Kibosho1
JF-Expert Member
- Dec 12, 2017
- 2,621
- 4,293
Kwa mujibu wa BBC
Kwakweli ndio maana Urusi inapaswa kukubali tu yaishe kama Poland itapeleka Leopard 2 Uingereza itapeleka Chalenger Us ikapeleka Abram,T90 ya Urusi haitakuwa na kazi tenaKwa nini Leopard 2?
Kifaru cha Leopard ndicho chaguo bora kwa Ukraine, kwani ndicho kinachotumika sana na kimeenea zaidi kati ya nchi za Ulaya ambazo ni wanachama wa NATO, kwani kwa sasa kuna zaidi ya vifaru 2,300 ya mifano mbalimbali inayotumika katika majeshi ya nchi hizi na inaweza kwa urahisi kusafirishwa hadi katika ardhi ya Ukraine.
Kifaru hiki kinatumia risasi za NATO, na risasi hizi zinaweza kupatikana kwa idadi inayofaa kutoka kwa nchi yoyote ya NATO, pamoja na nchi hizi kuwa na idadi kubwa ya risasi hizi, na vifaru vya Marekani aina ya M1 Abrams ambavyo pia hutumia risasi sawa na Leopard 2, na kwa hivyo Marekani inaweza kutoa risasi za vifaru hivi.
Ingawa mfano wa kwanza wa kifaru cha Leopard uliingia katika huduma zaidi ya miongo minne iliyopita, ilipata michakato mingi ya maendeleo na ya kisasa, na kuwa mojawapo ya kifaru bora zaidi ulimwenguni kwa suala la usahihi wa kutumia, ulinzi na wepesi. Inatumiwa na majeshi ya nchi 18 kote duniani, ikiwa ni pamoja na Qatar, Singapore, Indonesia na Chile. Canada, pamoja na majeshi mengi ya Ulaya
Souce: BBC News Swahili