Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Leo tumeshuhudia Shirikisho la Mpira wa miguu Afrika ( CAF) wa upangaji wa hatua ya makundi kombe la Klabu Bingwa Afrika (CAFCL) na Kombe la Shirikisho Afrika ( CAFCCL) ambapo Yanga kwenye Klabu Bingwa Afrika wamepangwa na TP Mazembe DR Congo, Al Hilal ya Sudan na MC Alger ya Algeria.
Kwa upande wa Simba wao kwenye Kombe la Shirikisho Afrika msimuwa 2024/2025 pamoja na CS Sfaxien ya Tunisia, CS Constantine ya Algeria na Fc Bravos ya Angola.
Sasa nitaweka mambo kama matatu ambao Yanga wanapaswa kuyafanya ili wafanikiwe kufuzu hatua ya robo fainali. Kwanza timu ambazo Yanga SC amepangwa nazo si ngeni kabisa maana ya kwamba katika misimu ya hivi karibuni wamekutana katika misimu miwili iliyopita walikutana na TP Mazembe katika kombe la shirikisho na Yanga aliibuka kwa ushindi katika mechi zote za nyumbani na ugenini kwa kumfunga jumla ya magoli manne kwa moja (4 - 1).
Lakini kwa upande mwingine Yanga katika misimu 3 hivi pia walikutana na Al Hilal katika hatua za awali kabisa Yanga alipoteza mbele ya AL Hilal na kushindwa kwenda katika hatua inayofuta. Lakini huyu MC Alger waliwahi kucheza na Yanga misimu kadhaa nyuma na Yanga nakumbuka alipasuka goli 4.
Sasa ukitazama hapa unaona Yanga anafaida ya kuwafahamu wapinzani wao katika hatua hizi za makundi .
1. Yanga SC ahakikishe anashinda mechi zake zote za home ili kuhakikisha anapata nafasi ya kwenda hatua ya Robo fainali. Asikubali yatokee ya msimu uliopita licha alifanikiwa kwenda katika hatua ya robo fainali. Maana alianza nyumbani dhidi ya AL ahly na kulazimishwa sare ya 1 -1, na awamu hii anaanzia home dhidi ya AL Hilal.
2. Kuwaheshimu sana wapinzani katika mechi zao zote ziwe za nyumbani au ugenini ii kujihakikishia nafasi ya kufuzu robo fainali.
3. Kocha na bechi lao lote la ufundi sasa ni wakati wa kuanza kuzifutailia mechi za wapinzani wao kalba awajakutana hii inaweza kuwasidia kufahamu ubora na udhaifu wa wapinzani wao upo vipi na wao kwenda kuyafanyia kazi ili waweze kupata matokeo mazuri kwa kila mchezo.
Timu ya Wananchi naiyona Nusu fainali kama akipita hapa. Ni hayo wadau wa soka!
Soma Pia: CAFCL & CAFCC Group Stage Draw 2024