na wasiwasi wa namna Donald Trumpo atakavyofanya mawasiliano nazo ni Iran ambayo jana imeshutumiwa kuhusika na mpango wa kutaka kumuua Donald Trump alipokuwa akifanya mikutano yake ya kampeni. Mipango hiyo yadaiwa kufanywa na raia wa Iran aitwae . Waziri wa mambo ya nje wa Iran Abbas Araqchi amekanusha Iran kufanya mpango kama huo na kusema huo ni mpango wa Israeli na wapinzani wa serikali waliopo nje ya Iran katika kutafuta namna ya Marekani kuiruhusu kuendeleza vita kati yao (Reuters, https://www.reuters.com/world/iran-...urges-confidence-building-with-us-2024-11-09/).

Marekani imedai kwamba jeshi la mapinduzi la Iran la IRGC lilihusika kusuka mpango wa kumuua Donald Trump. Katika mpango yadaiwa kuwa IRGC ilifanya mawasiliano na raia wa Iran aitwae Farjad Shakheri mwenye umri wa miaka 51 kufanya mauaji hayo lakini jambo hilo likaahirishwa kwa kudhani kwamba Trmp angeshindwa kwenye uchaguzi.

Baada ya jaribio hilo kufeli, Shakheri alikimbia na kutoroka kwenda Iran ambako amepotelea kusikojulikana huku akiwaacha raia wengine wa waishio Marekani Carlisle Rivera (miaka 49) wa Brooklyn, New York, na Jonathon Loadholt (miaka 36) wa Staten Island wakishtakiwa kwa kupanga mauaji na kutakatisha fedha.

Lakini nchi ambayo yaonekana kutokuwa na wasiwasi sana ni Israeli ambayo ina uhakika wa kuwa karibu zaidi na raisi Donald Trump pale atapoanza kazi rasmi mwezi Januari mwaka 2025, laandika Guardian, Trump’s win boosts chances of Netanyahu remaining in power until Israel’s 2026 elections. Waziri mkuu Benjamin Netanyahu amejihakikishia kuendelea kuwa madarakani hadi mwaka 2026 utakapofanyika uchaguzi mkuu nchini Israeli na khasa baada ya juzi kumfukuza kazi waziri wake wa ulinzi Yoav Gallant ambae ameonekana na Netanyahu kama kikwazo kwa mpango wake wa Gaza (obstacle to progress).

Nchi ya Qatar ambayo imekuwa kama mpatanishi wa mgogoro wa Israeli na Hamas leo imetoa kauli kwamba haitakuwa tayari kutayarisha mazungumzo ya Hamas na Israeli endapo Hamas hawatakuwa wakionyesha kukubali mapendekezo kadhaa watayopewa katika kufikia suluhisho. Tayari ofisi ya Hamas mjini Doha imefungwa. Hamas kwa sasa yajaribu kufungua ofisi katika moja ya nchi za Uturuki, Iran, Mauritania au Algeria.

Ofisi za wizara ya mambo ya nje za nchi kadhaa duniani zimekuwa na wakati mgumu wa kusikia yale yanojiri kupitia njia za mawasiliano za raisi mtarajiwa Donald Trump khasa ya X feed (zamani Twitter) kwani wanadiplomasia wana ufahamu wa tabia ya raisi Trump ya kubadilikabadilika. Hivyo suala la diplomasia na sera ya mambo ya nje ya Marekani kuanzia sasa hakuna anaefahamu itakuwa na sura ipi.

Kwa upande wa China ni wazi kuwa nchi hiyo itakuwa tayari imejiandaa na sheria mpya za tozo kwenye magari yake ya umeme yanoingizwa Marekani lakini kikubwa kikiwa ni tangazo lilotolewa na bodi ya biashara ya Marekani ya US Chambers of Commerce kwamba ifikapo mwaka 2026 magari yote kutoka China hayataruhiwa kuwa na vifaa vya umeme vilofungwa China kwa sababu za kiusalama,
US seeks to ban Chinese software from cars, citing national security concerns. Marekani yahofia magari hayo kuweza kufungwa vifaa mbalimbali vitavotumika kijasusi kama kamera,vipaza sauti, GPS na vifaa vingine ambavyo vitatumia mtandao wa internet.

