TANZANIA YA MAGUFULI
Hii ndiyo Tanzania mpya ya Dr. John Magufuli
1. Vijiji vyote Tanzania vitakuwa na umeme wa uhakika, Rural Energy Argency (REA) imeshaanza kazi hiyo.-Mijini tu hautoshi kila siku mgao,Pia huu ni mpango wa serikali na unachangiwa na wanachi wenyewe any one can
1. Vijiji vyote Tanzania vitakuwa na umeme wa uhakika, Rural Energy Argency (REA) imeshaanza kazi hiyo.-Mijini tu hautoshi kila siku mgao,Pia huu ni mpango wa serikali na unachangiwa na wanachi wenyewe any one can do
2. Wanawake na vijana watapata mikopo kupitia vikundi vyao. Milioni 50 zitatengwa kufanikisha mikopo hiyo inatolewa ili kupunguza umasikini katika ngazi ya familia-Hii ni pointless,somesha watoto wao,wape watoto wao elimu bora,si kuwarubuni na kufanya umachinga kwa kuuza bidhaa ya kichina.
3. Madereva wote watakuwa na mikataba ya ajira. madereva jiandaeni kusaini mikataba nikiingia ikulu-hapa unataka kusolve nini,kukosa mkataba au kuboresha kipato cha Dereva?Kumbe dereva wa dala dala yangu ataanza kulipwa na serikali?au una maanisha magari yote yatamilikiwa na serikali? Nijuavyo mimi mkataba wa ajira ni kati ya mwajiri na wajiriwa
4. Wanyonge wote watathaminiwa mf: wamachinga na mama nitilie. serikali yangu ya awamu ya tano haitowaonea wanyonge-Du!kumbe leo watu wanaonewa na hakuna kufuata sheria?basi aanze kwa kuwarudishia nyumba zao wale aliowabomolea maana ina onekana sheria hazikufuatwa na watangulizi wake
5. Watumishi wa serikali watapata nyumba za kuishi karibu na vituo vyao vya kazi. Nikiapishwa watendaji wote wa serikali wajiandae kuishi kwenye vituo vyao vya kazi, sivyo waache kazi.Naamini hizi nyumba zitashuka kutoka mbinguni, maana zilizokuwepo zimeshauzwa na Magufuli aliziuza kwa mkono wake mwenyewe
6. Kila kijiji kitakuwa na zahanati, kila kata itakuwa na kituo cha afya, kila wilaya itakuwa na hospitali ya wilaya na kila mkoa utakuwa na hospitali ya rufaa-Kwa maana ya majengo au? otherwise unadanganya
7. Shule zitajaa walimu wa sayansi-Hawa walimu kama hawatashuka toka mbinguni,basi tutawatoa nje,maana kumuuanda mtu mpaka awe mwalimu na shule zijae si kazi ya miaka mitano,unless uniambie kuwa mpaka leo wapo mitaani ila serikali ya ccm imeshindwa kuwapa kazi
8. Miundombinu ya barabara itaimarishwa zaidi na barabara zitapitika majira yote ya mwaka-Du
9. Wafanyakazi wazembe wote watawajibishwa
CHAGUA MAGUFULI MWANA MABADILIKO YA KWELI