KING MIDAS
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 8,589
- 16,936
UCHAMBUZI WA KISHIRIKINA KUFUNGWA KWA SIMBA.
Na Yericko Nyerere
Hadi Siku 6 kabla mechi Simba ilikuwa imeushika mchezo vizuri nje ya Uwanja. Kuanzia Kaskazini, Kusini, Mashariki na Magharibi. Makafara makubwa yalikuwa yamefanyika ipasavyo, na Tulikuwa tumeulinda Uwanja mwanzo mwisho.
Hadi inafika siku moja kabla ya mchezo @simbasctanzania
ilikuwa inaongoza 2-0 kwenye ungo wa Mizimu. Ushindi huu wa Simba wa bao 2 siku moja kabla ya game ulikuja baada ya Kamati za Simba kunasa na kuharibu vikosi vya Wachawi wa Yanga vilivyokuwa vimeenda Ngende, Sumbawanga, Kigoma na Zanzibar.
Kukamatwa kwa kamati hizo kuliihakikishia Simba Ushindi, izingatiwe kwamba kwa Wiki nzima Uwanja wa Mkapa ulikuwa umehamishwa na huku pale Taifa pakilindwa kwa nguvu kubwa. Makafala makubwa yalipigwa njia zote atakazopita Yanga kuanzia akitokea Avic Town hadi kufika Uwanja wa Taifa.
Ilipofika saa moja kabla ya mchezo kuanza, ungo ulisoma matokeo 2-1, hali hii ilifanya tuanze uchambuzi kujua yanga wamepataje bao hilo moja ilihali ilikuwa 2 bila. Na hata mpira ulipoanza Yanga wakapata bao, na kisha Simba kusawazisha, Ungo uliendelea kuonyesha matokeo yatakuwa 2-1. Kufumba na kufumbua baada ya mapumziko tu, Hali ilibadilika.
Uchanbuzi wa Kishirikina umekuja kubaini Walituzidi ujanja, Kwanza baada ya kuzikamata zile kamati za uchawi zilizotumwa Ngende, Sumbawanga na Zanzibar, Wenzetu walibadili mbinu haraka wakaenda Mwandoya kwa Mwana Kingi, walibadili mbinu siku moja kabla ya mchezo, muda wa kwenda uwanjani wakakwepa njia zote tulizotega kuanzia Avic Town, wakati wa kutoka kambini kuja uwanjani walipita Mwasonga, Kibada, Kongowe na kutokea Mbagala (kimizimu japo wengi waliona timubimepita Darajani Kigamboni) tofauti na ilivyozoeleka.
Vita vilikuwa vikubwa Uwanjani, Mwanakingi alifanikiwa kuua njia zote za Kamati ya Simba na ilipofika mapumziko alikuwa amefaulu kupora uwanja na kugeuza kibra na kutuingiza kwenye mfumo. Na hivyo ni wazi pekee Wachawi wa Simba tulizidiwa, Yanga walifanikiwa