Kwa upande wa bara la Afrika la mtazamo wake kuhusu ujio wa mara ya pili wa raisi Trump, bara hilo kihistoria halijawahi kutiliwa maanani na tawala za Marekani isipokuwa kwenye suala la rasilimali zake linaandika jarida la African Report, https://www.theafricareport.com/367...ore-africas-2-5bn-people-and-their-resources/. Ingawa yapo madai kwamba Marekani yazidi kupoteza ushawishi wake barani humo kwa China na Russia sababu kubwa ikiwa ni masharti ya ushirikiano kati ya Marekani na nchi za bara hilo pale inaposisitiza nchi zake kufuata masharti ya kimataifa yalowekwa na Marekani yaani Rules International Based Order, utawala bora na sheria za haki za binadamu huku nchi za China na Russia zikifumbia macho masuala hayo na kujali maslahi zaidi.

Mwandishi Adewunmi Emoruwa nae katika mtandao wa open democracy, What Trump’s win means for Africa, aweka mtazamo wake kwamba nchi za Afrika ndo utakuwa mwanzo wa kufanya biashara na uwekezaji na kwa kuzingatia uwezo wa kibiashara na uchumi wa raisi Trump itakuwa rahisi wake kufanya mazungumzo ya kibiashara zaidi na bara la Afrika kuliko kufanya mazungumzo ya kisiasa.

Jiografia ya kisiasa huenda ikawa si mbaya sana ukizingatia kuwa baadhi nchi za Afrika kama Afrika Kusini zamchukulia Donald Trump kama alivyo kwamba kile ukionacho ndicho ukipatacho "What you See is what you get". Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Afrika Kusini Clayson Monyela alimkaribisha raisi mtarajiwa Donald Trumpo kwa kusema kuwa ushirikiano baina ya Marekani na Afrika Kusini utastawi zaidi chini ya utawala wa Trump, ikizingatiwa kuwa wakati wa utawala wake Donald Trump 2017-2022 alimchagua Lana Marks ambae amezaliwa Afrika Kusini kuwa balozi wa Marekani Afrika Kusini, jambo linoonyesha kwamba Donald Trump anatambua umuhimu wa kuwa na mtu kama huyo.

Pia lipo suala la ushirikiano wa kibiashara kati ya Marekani na Afrika (AGOA) ushirikiano ambao waipa Afrika uwezo wa kuuza bidhaa zake katika masoko ya Marekani jambo ambalo limeisaidia Afrika Kusini kuweza kuuza bidhaa zake kama magari, mvinyo na matunda, MSN.

Lakini wengi barani Afrika hawajasahau maneno ya kashfa aloyasema Donald Trump ya shimo la uchafu (shithole countries), pamoja na kutolizingatia kabisa bara hilo, kubinya uhamiaji na kupunguza baadhi ya misaada. Raisi aneondoka Joe Biden amejitahidi kuweka ushirikiano na bara hilo kwa kuwezesha kuwepo miradi kama Lobito ambao ni wa reli inopita katika nchi za Angola, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ikibeba malighafi na kwamba Marekani imewekeza zaidi ya dola bilioni 22, wanaandika bbc Donald Trump and Africa: What does his win mean?.

Hata hivyo Donald Trump pamoja na mambo yake bado katika utawala wake aliwezesha kuanzisha miradi kadhaa barani Afrika kwa ajili ya kuwasaidia wamerekani wanotaka kuwekeza barani humo inoongozwa na Prosper Afrika ambao umeweka miradi ya DFC (development finance corporation ), unosaidia miradi ya maendeleo barani Afrika na sehemu zingine duniani.

