Zanzibar 2020 Uchambuzi: Nafasi ya Profesa Makame Mbarawa kwenye Urais Zanzibar

Zanzibar 2020 Uchambuzi: Nafasi ya Profesa Makame Mbarawa kwenye Urais Zanzibar

aleesha

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
798
Reaction score
1,178
Mengi yamesemwa kuhusu nia ya Profesa Makame Mbarawa kugombea Urais Zanzibar 2020. Wapo waloandika makala zenye uwiano bora, wapo walomponda na kusema hana nafasi lakini pia wapo walomsifia. Makala hii inachambua pande mbili za mjadala na kumpa msomaji ama uwanja mpana wa kuwa na hitimisho lake mwenyewe au kuendelea na tafiti zaidi, kujaribu kuona ipi hasa nafasi ya Profesa Mbarawa katika mbio za Urais Zanzibar 2020.



Profesa Makame Mbarawa
Profesa Makame Mbarawa


Upande wa kwanza ni kutazama yale ambayo Profesa Mbarawa ameyabainisha kwa watu wake wa karibu kuwa sehemu ya vipaumbele vyake iwapo atafanikiwa kuwa Rais wa Zanzibar. Japo mara nyingi wagombea wa CCM hunadi ilani ya chama chao, sote twafahamu kwamba Rais anaweza kuamua kuchomekea na kutekeleza hata yale ambayo si ilani kwa asilimia mia moja alimradi tu yako katika maono yake.

Jambo la kwanza ni kuondoa ubadhirifu katika manunuzi ya umma. Moja ya eneo ambalo amelitaja mara nyingi katika viunga mbalimbali na watu wake wa karibu ni ununuzi kwa gharama kubwa wa meli mpya ya abiria ya MV Mapinduzi II ambayo watafiti wengi wanaonesha si mpya, haijaleta tija Zanzibar na ilinunuliwa kwa gharama isiyo sahihi ikigubikwa na rushwa na ufisadi.



rs=w:1280





Jambo la pili analotajwa kuwa na kiu nalo ni kuona SMZ inatengeneza mazingira ya watu kufanya biashara badala ya yenyewe kujaribu kufanya biashara. Kwenye hili anaelezwa kukerwa na madudu ya SMZ ya ununuzi wa gharama kubwa wa meli mbili za uvuvi, Sehewa 1 na Sehewa 2 ambazo SMZ haikulazimika kununua.



rs=w:1280



Mbarawa anasisitiza kuwa kazi ya SMZ si kuingia kwenye biashara bali kuweka mazingira mazuri ya kisera na sheria kwa sekta binafsi.

Kosa la tatu ambalo Mbarawa anatajwa kuahidi kulisahihisa ni lile la SMZ kuanzisha miradi mikubwa ambayo thamani yake imepita uhalisia na haijakamilika. Mifano ya miradi hiyo maarufu kama miradi zimwi na ya upigaji ni ujenzi wa jengo la abiria Uwanja wa Ndege Zanzibar, miradi ya maji, barabara zisizo na viwango Unguja na Pemba, miradi ya kuweka taa barabarani, mitaro ya maji na ile ya kamera za usalama (CCTV). Mbarawa anaamini miradi hii haikuwa na dira (vision) na usimamizi ipasavyo na imeiletea Zanzibar hasara kubwa.



rs=w:1280



Kosa la nne analotajwa kukusudia kurekebisha ni kuhakikisha hakuna tena matumizi yasio ya msingi ya fedha za ZSSF kujenga miradi mikubwa ambayo uchambuzi wake unaonesha ni hasara kubwa kwa serikali na pesa za wananchi. Mifano ya miradi hiyo ni ujenzi wa nyumba za makaazi Mbweni na Kwahani, ujenzi wa viwanja vya burudani vya Kariakoo na Tibirinzi na ujenzi wa maduka ya kisasa Michenzani na Darajani.



rs=w:1280





Mbarawa anatajwa kuwa muumini wa kuijengea nguvu sekta binafsi na anasisitiza kwamba SMZ ilikosea kujiingiza katika miradi hiyo na badala yake ingeweza kutekelezwa moja kwa moja na sekta binafsi.

Jambo jengine linalotajwa katika mipango yake ya awali ni kupitia upya ubadhirifu mkubwa uliopelekea kupewa mwekezaji asie na uwezo kujenga Hoteli ya Bwawani.



rs=w:1280



Hoteli hiyo hivi sasa imekuwa magofu. Pia anatajwa kuweka bayana kwamba panapo majaliwa akapata ridhaa lazima kutazama sababu za kutokamilika ujenzi wa gati ya kisasa ya Mpigaduri.



