Matanga
JF-Expert Member
- Nov 13, 2019
- 2,281
- 3,976
UCHAMBUZI KUELEKEA DERBY
YA KARIAKOO
________________________________
Waliouzungumza wamezungumza, waliotamba wametamba sana na waliochambua bado tunachambua maana heshima ya mpira ni baada ya dakika 90, sio maneno ya mtaani wala vijiweni, matambo na majigambo hayana nafasi kabla ya dakika 90,
Kwangu ninayo ya kuzungumzia kuhusu derby hii lakini nayoyazungumza sio msimamo wa dakika 90 maana hapa tunazungumzia kile kilichoonekana nyuma na matarajio ya kitatokea nini na nini kinachotakiwa kufanywa na timu hizi kuelekea derby hii,
Kwa upande wa Simba Sc
Wamekuja na slogan ya One touch, pengine hii ni kutokana na aina ya soka wanalolicheza kwa sasa, simba wanacheza mpira wa pasi nyingi haswa eneo la katikati nyuma yao, mipango yao huanzia hapa maana unaweza kuwaona kama wanacheza show game lakini move ya kuondoka kuelekea nusu ya uwanja wa lango la mpinzani huwa na madhara makubwa,
Kwa style hii imekuwa na faida kwao ukizingatia wana viungo wengi wabunifu, mpira hamsubiri Chama au kahata au Sharaaf Shiboub kuupeleka kwenye nafasi walizokaa washambuliaji, kiungo yeyote wa simba ana uwezo wa kupiga pasi za mwisho kwa usahihi, hapa wapinzani unashindwa umfanyie nani marking maana simba inamiliki aina ya viungo wajanja wajanja sana, ndio maana hata kufunga wanafunga sana maana wanafanya overlap kwenye maeneo mengi,
Final third, hili eneo kwa msimu huu limekuwa sio hatarishi sana kulinganisha na msimu jana, lakini ujio wa Deo Kanda umekuwa na uhai kwa siku za karibuni, awali hakuonekana mtu mwenye madhara lakini kwa sasa huyu ndiye mtu hatari kuliko medie Kagere, ni mwepesi, ana kasi, ana dribbling nzuri halafu muda wote anawaza kuingia kwenye box, hii ni hatari sana kama akitumiwa vyema,
Kiujumla simba wana chemistry nzuri lakini wanapokutana na timu ambayo inacheza soka la kupamia huwa wanakosa ule umakini na kujikuta wakiondoka kwenye soka lao na hii inatakiwa kuwa mbinu ya kwanza ya Yanga kwa siku ya leo.
Kwa upande wa Yanga
Yanga inacheza Direct football, hili ni soka ambalo halihitaji kufanya possession nyingi wala movement nyingi kwenye nusu ya eneo lao, ni soka ambalo kila mchezaji akiupata mpira humuhitaji kukimbia nao kuelekea mbele ndio maana unaona watu kama mrisho Ngassa wamekuwa wanafiti sana kwa sababu ya aina ya soka analocheza,
Hii ni nature ya klabu kwa miaka yote lakini kwa misimu ya karibuni wamekuwa wakifeli kwa sababu wanawakosa mawinga wenye kasi kubwa na uwezo wa kuuchezea mpira,
Utaona mtu kama Sibomana ana uwezo mzuri lakini nature ya timu inamfanya tusione kile alichonacho, kwa mechi ya leo mtu atayeleta madhara kwa simba ni Ngassa, sio kwamba Ngassa ana uwezo mkubwa kuliko akina Molinga au Sibomana, Ngassa atabebwa na nature ya klabu
Idara ya kiungo ambayo Muhimili mkubwa ni Tshishimbi, inatakiwa Mkwassa kupanga Double pivot eneo la chini, yaani makame na Tshishimbi wacheze kama viungo wakabaji, ukizingatia kwamba Makame analiweza soka la kupamia, halafu juu yao ndio waweke kiungo mwingine wa kuiunganisha timu Niyonzima/ Balama Mapinduzi,
Hii inamaanisha, kwakuwa mipango na ngumvu kubwa ya simba inaanzia katikati, basi Yanga wanatakiwa kuja na mbinu ya kuwavuruga Simba eneo la katikati ili wawalazimishe Simba kucheza Direct football, soka ambalo kwa simba hawaliwezi, wakifanikiwa hapa wanaweza kuondoka na ushindi,
Asikudanganye mtu kuwa kila soka la kujilinda ni kupaki basi, unaweza kucheza kwa kushambulia lakini ukiwa unajilinda, ni namna gani tu wachezaji wako watakuwa wepesi kufanya coverage pindi wanapopoteza mpira, lakini pia soka la kujilinda ambalo timu hulicheza linamuhitaji mcheza kucheza akisaziba nafasi yake huku akilinda nafasi ya mwingine, yaani wachezaji wanatekeleza majukumu mawili kwa pamoja, hivyo basi, Yanga pia wanaweza kucheza soka la aina hii na kuwafanya simba kuwa bize kulinda kuliko kushambulia, tatizo la soka la aina hii ni pale ambapo Yanga watachoka,
Kwa Ujumla Wake
Kwa maana ya uzoefu, wachezaji wa simba wana uzoefu mkubwa kuliko wachezaji wa Yanga,
Kikosi cha Simba kimecheza kwa pamoja kwa muda sasa, wamecheza mechi nyingi tena zenye presha na wamekuwa hawatoki mchezoni, hivyo presha ya mechi hii usitegemee Simba wakatoka mchezoni, wamecheza mechi za ugenini kubwa na nyingi licha ya Figisu na joto la mechi hawakutoka mchezoni, walifungwa kwa kuzidiwa uwezo sio kwa sababu ya presha ya mechi, hivyo hata Yanga wakija na mbinu za kuwatoa kimchezo naamini hawatafanikiwa,
Tofauti iliyopo Yanga ni kuwa kuna mambo mengi nje ya uwanja ambayo hayapo sawa, usisahau kwamba mambo ya nje ya uwanja yana athari zake ndani ya uwanja, lakini hata wachezaji wao wengi wanaotegemewa kutumika leo hawajatengeneza muunganiko mzuri, lakini pia wana wachezaji wengi ambao hawajaonja joto la mechi kubwa kama hizi, kwa maana hiyo ni rahisi Yanga ukawatoa mchezoni kuliko simba,
Mechi hii inahitaji utulivu, umakini, na heshima kwa mpinzani ili kuicheza, na hupaswi kuamini umeshinda kabla ya Kipyenga cha mwamuzi kupulizwa maana kosa moja likitumika vyema ni adhabu kwa mkosaji, timu zote zinatakiwa kuingia kwa heshima kubwa ili ziweze kutekeleza majukumu pewa,
All in all karata yangu naitupa kwa Simba kushinda leo, ikitokea simba kufungwa ndio ile tunasema mpira haujadunda ila umedundishwa.
____________________
Kama ulichelewa kuileta usione gere jilaumu kwa uzembe wako [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sent using Jamii Forums mobile app