Kwenye masuala ya uhamiaji, ulinzi na usalama bara la Afrika litakuwa lipo na wasiwasi kutokana na sera ya kuwarudisha makwao raia wa nchi za Sudan, Eritrea na Nigeria ambao wapo nchini humo kinyume cha sheria. Katika utawala wake wa 2017/2021 Donald Trump aliweka sheria kali za kuzuia wahamiaji wa kutoka nchi za Afrika zikiwemo Nigeria, Eritrea, Sudan na Tanzania. Kwa rekodi ya mwaka 2022 raia wapatao 13,000 kutoka Afrika walirekodiwa kufika katika mpaka wa Marekani na Mexico na hiyo ni kwa mujibu wa idara ya uhamiaji ya Marekani https://www.cbp.gov/newsroom/stats/travel.

Ulinzi na Usalama barani Afrika bado litakuwa ni jambo linoendelea kuleta changamoto barani humo khasa vita ya wenyewe kwa wenyewe baina ya majeshi nchini Sudan, migogoro Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ghasia za kisiasa ziloibuka hivi karibuni nchini Msumbiji ambapo chama cha FRELIMO chatuhumiwa kuchakachua kura.

Pia lipo suala la nchi ya Russia kuendelea kujikita kijeshi katika nchi za Burkina Faso, Mali na Niger kwa kutoa msaada wa kijeshi na vifaa kusaidia nchi hizo kukabiliana na vikundi vya kigaidi ambavyo vimekuwa na makazi yake kwenye jangwa la Sahara. Kwa raisi Trump haifahamiki ataweka sera zipi kukabiliana na raisi Putin kwa kuzingatia kuwa hamchukulii Putin kuwa ni tishio kwake.

Kwa kuhitimisha Dunia bado haijapata khasa kile ambacho bwana Trump amepania kukifanya isipokuwa ni kusubiri aapishwe mwezi Januari 2025. Ila bado nchi nyingi duniani zina muda wa mwezi mmoja na nusu kujipanga upya na kungojea sera mpya ya mambo ya nje ya Marekani.
 
Lengo kuu ni kusitisha vita, na mauaji ya wapiganaji wanaokufa bila sababu ya msingi.

Pande zote mbili zenye vita, wataingia kwenye makubaliano chini ya uongozi au msuluhishi akiwa ni USA.

Na ni lazima wataafikiana tu; kwa sababu pande zote mbili zilishachoka kuwa kwenye vita.​
 
Kwa Russia na Ukraine ni inatafutwa sababu TU ya Win win situation ila pale ni maji marefu.Hapa kwa Israel ndo kwenye sura halisi ya USA na ISRAEL,ni kuzidi kuwaonea zaid hao HAMAS na ndugu zao waarabu pamoja na Persian.Hata Mu-Iran asitegemee kabisa msaada mkubwa toka Russia maana Russia/USA ni nchi zinazoongozwa na watu wengi wenye mlengo wa Israel ambao wanachuki sana,ninawasikitikia sana watu wa Gaza maana wataporwa Rasmi nchi yao kupitia bwana Trump
 
Iran kumpiga Israel wala haitaji support ya urusi.,
In short jeshi la Israel kwenye ground wameachwa mbali hata na jwtz hii nauhakika nayo kabisaa
Kwa Russia na Ukraine ni inatafutwa sababu TU ya Win win situation ila pale ni maji marefu.Hapa kwa Israel ndo kwenye sura halisi ya USA na ISRAEL,ni kuzidi kuwaonea zaid hao HAMAS na ndugu zao waarabu pamoja na Persian.Hata Mu-Iran asitegemee kabisa msaada mkubwa toka Russia maana Russia/USA ni nchi zinazoongozwa na watu wengi wenye mlengo wa Israel ambao wanachuki sana,ninawasikitikia sana watu wa Gaza maana wataporwa Rasmi nchi yao kupitia bwana Trump
 
Waarabu WA buza bwana,Yani Rais wao kauawa,hanniya kauawa Teheran etii Leo Irani ana nguvu,hakuna nchi mashariki ya kati anaweza pigana na israeli
Mwamzoni nilikuwa na wazo kama la kwako nikajq gundua nguvu kubwa ilitumika sana kuifanya isreli iogopwe ila kwa hii vita ya gaza imewaacha uchi halafu uje kulinganisha na irani mtu anarusha missle umbali wa 2000km na bado inalenga shabaha ha west hawana huo uwezo achilia mbali isreli inayoitegemea west kwa kila kitu
 
Baada ya raisi Donald Trump kushinda uchaguzi mkuu nchini Marekani na kuwa raisi mtarajiwa wa 47 wa taifa hilo kubwa Duniani, nchi kadhaa duniani zimeanza kujiweka sawa.

