Uchambuzi: TRUMP na suala la Marekani kutumbua jinsia mbili, Wamefikaje huko?

incognitoTz

Senior Member
Joined
Apr 19, 2019
Posts
133
Reaction score
172
Misuguano ya hivi karibuni juu ya masula ya jinsia ilianza baada ya yanyongeza katika "Title IX" iliyoathiri Marekebisho ya sheria ya Elimu ya 1972 (Education Amendments of 1972)

Nyongeza ya Title IX, Inasema:

"Hakuna mtu nchini Marekani, kwa misingi ya jinsia, atatengwa kwa kushiriki, kunyimwa manufaa ya, au kubaguliwa chini ya mpango wowote wa elimu au shughuli inayopokea usaidizi wa kifedha wa Nchi."

Chini ya uongozi wa Biden, Title IX, ambayo ni sheria ya haki za raia wa Marekani, ilipanuliwa kujumuisha wanafunzi wa transgender. Hii ilimaanisha wanafunzi wa transgender walipewa haki ya kutumia vyoo vya kike au kiume na kushiriki michezo kulingana na wao wanavyo jitambulisha kijinsia na si tu kwa jinsia walizopewa wakati wa kuzaliwa.
kjkwbn2h.png

Hii ilisukumwa na kilichodaiwa kuwa kuzifanya shule ziwe na mazingira rafiki na ya usawa zaidi ili kupunguza ubaguzi wa kijinsia.

Jambo lililopokelewa tofauti na wakosoaji wa mlengo wa kuria, wakidai nyongeza hiyo ya Title IX inaweza kuharibu faragha na haki katika michezo, hasa michezo ya wanawake.

Kumbuka nyongeza ya Title IX iliwezasha mtu aliyezaliwa na mauongo ya kiume kuingia kwenye vyoo vya wanawake kama ataamua kujitambulisha kama mwanamke.

Trump anamtazamo gani kuhusu Masuala ya Jinsia?
Kuchaguliwa tena kwa Trump kumekuja na mabadiliko makubwa hususani sera zinazoshughulikia jinsia, kwani Trump anakusudia:

Kutambua jinsia mbili tu za kimwili: Hii itaondoa ulinzi wa sheria kwa watu wa transgender na wasio na jinsia kati ya hizo mbili, na itaenda kuakiathiri jinsi shule na michezo itakavyotambua jinsia.

Kuondoa huduma za kusaidia watoto wanao jitambaluisha kwa jinsia tofauti na zile za kuzaliwa nazo. Trump anapanga kuachana na ufadhili matibabu, kama vile matibabu ya kisaikolojia au ya homoni, kwa wanufaika wa kundi hilo la transgender.

Soma Pia: Donald Trump: Kuanzia sasa Serikali ya Marekani itatambua jinsia mbili pekee, Mwanaume na Mwanamke

Kukomesha ushiriki wa wanawake wa transgender katika michezo ya kike: Hii inamaanisha wanawake wa transgender hawatashiriki michezo ya wanawake, hawaturuhusiwa kutumia sehemu za kuhifadhi vifaa vya michezo wala vyoo vya kike.

Maamuzi haya yanaweza kuibua misuguano gani kwa Jamii ya Marekani?
Kwa jamii ya LGBTQ+: Bila ya shaka Sera hizi zitawafanya watu wa kundi hilo kuhisi kutotambulika na kuona wanafanyiwa ubaguzi zaidi. Suala linaloweza kupelekea matukio ya machafuko na maandamano ya makundi mbali mbali yanayopinga msimamo huo wa Trump. Makundi ya LGBTQ+ yana historia ndefu katika ya kutumia mbinu za ghasi kushinikiza jamii kukubali sera zenye manufaa kwao na mbinu hizi hazikuanzia kipindi cha Maandamano ya Stonewall, zilikuwepo kabla.

Stonewall-and-Five-Historical-LGBT-Events-That-You-Should-Know-About-1024x683.jpg

Kwa upande wa sekta ya Elimu, Shule zitahitaji kuzirudia sera za zamani za jinsia, inaweza kugeuza michezo na utaratibu wa shule, na hivyo kuleta mzozo wa kisheria na kijamii katika mchakato huo wa mabadiliko

Kwa wanamichezo wa Kike: Katika michezo ya wanawake wapo watakaona hii wametendewa haki kwani haikuwa rahisi kwa Mwanamke aliezaliwa mwanamke kupanda ulingoni na kurushiana makonde na dhidi ya aliyezaliwa mwanaume lakini anajitambulisha kama mwanamke. Hata hivyo kuna kundi watalipokea suala hili kwa hisia tofauti na kuona ni jitahada za kibaguzi dhidi ya wanawake wa transgender.

Kiujumla, Sera hizi lazima zitaigawa jamii kwani tayali zinamgongano wa maslahi, kati ya wale wanaopenda mila na wale wanaotaka usawa kwa kila mtu.
Kitaifa: Mabadiliko haya yanamaanisha msimamo huu kihafidhina (Conservatism)
utaenda mbali zaidi na unaweza kuathiri masuala mengine kama afya, kazi, na hata kuhudumu katika jeshi.

Kiufupi, Trump anapanga kurudisha nyuma sera za jinsia za Biden, kitu kitakachopelekea mjadala mkubwa kuhusu usawa na haki za watu wa transgender. Suala la mgawanyiko, ghasia na kuongezeka kwa migogoro ya kisheria halitahepukika katika jamii ya Marekani.
Hatahivyo sio rahisi kutokea shinikizo lolote litakalo weza kumtungisha Trump katika msimamo huu, kwani huu ni mhula wake wa Mwisho na hana la kupoteza wala hitaji la kuungwa mkono na kundi lolote kwasasa, hali hii inaweza kudokeza juu ya nguvu na namna atakavyodhibiti makundi yatakayo pinga msimamo wake kwa njia ya vurugu.
 
