Uchambuzi huru wa mchezaji mmoja mmoja

Uchambuzi huru wa mchezaji mmoja mmoja

mzee wa kijiwe

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2012
Posts
947
Reaction score
685
ASahau habari ya Makambo ambaye ndiye mchezaji anayeongelewa kwa wingi sasa hapa Tanzania, Sahau habari ya Tambwe mchezaji tishio kwa wana Msimbazi wote, yupo mchezaji ambaye ndiye roho ya wana Jangwani kwa sasa, huyu ndiye aliyekuwa anakosekana kwenye timu yetu ya Taifa ili kuleta uwiano mzuri kati ya washambuliaji na viuongo wachambuliaji

Hapa sii mzungumzii mwingine Bali ni Ibrahim Ajib kiungo mshambuliaji mwenye kuweza kuudhibiti mpira mguuni na mpira ukamtii, mwenye uwezo wa kuinua kichwa na kuona mahali sahihi aliposimama mshambuliaji wa timu yake. Ajib wa sasa amezaliwa upya, huyu anayo pumzi na stamina, anakimbia pande zote za uwanja bila kuchoka lakini anayo sifa kuu moja ambayo ndiyo inayompambanua na aina ya viungo wengine waliopo hapa nchini kwa sasa.

Ajib anapiga pasi za nwisho maarufu kama assists ambazo ni chakula kwa washambuliaji wengi.

Kwa muda mwingi nchi yetu ilikosa vyakula vya namna hii, Samata Leo hii angekuwa amevunja rekodi zote za Taifa hili katika ufungaji kama angecheza na huyu Ajib wa Leo. Kazi yake ingelikuwa ni rahisi sana, kucheka na nyavu.

Mlimwona Makambo kwenye mechi ile ya Yanga na Costal Union? Kwa wale walioitizama ile mechi hawawezi kusahau kamwe kile ambacho Ajib alikifanya. Unajua ni kwanini Makambo aliomba kutoka uwanjani? Wengine watasema eti Makambo aliumia ,hakuna kitu kama hicho. Makambo aliomba poo kwa lugha yetu ya mtaani.Ajib alipeleka chakula kingi kuzidi uwezo wa mlaji, Ajib alipiga mipira yote kwa Makambo, na mipira asilimia tisini ilimfikia Makambo, ilimlazimu Makambo kukimbia kulia, kushoto na katikati, ukweli ni kwamba Ajib alimchosha sana Makambo.

Ubora wa Tambwe kwenye mechi kati ya Yanga na Singida United umetokana kwa sehemu kubwa na kazi murua ya Ajib.

Ni kiungo yupi mshambuliaji anayeweza kuuleta mipira juu ya kichwa cha mfungaji kama Ajib? Ajib anapiga pasi zile zinazo katiza uwanja, nimeziona pasi za Ajib zinafanana kabisa na pasi anazopiga Pogba pale OT na pia Alex Sancches.

Nasubiria kumwona Ajib wa tarehe 30/9 pale uwanja wa Taifa, nasubiria kumsikia kocha mkuu wa Taifa stars Amunike akichanga karata zake za jinsi ya kuelekea Afcon 2019, Ajib amebeba siri ya mafanikio ya Amunike, sitegemei kumshauri Amunike ili amwite Ajib kwenye kikosi chake, nilimwona Amunike pale uwanja wa Taifa akicheka kila Ajib alipogusa mpira, kichwani niliwaza Amunike hayupo pale uwanjani bali mawazo yake yote yalirudi nyuma miaka kumi iliyopita pale Nigeria ilipokuwa ikifanya mambo makubwa chini ya kiungo mshambuliaji asiye na mfano JJ Okocha.

Je Ajib nguvu za soda? Ni swala la muda tuu, hii ni mechi yake ya NNE akitoa assist mfululizo na yeye mwenyewe akifunga moja ya magoli ambayo yataingia kwenye kinyanganyiro cha goli bora la msimu.