Baadhi ya nchi hizo ni Russia, Ukraine, Iran na Israeli. Nchi zingine ni pamoja na Nigeria, Eritrea,Sudan na Tanzania.

Nchi nyingi hususan za bara la Ulaya zimekumbwa na sintofahamu kubwa huku viongozi wa nchi hizo wakikutana mjini Budapest nchini Hungary ambapo waziri mkuu wa nchi hiyo Victor Orban ambae ni mmoja wa watu wanomhusudu Donald Trump ametoa kauli ya kumkaribisha kiongozi huyo. Viongozi hao wa Jumuiya ya nchi 27 za Ulaya na NATO wamekutana kwa siku mbili za Alhamisi na Ijumaa (AP Hungary's leader Orbán predicts Trump will end support for Ukraine in comments before EU summit) linaripoti kujadili changamoto watazokutana nazo pale watapoanza kufanya kazi na raisi Trump.

Jana Ijumaa waziri mkuu wa Hungary Victor Orban akatoa kauli kwamba Donald Trump atasitisha kuendelea kutoa msaada kwa Ukraine kwenye vita yake na Russia na kwamba ni lazima viongozi wa Ulaya wafikirie upya juu ya msaada wao wa kijeshi kwa Ukraine.

Mapema leo mshauri mwandamizi wa raisi Donald Trump bwana Bryan Lanza amesema kuwa jitihada kubwa za Marekani katika kutatua mgogoro wa Russia na Ukraine mkazo wake mkubwa utakuwa ni kufatuta amani. Katika mahojiano yake na BBC leo, Trump campaign adviser says Ukraine focus must be peace, not territory, Lanza ambae pia ni mwana stratejia wa chama cha Republican amesema utawala wa Marekani utamuuliza raisi wa Ukraine Volodymyr Zelensky mtazamo wake halisi wa kufikia amani.

Bwana Lanza akaendelea kusema, ikiwa Zelensky atakuja na kauli kwamba kutakuwa na amani tu endapo Russia itarudisha Ukraine basi hiyo itaonyesha Zelensky aleta mzaha. Lanza akamalizia kwa kusema "Crimea imeishakwenda" akimaanisha kwamba Russia imeishaichukua Crimea.

Russia ilitwaa Crimea iliyoko mashariki mwa Ukraine kuwa chini ya himaya yake mwaka 2014. Chama cha Democrats tayari kimetoa shutuma kwa raisi mtarajiwa Donald Trump kwa kuonyesha kuwa tayari kukubali mahitaji ya raisi Vladimir Putin. Mapema mwezi Octoba raisi Zelensky aliwasilisha mpango alouita "Victory Plan" kwenye Bunge la Ukraine mpango alodai unasisitiza Ukraine kutokuwa tayari kuachia majimbo yalochukuliwa na Russia pamoja na kulinda uhuru wake.

Russia kwa upande wake imetoa kauli kuashiria kuwa tayari kuzungumza na kumsikiliza Donald Trump atakuja na mapendekezo yapi, wanaripoti AP. Naibu waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergei Lyabkov amesema Washington na Moscow wamekuwa wakibadishana mawasiliano (Communication Channels).

Nalo Jarida la Wall Street Journal laandika kuwa washauri wa raisi mtarajiwa Donald Trump wamekuwa wakihangaikia ahadi aloitoa bwana Trump kwamba atawarudisha kwenye nchi wanazotoka wale raia wote ambao hawana vibali halali vya kuishi nchini Marekani, https://www.wsj.com/politics/policy/trump-mass-deportation-immigrants-plan-348eaa91?st=56N5g1.