Eneo la ujenzi wa gati ya kisasa ya Mpigaduri
Eneo la ujenzi wa gati ya kisasa ya Mpigaduri


Kabla ya hitimisho, tutazame upande wa pili wa mambo ambayo tunaweza kuyaita vikwazo. Hivi lazima Profesa Mbarawa kuviruka ili kufikia ndoto yake ya kuteuliwa na CCM kupeperusha bendera yake kwenye uchaguzi wa Rais Zanzibar 2020.

Kikwazo cha kwanza kinatajwa ni kutokubalika vya kutosha Pemba ambako ni kwao. Tafiti zinaonyesha hata kabla ya zoezi la kuchukua fomu, kutafuta wadhamini na kuzirudisha halijaanza tayari kuna dalili kwamba Profesa Mbarawa ameanza kuwa na wakati mgumu kupata wadhamini kwao Pemba. Ili aweze kufanikiwa ni lazima atengeneze mazingira kwanza ya kukubalika na watu wa kwao.

Pili, inasemekana kwamba Profesa Mbarawa hajakwenda kumuona Rais wa Zanzibar Dk Shein muda mrefu. Hii inaleta ukakasi katika kuungwa kwake mkono. Katika siasa Rais aliye madarakani hasa kama anatoka chama chako ni mtu mwenye nguvu sana kwenye hatma yako. Kwakuwa muda bado kiasi tutegemee kumuona Profesa Mbarawa akijaribu kusahihisha hili kwa kwenda kumuona Rais na kwa namna fulani kuomba kuungwa mkono.

Jambo la tatu ambalo lazima kiunzi chake akiruke ni tuhuma za kuwa na mke Rai wa Uganda. Wazanzibari na hakika Watanzania ni watu wanaokumbatia sana utaifa na japo wanaweza kujinadi kwamba wanaheshimu na kujali watu wote, ni watu tofauti sana wanapoona mtu anayetaka ridhaa ya kuwaongoza ana mke mgeni. Bado ni ngumu kufahamu mbinu gani itatumika kupindua mjadala wa jambo hilo lakini ni jambo ambalo huenda likawa na mjadala mkubwa katika maamuzi ya CCM kwani lina athari kwenye sanduku la kura.

Taarifa za ugomvi wake na Bi Saada Mkuya nazo huenda zikaibuka na lazima kupatiwa maelezo. Inaelezwa kwamba katika utawala wa awamu ya nne Mbarawa akiwa Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia aligombana na Bi Saada kutokana na kile kilochotajwa Mbarawa kutoijali Zanzibar na kwa kuipa kipaumbele kwenye miradi. Hii inaweza kutumika kama taarifa ya kuhoji mapenzi yake kwa Zanzibar na huenda ikamtesa katika uchaguzi.

Jambo jengine linaloweza kuwa kiunzi kwake na lazima kutafutiwa maelezo mapema ni kiwango cha mali zake ambazo kazipata katika kipindi kifupi cha utumishi wake serikalini. Mali mbalimbali zimeanza kutajwa kama shamba kubwa la mikarafuu analomiliki Pemba, nyumba ya ghorofa Mbweni jijini Dar es Salaam na kadhalika.

Viunzi hivyo vyaweza kuchukuliwa kama vita ya kisiasa ya wapinzani wake kuibua mapungufu yake lakini ni mambo muhimu ambayo lazima ajiandae vyema kuyaondoa njiani. Iwapo atafanikiwa na malengo yake juu ya Zanzibar yakaeleweka na wengi basi anaweza kuwa na nuru kwenye nia yake, kinyume na hapo nafasi yake kwenye mbio za Urais 2020 itazidi kudidimia.
 
Waachiwe Wananchi waamue chini ya Tume Huru vinginevyo yeye na wengne wataowekwa na Mafia ya CCM ndio wale wale hawana jipya zaidi ya kumtumikia Mvamizi wa Dodoma
 
Hiyo hoja ya pili haina mashiko hatumchagui Mtu/Rais kwa kigezo cha Ukabila, Dini, rangi wala Mkoa au Wilaya anayotoka bali tunazingatia Sifa, weledi na umahiri wa kuongoza Nchi hata kama wakitoka Pemba mara 10 lakini wana sifa zote watachaguliwa kuwa Rais tu!
 
