BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 706
- 1,716
Vijana ni uti wa mgongo wa Taifa la Tanzania na nguzo kuu ya mustakabali wake. Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, zaidi ya asilimia 60 ya Watanzania wana umri chini ya miaka 25, huku takriban asilimia 35 wakiwa vijana wa umri kati ya miaka 15 hadi 35. Takwimu hizi zinaonesha wazi kuwa vijana ndilo kundi kubwa zaidi la wananchi, lenye nafasi ya kubwa katika kuchochea maendeleo ya Nchi kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Hata hivyo, uchunguzi wa mwenendo wa kidemokrasia ndani ya kipindi cha miaka 10 iliyopita unabaini kuwa kundi la vijana limekuwa miongoni mwa waathirika wakubwa wa changamoto za kidemokrasia nchini, ikilinganishwa na makundi mengine ya kijamii. Changamoto hizo zimeacha athari za muda mrefu zilizoelezwa na baadhi ya wadau kama makovu ya kisiasa na kijamii hasa kwa vijana.
Demokrasia katika Mwelekeo Tata
Katika muongo mmoja uliopita, hali ya demokrasia nchini Tanzania imepitia nyakati zenye mabadiliko makubwa. Uchunguzi huu unaonesha kuwa changamoto zimejikita zaidi katika nyenzo kuu za demokrasia, zikiwemo:
Utawala wa sheria
Uhuru wa kujieleza
Ushiriki wa wananchi katika shughuli za kisiasa
Uwepo wa chaguzi huru na za haki
Changamoto katika maeneo haya zimeathiri kwa kiwango kikubwa vijana, ambao kwa asili yao ndio kundi lenye nguvu ya kuhoji, kushiriki na kusukuma mabadiliko ya kijamii na kisiasa.
1. Wimbi la madai ya utekaji wa vijana
Moja ya matukio mazito yaliyoibua wasiwasi mkubwa katika kipindi cha miaka 10 ni wimbi la madai ya kutekwa kwa vijana, matukio ambayo mara nyingi yamehusishwa na misimamo au shughuli za kisiasa.
Baadhi ya vijana waliripotiwa kutekwa na baadaye kuonekana, huku wengine wakidaiwa kupotea kabisa bila maelezo rasmi. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiliripoti kutekwa kwa baadhi ya wanachama wake vijana, akiwemo aliyekuwa kiongozi wa chama hicho, Deusdedit Soka. Madai ya kutekwa kwake yalijitokeza muda mfupi baada ya kuonekana akitoa kauli za ukosoaji, ikiwemo kuhusu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Vijana wengine waliotajwa katika madai hayo ni pamoja na Mdude Nyangali, Kipanya na Chaula, ambao walidaiwa kutekwa katika mazingira yaliyoelezwa kuwa ya kutatanisha, na hadi sasa hatima yao bado haijafahamika wazi.
Kwa upande mwingine, yapo matukio ya vijana waliodaiwa kutekwa na baadaye kuonekana wakiwa na majeraha, akiwemo Abdul Nondo. Hata hivyo, wahusika wa matukio hayo hawakuwahi kubainishwa hadharani.
Ripoti ya Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) ilinukuu jumla ya watu 83 waliodaiwa kutekwa, ambapo asilimia kubwa walitajwa kuwa ni vijana. Katika tamko lake, TLS ilikemea vikali vitendo vya utekaji na utesaji, ikivitaja kuwa ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu kama zinavyolindwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na mikataba ya kimataifa. TLS pia ilitoa wito kwa Serikali kuunda Tume Maalum ya Uchunguzi ili kuchunguza matukio hayo na kuwabaini wahusika.
2. Hofu ya vijana kutoa maoni yao
Athari nyingine iliyobainika ni kuenea kwa hofu miongoni mwa vijana katika kutoa maoni yao ya kisiasa au kijamii. Uchunguzi unaonesha kuwa hali hiyo imechangia kupungua kwa mijadala huru na kuibuka kwa kundi la vijana wanaojikita zaidi katika kusifia mamlaka, hali inayojulikana mitaani kama “uchawa”.
Hofu ya kukumbana na vitisho, unyanyasaji au matatizo ya kisheria imewafanya vijana wengi kushindwa kuwasilisha hoja zao kwa uwazi kwa mamlaka husika, jambo linalodhoofisha msingi wa uwajibikaji katika mfumo wa kidemokrasia.
3. Wimbi la wakimbizi wa kisiasa miongoni mwa vijana
Kutokana na mazingira hayo, baadhi ya vijana hasa wale waliokuwa wakosoaji wa sera au Serikali walilazimika kuondoka nchini na kutafuta hifadhi katika mataifa mengine. Ingawa takwimu rasmi hazipo wazi, simulizi za wahusika na ripoti za wadau wa haki za binadamu zinaonesha kuwepo kwa kundi la vijana waliogeuka wakimbizi wa kisiasa kwa kuhofia usalama wao binafsi.
Hali hii imeathiri sio tu maisha ya vijana hao, bali pia mchango wao katika maendeleo ya Taifa.
4. Kuporomoka kwa imani ya vijana katika mifumo ya kidemokrasia
Athari nyingine, lakini yenye uzito mkubwa, ni kupungua kwa imani ya vijana katika mifumo ya kidemokrasia. Uchunguzi unaonesha kuwa vijana wengi wamepunguza au kuacha kabisa kushiriki katika shughuli za kisiasa kama vile kupiga kura, kuhudhuria mikutano ya kisiasa au kujihusisha na vyama vya siasa.
Hali hii inatajwa kuchangiwa na mtazamo kuwa ushiriki wao hauleti mabadiliko ya kweli, pamoja na hofu ya madhara yanayoweza kujitokeza.
Rai ya Mwandishi
Kwa ujumla, uchunguzi wa miaka 10 ya mwenendo wa kidemokrasia nchini Tanzania unaonesha wazi kuwa vijana wamebeba mzigo mkubwa wa changamoto hizo. Kuanzia madai ya utekaji, hofu ya kutoa maoni, ukimbizi wa kisiasa hadi kupotea kwa imani katika mifumo ya kidemokrasia, hali hii inaacha maswali mazito kuhusu mustakabali wa ushiriki wa vijana katika ujenzi wa Taifa la kidemokrasia.
Bila hatua za makusudi za kurejesha imani, kulinda haki za msingi na kuimarisha taasisi za kidemokrasia, makovu haya yanaweza kuendelea kuathiri kizazi cha sasa na kijacho cha vijana wa Tanzania.