Misuguano ya hivi karibuni juu ya masula ya jinsia ilianza baada ya yanyongeza katika "Title IX" iliyoathiri Marekebisho ya sheria ya Elimu ya 1972 (Education Amendments of 1972)

Nyongeza ya Title IX, Inasema:

"Hakuna mtu nchini Marekani, kwa misingi ya jinsia, atatengwa kwa kushiriki, kunyimwa manufaa ya, au kubaguliwa chini ya mpango wowote wa elimu au shughuli inayopokea usaidizi wa kifedha wa Nchi."

Chini ya uongozi wa Biden, Title IX, ambayo ni sheria ya haki za raia wa Marekani, ilipanuliwa kujumuisha wanafunzi wa transgender. Hii ilimaanisha wanafunzi wa transgender walipewa haki ya kutumia vyoo vya kike au kiume na kushiriki michezo kulingana na wao wanavyo jitambulisha kijinsia na si tu kwa jinsia walizopewa wakati wa kuzaliwa.
View attachment 3208017

Hii ilisukumwa na kilichodaiwa kuwa kuzifanya shule ziwe na mazingira rafiki na ya usawa zaidi ili kupunguza ubaguzi wa kijinsia.

Jambo lililopokelewa tofauti na wakosoaji wa mlengo wa kuria, wakidai nyongeza hiyo ya Title IX inaweza kuharibu faragha na haki katika michezo, hasa michezo ya wanawake.

Kumbuka nyongeza ya Title IX iliwezasha mtu aliyezaliwa na mauongo ya kiume kuingia kwenye vyoo vya wanawake kama ataamua kujitambulisha kama mwanamke.

Trump anamtazamo gani kuhusu Masuala ya Jinsia?
Kuchaguliwa tena kwa Trump kumekuja na mabadiliko makubwa hususani sera zinazoshughulikia jinsia, kwani Trump anakusudia:

Kutambua jinsia mbili tu za kimwili: Hii itaondoa ulinzi wa sheria kwa watu wa transgender na wasio na jinsia kati ya hizo mbili, na itaenda kuakiathiri jinsi shule na michezo itakavyotambua jinsia.

Kuondoa huduma za kusaidia watoto wanao jitambaluisha kwa jinsia tofauti na zile za kuzaliwa nazo. Trump anapanga kuachana na ufadhili matibabu, kama vile matibabu ya kisaikolojia au ya homoni, kwa wanufaika wa kundi hilo la transgender.

Soma Pia: Donald Trump: Kuanzia sasa Serikali ya Marekani itatambua jinsia mbili pekee, Mwanaume na Mwanamke

Kukomesha ushiriki wa wanawake wa transgender katika michezo ya kike: Hii inamaanisha wanawake wa transgender hawatashiriki michezo ya wanawake, hawaturuhusiwa kutumia sehemu za kuhifadhi vifaa vya michezo wala vyoo vya kike.

Maamuzi haya yanaweza kuibua misuguano gani kwa Jamii ya Marekani?
Kwa jamii ya LGBTQ+: Bila ya shaka Sera hizi zitawafanya watu wa kundi hilo kuhisi kutotambulika na kuona wanafanyiwa ubaguzi zaidi. Suala linaloweza kupelekea matukio ya machafuko na maandamano ya makundi mbali mbali yanayopinga msimamo huo wa Trump. Makundi ya LGBTQ+ yana historia ndefu katika ya kutumia mbinu za ghasi kushinikiza jamii kukubali sera zenye manufaa kwao na mbinu hizi hazikuanzia kipindi cha Maandamano ya Stonewall, zilikuwepo kabla.

View attachment 3207955

Kwa upande wa sekta ya Elimu, Shule zitahitaji kuzirudia sera za zamani za jinsia, inaweza kugeuza michezo na utaratibu wa shule, na hivyo kuleta mzozo wa kisheria na kijamii katika mchakato huo wa mabadiliko

Kwa wanamichezo wa Kike: Katika michezo ya wanawake wapo watakaona hii wametendewa haki kwani haikuwa rahisi kwa Mwanamke aliezaliwa mwanamke kupanda ulingoni na kurushiana makonde na dhidi ya aliyezaliwa mwanaume lakini anajitambulisha kama mwanamke. Hata hivyo kuna kundi watalipokea suala hili kwa hisia tofauti na kuona ni jitahada za kibaguzi dhidi ya wanawake wa transgender.

Kiujumla, Sera hizi lazima zitaigawa jamii kwani tayali zinamgongano wa maslahi, kati ya wale wanaopenda mila na wale wanaotaka usawa kwa kila mtu.
Kitaifa: Mabadiliko haya yanamaanisha msimamo huu kihafidhina (Conservatism)
utaenda mbali zaidi na unaweza kuathiri masuala mengine kama afya, kazi, na hata kuhudumu katika jeshi.

Kiufupi, Trump anapanga kurudisha nyuma sera za jinsia za Biden, kitu kitakachopelekea mjadala mkubwa kuhusu usawa na haki za watu wa transgender. Suala la mgawanyiko, ghasia na kuongezeka kwa migogoro ya kisheria halitahepukika katika jamii ya Marekani.
Hatahivyo sio rahisi kutokea shinikizo lolote litakalo weza kumtungisha Trump katika msimamo huu, kwani huu ni mhula wake wa Mwisho na hana la kupoteza wala hitaji la kuungwa mkono na kundi lolote kwasasa, hali hii inaweza kudokeza juu ya nguvu na namna atakavyodhibiti makundi yatakayo pinga msimamo wake kwa njia ya vurugu.
Machoko chali, on this matter Tramp is doing great.
 
Back
Top Bottom