Hiyo hoja ya pili haina mashiko hatumchagui Mtu/Rais kwa kigezo cha Ukabila, Dini, rangi wala Mkoa au Wilaya anayotoka bali tunazingatia Sifa, weledi na umahiri wa kuongoza Nchi hata kama wakitoka Pemba mara 10 lakini wana sifa zote watachaguliwa kuwa Rais tu!

Maneno jumba ya maneno , Vitendo vinasema zaidi ya maneno
 
Good analysis.

Hili la kuwa na mke foreigner hakina mashiko kwa dunia ya leo hapo duru za kijasusi zinatahadharisha first family kuwa na uzalendo zaidi.

Lakini wapi viongozi wengi wameoa jamii ya kutoka Rwanda na wanajinasibu Kama wazalendo kupitiliza mbele ya vipaza sauti
 
Good analysis.

Hili la kuwa na mke foreigner hakina mashiko kwa dunia ya leo hapo duru za kijasusi zinatahadharisha first family kuwa na uzalendo zaidi.

Lakini wapi viongozi wengi wameoa jamii ya kutoka Rwanda na wanajinasibu Kama wazalendo kupitiliza mbele ya vipaza sauti
Mbona Salimin Amour alio Mtu wa Bara na sio wa Visiwani au alio wa Bara ili awapendele wabara na Muungano.

Na kama kuo mganda ni kikwazo basi atakuja kuo kwenye ukoo wenu wakati ukifika wa kupitishwa aliyeteuliwa
 
Prof huyu ambaye wizara yake kote alipopita kunaufisadi mwingi tu umefanyika leo akauondea huko zenji.

Aache utani,labda aseme kwa nini alishindwa huku na huko ataweza.
 
Kwenye vikwazo kuna mambo muhimu hujayataja.

Kwanza profesa hana mizizi Ya kisiasa Zanzibar na iangaliwe kikwazo cha kukosa suppoti ya wahafidhina...
La wahafidhina sioni kuwa ni kikwazo. Wao siku zote wanataka kiogozi uwe mkatili. Kuongoza ni kuonesha njia kwa kutumia hekima, na hili sioni kama ni kiwazo. Kuwa Mpemba na Rais anayeondoka ni Mpemba halina uzito.

Ikumbukwe kuwa hii inayomaliza ni awamu ya saba. Awamu zote sita kulikuwa na Waunguja. Wahafidhina walikuwa wapi wakati huo mpaka wakashindwa kuliona?

Suala la kuonekana mwenye baraka zote kutoka Bara: Hata Rais anayeondoka alionekana hivyohivyo. Kwangu naona tunapaswa kuangalia atafanya nini akiingia madarakani.
 
Hilo la Serikali kufanya "Biashara" yeye akiwa waziri wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amelisimamiaje? Maana mwelekeo wa Serikali ambaye naye Waziri ni Taasisi za Serikali kufanya biashara mfano TPDC, Karandasi kupewa kampuni za Serikali n.k
 
Hawakutokea wilaya moja kwa kufuatana
La wahafidhina sioni kuwa ni kikwazo. Wao siku zote wanataka kiogozi uwe mkatili. Kuongoza ni kuonesha njia kwa kutumia hekima, na hili sioni kama ni kiwazo. Kuwa Mpemba na Rais anayeondoka ni Mpemba halina uzito.

Ikumbukwe kuwa hii inayomaliza ni awamu ya saba. Awamu zote sita kulikuwa na Waunguja. Wahafidhina walikuwa wapi wakati huo mpaka wakashindwa kuliona?

Suala la kuonekana mwenye baraka zote kutoka Bara: Hata Rais anayeondoka alionekana hivyohivyo. Kwangu naona tunapaswa kuangalia atafanya nini akiingia madarakani.

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Mbarawa ni mtu practical mwenye uwezo wa kuanzisha jambo na kulifuatilia mpaka ukamilifu wake ukaonekana.

Ni mtu mwenye uwezo kikazi, utekelezaji wa miradi mingi ya maji ndani ya muda mfupi ni kielelezo cha uwezo wake.
 
Hawakutokea wilaya moja kwa kufuatana

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
Mkuu umesahau. Uzee NI tatizo na kuishiwa kumbukukumbu. Kama ni kijana hujui hata historia. Karume Senior alitokea wilaya ya Mjini. Jumbe wa awamu ya pili alitokea wilaya ya Mjini.

Mwinyi wa awamu ya tatu alitokea wilaya ya Mjini. Wakil aesmu ya nne alitokea Kusini Unguja, Salmin awamu ya tano Kuskazini A, Karume junior awamu ya sita alitokea Mjini na Sheni Mkoani Pemba.
 
Back
Top Bottom