Moja ya nchi kadhaa zingine ambazo zimekuwa na wasiwasi wa namna Donald Trumpo atakavyofanya mawasiliano nazo ni Iran ambayo jana imeshutumiwa kuhusika na mpango wa kutaka kumuua Donald Trump alipokuwa akifanya mikutano yake ya kampeni. Mipango hiyo yadaiwa kufanywa na raia wa Iran aitwae . Waziri wa mambo ya nje wa Iran Abbas Araqchi amekanusha Iran kufanya mpango kama huo na kusema huo ni mpango wa Israeli na wapinzani wa serikali waliopo nje ya Iran katika kutafuta namna ya Marekani kuiruhusu kuendeleza vita kati yao (Reuters, https://www.reuters.com/world/iran-...urges-confidence-building-with-us-2024-11-09/).

Marekani imedai kwamba jeshi la mapinduzi la Iran la IRGC lilihusika kusuka mpango wa kumuua Donald Trump. Katika mpango yadaiwa kuwa IRGC ilifanya mawasiliano na raia wa Iran aitwae Farjad Shakheri mwenye umri wa miaka 51 kufanya mauaji hayo lakini jambo hilo likaahirishwa kwa kudhani kwamba Trmp angeshindwa kwenye uchaguzi.

Baada ya jaribio hilo kufeli, Shakheri alikimbia na kutoroka kwenda Iran ambako amepotelea kusikojulikana huku akiwaacha raia wengine wa waishio Marekani Carlisle Rivera (miaka 49) wa Brooklyn, New York, na Jonathon Loadholt (miaka 36) wa Staten Island wakishtakiwa kwa kupanga mauaji na kutakatisha fedha.

Lakini nchi ambayo yaonekana kutokuwa na wasiwasi sana ni Israeli ambayo ina uhakika wa kuwa karibu zaidi na raisi Donald Trump pale atapoanza kazi rasmi mwezi Januari mwaka 2025, laandika Guardian, Trump’s win boosts chances of Netanyahu remaining in power until Israel’s 2026 elections. Waziri mkuu Benjamin Netanyahu amejihakikishia kuendelea kuwa madarakani hadi mwaka 2026 utakapofanyika uchaguzi mkuu nchini Israeli na khasa baada ya juzi kumfukuza kazi waziri wake wa ulinzi Yoav Gallant ambae ameonekana na Netanyahu kama kikwazo kwa mpango wake wa Gaza (obstacle to progress).

Nchi ya Qatar ambayo imekuwa kama mpatanishi wa mgogoro wa Israeli na Hamas leo imetoa kauli kwamba haitakuwa tayari kutayarisha mazungumzo ya Hamas na Israeli endapo Hamas hawatakuwa wakionyesha kukubali mapendekezo kadhaa watayopewa katika kufikia suluhisho. Tayari ofisi ya Hamas mjini Doha imefungwa. Hamas kwa sasa yajaribu kufungua ofisi katika moja ya nchi za Uturuki, Iran, Mauritania au Algeria.

Ofisi za wizara ya mambo ya nje za nchi kadhaa duniani zimekuwa na wakati mgumu wa kusikia yale yanojiri kupitia njia za mawasiliano za raisi mtarajiwa Donald Trump khasa ya X feed (zamani Twitter) kwani wanadiplomasia wana ufahamu wa tabia ya raisi Trump ya kubadilikabadilika. Hivyo suala la diplomasia na sera ya mambo ya nje ya Marekani kuanzia sasa hakuna anaefahamu itakuwa na sura ipi.

Kwa upande wa China ni wazi kuwa nchi hiyo itakuwa tayari imejiandaa na sheria mpya za tozo kwenye magari yake ya umeme yanoingizwa Marekani lakini kikubwa kikiwa ni tangazo lilotolewa na bodi ya biashara ya Marekani ya US Chambers of Commerce kwamba ifikapo mwaka 2026 magari yote kutoka China hayataruhiwa kuwa na vifaa vya umeme vilofungwa China kwa sababu za kiusalama,
US seeks to ban Chinese software from cars, citing national security concerns. Marekani yahofia magari hayo kuweza kufungwa vifaa mbalimbali vitavotumika kijasusi kama kamera,vipaza sauti, GPS na vifaa vingine ambavyo vitatumia mtandao wa internet.

