Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii ya 20152020, Chama Cha
Mapinduzi kitaielekeza Serikali kuweka nguvu kubwa katika kukamilisha
utekelezaji wa Sera ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda Awamu ya Tatu
(20102020) ambayo malengo yake ni kuiwezesha Sekta ya Viwanda
kuchangia katika kufikia malengo ya maendeleo ya muda mrefu kama
ilivyoanishwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025. Aidha, Utekelezaji
wa Ilani hii utakuwa ni sehemu ya Utekelezaji wa Mpango wa Pili wa
Maendeleo wa Miaka Mitano (2015/16-2020/21) ambao lengo lake ni
kuendeleza uchumi wa viwanda.
Katika kipindi hicho, utaanza ujenzi wa viwanda mama (basic industries)
na kuimarisha viwanda vilivyopo lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba:-
(a) Mchango wa Sekta ya Viwanda katika Pato la Taifa unaongezeka kutoka
asilimia 9.9 mwaka 2013 hadi asilimia 15 ifikapo mwaka 2020;
(b) Sekta ya Viwanda inaongeza ajira kufikia asilimia 40 ya ajira zote ifikapo 2020
kwa kuweka kipaumbele cha kujenga viwanda vinavyotumia malighafi
zinazozalishwa hapa nchini kama vile kilimo, mifugo, uvuvi na maliasili;
Viwanda hivyo ni pamoja na viwanda vya nguo, sabuni, korosho, matunda n.k.
(c) Kuandaa mikakati thabiti ya kuhamasisha sekta binafsi kuanzisha viwanda
vikubwa na vya kati na kuweka utaratibu wa kuvilinda dhidi ya viwanda vya
nje;
(d) Kujenga mazingira rafiki yatakayowezesha kupunguza gharama za uwekezaji
na uendeshaji wa viwanda;
26
(e) Kuanzisha viwanda vya msingi vinavyotumia malighafi ya chuma katika maeneo
ya Liganga na Mchuchuma;
(f) Sekta ya Viwanda inaongeza fursa za masoko hususan yenye upendeleo wa
ushuru wa forodha kama Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jumuiya ya Maendeleo
ya Kusini mwa Afrika, Utatu wa COMESA-EAC-SADC na Umoja wa Ulaya, nchi
rafiki kama India, China, Japan na Marekani; na
(g) Kuendeleza kasi ya ujenzi wa viwanda vidogo na vya kati hasa vinavyosindika
mazao.
(h) Kuhakikisha Benki ya Rasilimali (TIB) inapanua wigo wa Dirisha Maalumu ili liweze kutoa huduma zake kwenye maeneo yote nchini ikiwemo Tanzania
Zanzibar.
​