Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,112
- 34,951
Wakili Maduhu William Amechambua kuhusu kuitwa kwa CDF JACOB MKUNDA,,IGF CAMILLIUS WAMBURA NA DCI RAMADHAN KINGAI NA UTETEZI DHIDI YA KESI YA UHAIN NAYOMKABILI MHE LISSU
Na haya ndio maswali matatu mazito
Kwanza Je Jamhuri wanayo nafasi ya kukata rufaa juu ya haya Maamuz ya Mahakama? Na je iwapo kweli wataenda kutoa ushahidi kisha wakamgeuka Lisu nini kitatokea:
Nikamuuliza tena wakili wanaweza kuwakilishwa au ni lazima wafike Mahakamani wao wenyewe
Mwisho iwapo hawataenda Wanaweza kutolewa amri na Mahakama va kukamatwa? Yaani Mkuu wa Majeshi,DCI na IGP:
Haya hapa majibu ya wakili
kwanza ujue Mlango pekee walio nao upande wa Jamhuri ili kuwanasua mashahidi hawa ili wasije Mahakamani ni kukimbilia Mahakama ya Rufani kwa njia ya mapitio( Revision) kama nawajaridhika na uamuzi huo,, nje ya hapo hawana namna.
Ila ikitokea IGP Wambura, CDF Mkunda na DC Ramadhan Kingai wakakaidi wito wa Mahakama nini kitatokea??
Kwa sababu IGP, CDF na DCI hawana kinga ama dhidi ya kushitakiwa au kutoa ushahidi Mahakamani( yaani hawa ni both compentent and Compellable witnesses). Kwahiyo hawana namna ni lazima waje Mahakamani na kama watakaidi Mahakama inaweza kutoa wito wa kukamatwa( arrest warrant) au wanaweza kukumbana na mtego wa kosa la kuidharau Mahakama( contemp of Court)
Tatu: Nini kitatokea kama watatii wito wa Mahakama na wakaamua kumgeuka mshitakiwa na kuwa upande wa Jamhuri??
Tukumbuke hawa ni mashahidi wanakuja kwa ajil ya utetezi, hivyo watalazimika kuwa katika mlengo wa kuijenga kesi dhidi ya mshitakiwa na ikitokea wakaamua kumgeuka mshitakiwa( yaani turning into hostile witness) Mhe Lissu atalazimika kuiomba Mahakama awaulize Maswali va Dododo( cross examination) suala ambalo itawafanya wapite kwenye tanulu la moto.
Nne: Je Wanaweza kuja mashahidi kutoa kwa niaba ya CDF, IGP na DCI??
Kwa mujibu wa Sheria za Tanzania hakuna ushahidi unatolewa kwa niaba. Kwa lugha nyingine wito( summons) zitatumwa kwa majina vao binafsi( on their personal capacity) na sio kwa mwamvuli wa taasisi wanazoziongoza. chanzo.BahariaTV