Kwa upande wa bara la Afrika la mtazamo wake kuhusu ujio wa mara ya pili wa raisi Trump, bara hilo kihistoria halijawahi kutiliwa maanani na tawala za Marekani isipokuwa kwenye suala la rasilimali zake linaandika jarida la African Report, https://www.theafricareport.com/367...ore-africas-2-5bn-people-and-their-resources/. Ingawa yapo madai kwamba Marekani yazidi kupoteza ushawishi wake barani humo kwa China na Russia sababu kubwa ikiwa ni masharti ya ushirikiano kati ya Marekani na nchi za bara hilo pale inaposisitiza nchi zake kufuata masharti ya kimataifa yalowekwa na Marekani yaani Rules International Based Order, utawala bora na sheria za hakiza binadamu huku nchiza China na Russia zikifumbia macho masuala hayo na kujali maslahi zaidi.

Mwandishi Adewunmi Emoruwa nae katika mtandao wa open democracy, What Trump’s win means for Africa, aweka mtazamo wake kwamba nchi za Afrika ndo utakuwa mwanzo wa kufanya biashara na uwekezaji na kwa kuzingatia uwezo wa kibiashara na uchumi wa raisi Trump itakuwa rahisi wake kufanya mazungumzo ya kibiashara zaidi na bara la Afrika kuliko kufanya mazungumzo ya kisiasa.

Jiografia ya kisiasa huenda ikawa si mbaya sana ukizingatia kuwa baadhi nchi za Afrika kama Afrika Kusini zamchukulia Donald Trump kama alivyo kwamba kile ukionacho ndicho ukipatacho "What you See is what you get". Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Afrika Kusini Clayson Monyela alimkaribisha raisi mtarajiwa Donald Trumpo kwa kusema kuwa ushirikiano baina ya Marekani na Afrika Kusini utastawi zaidi chini ya utawala wa Trump, ikizingatiwa kuwa wakati wa utawala wake Donald Trump 2017-2022 alimchagua Lana Marks ambae amezaliwa Afrika Kusini kuwa balozi wa Marekani Afrika Kusini, jambo linoonyesha kwamba Donald Trump anatambua umuhimu wa kuwa na mtu kama huyo.

Pia lipo suala la ushirikiano wa kibiashara kati ya Marekani na Afrika (AGOA) ushirikiano ambao waipa Afrika uwezo wa kuuza bidhaa zake katika masoko ya Marekani jambo ambalo limeisaidia Afrika Kusini kuweza kuuza bidhaa zake kama magari, mvinyo na matunda, MSN.

Lakini wengi barani Afrika hawajasahau maneno ya kashfa aloyasema Donald Trump ya shimo la uchafu (shithole countries), pamoja na kutolizingatia kabisa bara hilo, kubinya uhamiaji na kupunguza baadhi ya misaada. Raisi aneondoka Joe Biden amejitahidi kuweka ushirikiano na bara hilo kwa kuwezesha kuwepo miradi kama Lobito ambao ni wa reli inopita katika nchi za Angola, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ikibeba malighafi na kwamba Marekani imewekeza zaidi ya dola bilioni 22, wanaandika bbc Donald Trump and Africa: What does his win mean?.

Hata hivyo Donald Trump pamoja na mambo yake bado katika utawala wake aliwezesha kuanzisha miradi kadhaa barani Afrika kwa ajili ya kuwasaidia wamerekani wanotaka kuwekeza barani humo inoongozwa na Prosper Afrika ambao umeweka miradi ya DFC (development finance corporation ), unosaidia miradi ya maendeleo barani Afrika na sehemu zingine duniani.

