UCHAMBUZI: La Casa De Papel (Money Heist) S04

Chachasteven

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2014
Posts
1,941
Reaction score
2,044
Noma! Hayawi hayawi, leo yamekuwa. Baada ya kutikisa kwa seasons tatu mfululizo, La Casa De Papel au Money Heist imerudi tena mjini na NetFlix washaweka Season 04 kwenye platform yao.

Tukikumbushia kidogo na fasta sehemu ya tatu ilivyokuwa: Kundi la Profesa linaingia Benki kuu ya Hispania kwa sababu kuu mbili. Moja kutimiza ndoto ya Berlin ambaye ni marehemu. Na pili kumuokowa Rio ambaye alikamatwa na maaskari kwa sababu ya uzembe na mapenzi baada ya kukimbilia kusikojulikana.

Hata hivyo, Askari wanaleta vitimbwi na vikwazo kwenye mpango mzima wa Profesa na anajikuta kwenye mazingira magumu mpaka sehemu ya tatu inapoisha - Profesa anaamini polisi wamemuua demu wake, Raquel. Asichokijua ni kwamba ule ni mtego wa kumvuta ili anaswe. Kule benki pia, Nairobi alikuwa anapigania dakika za mwisho za uhai wake baada ya kupigwa shaba na askari.! Swali ni kwamba atapona au vipi? Profesa atanaswa au atachomoka?

Sasa Season 04 inayo majibu yote. Inaanzia pale ambapo Alex Pina alituacha tumepagawa. Nitahakikisha siharibu uhondo wote kwa wale ambao bado hamjakutana na hii sehemu ya nne, Kwa hivyo nitawapa ubuyu kidogo tu.

Kwa ufupi ni kwamba, Season 04 imekaa kibabe sana. Kuna sapraizi za kutosha kadri inavyofunguka, huku ikiwa imeshirikisha nyimbo za kimahaba za Kiingereza zilizotamba miaka ya 80 huko. Unatakiwa utegemee kuona vitu vya kushtusha - Unaweza kudhani unatazama filamu ya kutisha. Unatamani wahusika wafanye maamuzi kwa akili zao kuliko hisia, lakini huo ndiyo utamu wenyewe wa filamu...

Kinachofanya S04 iwe lazima kuitazama ni kwa sababu season 3 zilizopita Profesa ndiyo alikuwa bwana mipango. Hata pale ambapo mambo yalikuwa yanayumba, Lazima alikuwa anakuja na mpango wa kuokoa jahazi mapema. Lakini kwenye Season 03 mipango yake yote ilifeli na uwezo wa yeye kuja na namna ya kuokoa jahazi unakuwa kidogo sana awamu hii, kiasi ni ngumu kujiokoa hata yeye mwenyewe, achilia mbali kuokoa kundi lake.

Sababu ni nyingi, ila kubwa ni kwamba, Plan nzima ya kuvamia Benki kuu ya Hispania lilikuwa sio wazo lake ila la Berlin ambaye ni marehemu. Kwa hivyo taarifa za plan nzima zinakuwa haziko kamili kwenye kichwa chake. Pia, Inspekta Alicia Serria {Najwa Nimri} ambaye ni mjanja na ana akili nyingi pia, anayo hamu sana ya kumkomesha Profesa (Hapa ndiyo utaamini mwanaume usishindane na mwanamke). Hiyo inalifanya liwe ni swala la kufa na kupona kwa malaika wetu mtetezi, Profesa.

Hitimisho: Taarifa nyingine ni kwamba Season 05 ipo njiani, ingawa NetFlix hawajathibitisha, ila ndiyo inavyoonekana. Muda wa kumuwambia Professor na wanawe Bella Ciao bado haujafika.
 
Rio na yule manzi wake walikua wapuuzi, sema kuna sehemu nimeona Nairobi amepigwa shaba ya kichwa, aisee namzimia sana huyo dada. All in all ngoja tuone akili ya Prof this season.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gandia angekuwa upande wa professor bhanaaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] jamaaa linajua mpaka aibu
 
Gandia angekuwa upande wa professor bhanaaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] jamaaa linajua mpaka aibu
Ila tatizo ana makeke ya kimbuzi sana, kama angetulia angewauwa wote wale kimya kimya maana alikuwa na silaha za kutosha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Reactions: Lee
Gandia angekuwa upande wa professor bhanaaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] jamaaa linajua mpaka aibu
Baharia kwa nini mmedump ile forum?
 
Reactions: Lee
Najiuliza kama Gandia alikua panic room na professor alijulishwa na Antonniaz, sasa kwanini asinge waambia watu wake waongozane na governor akawaoneshe hiyo panic room ilipo kama walikua hawapajui..kwa kweli hapa professor aliyumba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…