Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
huenda zikaibuka na lazima kupatiwa maelezo. Inaelezwa kwamba katika utawala wa awamu ya nne Mbarawa akiwa Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia aligombana na Bi Saada kutokana na kile kilochotajwa Mbarawa kutoijali Zanzibar na kwa kuipa kipaumbele kwenye miradi. Hii inaweza kutumika kama taarifa ya kuhoji mapenzi yake kwa Zanzibar na huenda ikamtesa katika uchaguzi.
Kikwazo cha kwanza kinatajwa ni kutokubalika vya kutosha Pemba ambako ni kwao. Tafiti zinaonyesha hata kabla ya zoezi la kuchukua fomu, kutafuta wadhamini na kuzirudisha halijaanza tayari kuna dalili kwamba Profesa Mbarawa ameanza kuwa na wakati mgumu kupata wadhamini kwao Pemba. Ili aweze kufanikiwa ni lazima atengeneze mazingira kwanza ya kukubalika na watu wa kwao.
Jambo la tatu ambalo lazima kiunzi chake akiruke ni tuhuma za kuwa na mke Rai wa Uganda. Wazanzibari na hakika Watanzania ni watu wanaokumbatia sana utaifa na japo wanaweza kujinadi kwamba wanaheshimu na kujali watu wote, ni watu tofauti sana wanapoona mtu anayetaka ridhaa ya kuwaongoza ana mke mgeni. Bado ni ngumu kufahamu mbinu gani itatumika kupindua mjadala wa jambo hilo lakini ni jambo ambalo huenda likawa na mjadala mkubwa katika maamuzi ya
Hoja yako ya pili ndio hoja kuu kwa wahafidhina wa unguja.Kwenye vikwazo kuna mambo muhimu hujayataja.
Kwanza profesa hana mizizi Ya kisiasa Zanzibar na iangaliwe kikwazo cha kukosa suppoti ya wahafidhina...
Wewe ndio unasema hivyo ila kwa siasa za Visiwani hii ndio hoja kuu hasa kwa wahafidhina wa Unguja.Hiyo hoja ya pili haina mashiko hatumchagui Mtu/Rais kwa kigezo cha Ukabila, Dini, rangi wala Mkoa au Wilaya anayotoka bali tunazingatia Sifa, weledi na umahiri wa kuongoza Nchi hata kama wakitoka Pemba mara 10 lakini wana sifa zote watachaguliwa kuwa Rais tu!
TulimuandaaHoja yako ya pili ndio hoja kuu kwa wahafidhina wa unguja.
Prof Mbarawa ni mchapakazi mzuri ila asubiri kidogo mwaka huu tunampa tuliyemuandaa muda mrefu Dr. Hussein Mwinyi.
Prof yeye tutampa u makamu wa pili wa rais SMZ
Kwa ufahamu wangu. Karume Senior tulifundishwa kwao Mwera. Mwera so MJINI ni Maghrib .Mkuu umesahau. Uzee NI tatizo na kuishiwa kumbukukumbu. Kama ni kijana hujui hata historia. Karume Senior alitokea wilaya ya Mjini. Jumbe wa awamu ya pili alitokea wilaya ya Mjini.
Mwinyi wa awamu ya tatu alitokea wilaya ya Mjini. Wakil aesmu ya nne alitokea Kusini Unguja, Salmin awamu ya tano Kuskazini A, Karume junior awamu ya sita alitokea Mjini na Sheni Mkoani Pemba.