Kwenye masuala ya uhamiaji, ulinzi na usalama bara la Afrika litakuwa lipo na wasiwasi kutokana na sera ya kuwarudisha makwao raia wa nchi za Sudan, Eritrea na Nigeria ambao wapo nchini humo kinyume cha sheria. Katika utawala wake wa 2017/2021 Donald Trump aliweka sheria kali za kuzuia wahamiaji wa kutoka nchi za Afrika zikiwemo Nigeria, Eritrea, Sudan na Tanzania. Kwa rekodi ya mwaka 2022 raia wapatao 13,000 kutoka Afrika walirekodiwa kufika katika mpaka wa Marekani na Mexico na hiyo ni kwa mujibu wa idara ya uhamiaji ya Marekani https://www.cbp.gov/newsroom/stats/travel.

Ulinzi na Usalama barani Afrika bado litakuwa ni jambo linoendelea kuleta changamoto barani humo khasa vita ya wenyewe kwa wenyewe baina ya majeshi nchini Sudan, migogoro Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ghasia za kisiasa ziloibuka hivi karibuni nchini Msumbiji ambapo chama cha FRELIMO chatuhumiwa kuchakachua kura.

Pia lipo suala la nchi ya Russia kuendelea kujikita kijeshi katika nchi za Burkina Faso, Mali na Niger kwa kutoa msaada wa kijeshi na vifaa kusaidia nchi hizo kukabiliana na vikundi vya kigaidi ambavyo vimekuwa na makazi yake kwenye jangwa la Sahara. Kwa raisi Trump haifahamiki ataweka sera zipi kukabiliana na raisi Putin kwa kuzingatia kuwa hamchukulii Putin kuwa ni tishio kwake.

Kwa kuhitimisha Dunia bado haijapata khasa kile ambacho bwana Trump amepania kukifanya isipokuwa ni kusubiri aapishwe mwezi Januari 2025. Ila bado nchi nyingi duniani zina muda wa mwezi mmoja na nusu kujipanga upya na kungojea sera mpya ya mambo ya nje ya Marekani.
Ukraine aliiacha Crimea kitambo ila Urusi alitaka eneo zaid ndo shida ilianzia hapo
 
Urusi wanairudisha nyuma Dunia enzi za Goliati na Daudi,yaani mwenye nguvu anaweza kuongeza enao la nchi yake anavyo taka,Hali hiyo haiheshimu mipaka ya nchi Dunia ikenda huko basi vita zitakuwa nyingi sana ni heri Dunia ikaungana kupinga Hilo Putuni hafai
 
Mnatuchosha xx ,
Kwani huyo Trump ndio rais wa dunia au wamerekani
 
Binafsi naona Ukraine akikubali kuachia Crimea na huku akirudishiwa mikoa yote minne yaani kheson Donetsk, Lugansk,zapolzhia, itakuwa ni favor kubwa sana kwake
 
Kama ni hivyo Urusi itakuwa imetoa taswira mbaya sana Duniani, sasa Nchi yoyote yenye nguvu inaweza kumvamia jirani yake na kuteka eneo lolote ilitakalo na kusema kuwa ni lake.
 
Kama ni hivyo Urusi imetoa taswira mbaya sana Duniani sasa Nchi yoyote yenye nguvu inaweza jirani yake na kuteka eneo lolote ilitakalo na kusema kuwa ni lake.
Mkuu, hata Marekani wenyewe wametoa taswira mbaya sanakwa kuwaachia Israeli waue watu wanavyopenda huko Gaza na sasa Lebanon.

Ni wazi kabisa kinofanyika ni uhalifu wa kivita lakini hata UN mikono imefungwa.
 
Binafsi naona Ukraine akikubali kuachia Crimea na huku akirudishiwa mikoa yote minne yaani kheson Donetsk, Lugansk,zapolzhia, itakuwa ni favor kubwa sana kwake
Kwa Trump Ukraine watakuwa hawana Choice ni kukubali tu masharti mapya.

Lakini pia huenda Marekani wakagawana Ukraine na Russia na Ukraine ikaachiwa upande wa Magharibi ambako huenda kukawekwa Buffer zone.

Ila Donbass imekwenda pamoja na majimbo yote uloyataja.
 
Back
Top Bottom