Huu ni uchambuzi huru mitandaoni wa mwanamichezo
Peter John
0715829576
 
Vipi tena mlipiga kelele kuhusu Tshishimbi mkafungwa na Simba, sasa mmemgeukia Ajib. Huyo Ajib hajawahi kupata ushindi dhidi ya Simba akiwa na Yanga, sababu kubwa ni kuwa kiungo huwa kinamilikiwa na Simba, hata mechi ya jumapili kiungo kitamilikiwa na Simba maana ndio wenye viungo bora zaidi.
Ajibu mmoja = Mkude+Chama+MO+Niyonzima+Ndemla+Kotei
 
Vipi tena mlipiga kelele kuhusu Tshishimbi mkafungwa na Simba, sasa mmemgeukia Ajib. Huyo Ajib hajawahi kupata ushindi dhidi ya Simba akiwa na Yanga, sababu kubwa ni kuwa kiungo huwa kinamilikiwa na Simba, hata mechi ya jumapili kiungo kitamilikiwa na Simba maana ndio wenye viungo bora zaidi.
Naona Mbumbumbu FC hamuachi asili yenu kwa kuishi kwa matumaini Kwa kutumia past events,ngoja Jumapili ifike.
 
Naona Mbumbumbu FC hamuachi asili yenu kwa kuishi kwa matumaini Kwa kutumia past events,ngoja Jumapili ifike.
Wala huna haja ya kuniita mbumbumbu, siku zote past events (data) huwa zinatumika kudetermine future outcomes, hilo utakuwa unalijua kama umeenda shule.
Hapa naongelea records, mara nyingi Simba wanapocheza na Yanga na hasa miaka ya hivi karibuni Simba huwa wanamiliki zaidi katikati na kuwafanya wachezaji wa kati wa Yanga kushindwa kucheza mpira vizuri. Na kulingana na ubora wa viungo wa Simba hata kwenye mechi ya kesho kutwa Simba watamiliki mpira zaidi kati kuliko Yanga na hiyo itapelekea Ajibu kutolewa kwa kushindwa kucheza mpira. Hiyo ni analysis, naomba na wewe utoe analysis yako, usitukane matusi wala usiropoke kwa sababu hapa tupo JF.
 
Ajibu,Fei,Tshishimbi vs Mkude,Chama,Kotei.....kazi IPO...ninachokiona Mkude na Chama wako slow sana ..huyu Kotei anajua kucheza rafu tu(Nashangaa Mghana gani hana maajabu..huyu atakuwa muhamiaji Ghana)..anyways 4-3-3 ya Yanga itawasumbua sana mikia,maana mbele kutakuwa na Makambo,Tambwe na Ngasa...Ila mpira dk 90..
 
Uchambuzi mzuri, Simba kutokana na aina ya wachezaji wa viungo walionao ndio watakaoamua mpira uchezwe kwa kasi au la, kama Yanga wataamua kucheza mpira wa kasi bila umiliki wataishia kupiga mbele na kukimbiza. Hata hivyo Simba wanaweza kumchezesha Dilunga nyuma ya mastrikers wawili, huyu mtu ni hatari sana, ana kasi ya ajabu na uwezo mkubwa sana wa kupiga pasi za mwisho na hata kufunga. Kama ulivyosema end of the day dk 90 zitaamua.
 
Wala huna haja ya kuniita mbumbumbu, siku zote past events (data) huwa zinatumika kudetermine future outcomes, hilo utakuwa unalijua kama umeenda shule.
Hapa naongelea records, mara nyingi Simba wanapocheza na Yanga na hasa miaka ya hivi karibuni Simba huwa wanamiliki zaidi katikati na kuwafanya wachezaji wa kati wa Yanga kushindwa kucheza mpira vizuri. Na kulingana na ubora wa viungo wa Simba hata kwenye mechi ya kesho kutwa Simba watamiliki mpira zaidi kati kuliko Yanga na hiyo itapelekea Ajibu kutolewa kwa kushindwa kucheza mpira. Hiyo ni analysis, naomba na wewe utoe analysis yako, usitukane matusi wala usiropoke kwa sababu hapa tupo JF.
Nipe records za jumla Kati ya Simba na Yanga ni nani aliemfunga mwenzake goals nyingi,match nyingi na kuchukua ubingwa mara nyingi zaidi ya mwenzake.
 
Back
Top Bottom