Uchambuzi wa kitabu cha Rais Mstaafu Benjamin Mkapa "MY LIFE, MY PURPOSE"

Mh. Mkapa keshasema hakuwa nchini wakati haya mauaji yalivyotokea na aliyekuwa anakaimu Mungu kesha mpunzisha katika pumziko la amani milele.
Mmh kuwa nje ya nchi haiwezi kuwa sababu ya kutokuhusika.

Hawa viongozi wana siri nzito sana ndani ya mioyo yao.
 
Msichokijuwa kuhusu unafiki wa hawa viongozi wetu. mara baada ya mauaji yale Kuliofanywa muafaka wa Pili Zanzibar kama sikosei. Hali ya nchi ilikuwa tete na Yeye Mkapa alihusika kwenye Muafaka huu ambao nao ulikuwa wa kitapeli tu. Nakumbuka siku zile Profesa Lipumba akiwa Mwenyekiti wa CUF alimwambia Live pale Ikulu Zanzibar Kwamba Viongozi waache unafiki wa kuharibu Demokrasia. Kilichotokea 2005 Zanzibar ni mwendelezo ule ule. Na Mkapa alikuwa rais bado.

Nnachotaka kusema alichokifanya Mkapa ni kutafuta huruma ya jamii leo na wala haitoki moyoni. Kama ni kujuta au kufadhaishwa asingeruhusu 2005 kutokea tena hujuma ambazo zingesababisha chuki na Umwagaji damu kama si busara za Wapinzani.

CCM ni wale wale.

Jemedari wa Uzalendo wa Tanzania kwa sasa ni TUME YA WARIOBA TU.
 
Dunia yaleo uchumi kwanza hizo mambo za kujitoa ilikuwa zama za ujamaa,hakuna MTU yuko tayari kuteseka na familia take kiss kujitoa huku wengine wakijilimbikizia mihela... Leo professa anaona fahari kuacha profession take nakukimbilia siasa,walimu wengi hivyohivyo. Hatuwezi kubaki na nadharia za kijinga walimu wanapaswa kulipwa vizuri ili watuelimishie watoto wetu kwa viwango vya juu. Hivi hushangai kijana anamaliza std seven shule za serikali hajui KKK!!! Mabadiliko ni muhimu mmmno kama kweli tunataka kuendelea na kumkomboa mnyonge
 
kama prof analipwa milion 4min na bado anatamani siasa,mwalimu wa shule ya msingi anatakiwa alipwe milioni ngapi ili ajikite kwenye wito wake??

kuna kazi pamoja na ukuaji wa tech na maendeleo bado zitabakia kuwa ni wito kwa asili yake,kama wewe ni dactari au mwalimu,kwa kutolipwa stahiki zako unageukia kugoma ili umkomoe mgonjwa au mwanafunzi.hutoshi ulipo.tusisingizie zamani.
 
Ningesoma uchambuzi huu kama Mwandishi wa hicho kitabu asingetukana watanzania wengine wenye mtazamo tofauti na yeye! Kuita watu "malofa" kisa tu wanaeleza hisia zao ni sababu tosha ya kumwona "FARA" tu na sioni sababu ya kupoteza hela yangu niliyoipata kwa jasho halali kununua mawazo ya lofa mkubwa!
 
Sijasoma,ila kama kuna sehemu kakumbushia MALOFA basi itakua kagusia yote
 
"Tatu, anazungumzia kukosekana kwa itikadi na fikra pevu za kina juu ya mustakabali wa Taifa letu. Inabainishwa kuwa tunahitaji ukombozi wa pili, Kisiasa, Kiuchumi, Kiutamaduni. Tunahitaji kama Taifa, na mtu mmoja mmoja kuona aibu kuwa ombaomba".............

Jamani ukawa si waliyasema haya........akasema Tanzania ilishakombolewa 1961.......
Na anayetaka ukombozi wa pili Kama Ni mwanaume abebe Mimba????? Au sio yeye?????
Ni vigumu Sana kuilewa akili ya mwafrika.
 
Kimenikumbusha kitabu cha John Kiriamiti
MY LIFE IN CRIME
Kitabu cha jambazi, lakini kimeandikwa vizuri sana.

Ni moja kati ya vitabu ambavyo siwezi kuvisahau. Hususan kwa sababu nilikisoma nikiwa mdogo sana.
 
Profesa aliandika huu uchambuzi kwa kutumia simu huku akifukuzwa ama vipi?

Mbona muandiko kuna sehemu umekaa kiajabuajabu?
 
Bado hakijapatikana kitabu kama cha raisi wa Singapoor, Malaysia China na Urusi hao maraisi kiukweli wametransform uchumi na teknolojia ya hizo nchi na vinaonekana wazi, sisi tunwapenda tu viongozi wetu ila kwamba waneyafanya ya kushangaza dunia bado,labda mbeleni au tumsubiri magu amalize huenda tukaingia ktk historia.
ZI JIN PING NI Geneus of economic and tech. transoformation huyu jamaa atabaki kwenye vitabu karne nyingi sana huko mbeleni.
 
Kitabu cha jambazi, lakini kimeandikwa vizuri sana.

Ni moja kati ya vitabu ambavyo siwezi kuvisahau. Hususan kwa sababu nilikisoma nikiwa mdogo sana.
Unamaana gqani,huyu naye ni jambazi?
 
Approach lazima iwe ya haki maana hayo mashamba hawajayaiba bali wanayamiliki kihalali kabisa. Yanavorudishwa yarudishwe kwa haki na pia umakini unahitajika, mashamba yakurudishwa yawe ni yale ambayo hayajaendelezwa.
 
Approach lazima iwe ya haki maana hayo mashamba hawajayaiba bali wanayamiliki kihalali kabisa. Yanavorudishwa yarudishwe kwa haki na pia umakini unahitajika, mashamba yakurudishwa yawe ni yale ambayo hayajaendelezwa.
Nani aliewapa?
 
Dibaji imejaa hekima,maarfa na busara

Sijawahi kusikia Kiongozi wa upinzani ameandika kitabu

Napenda siku moja nisome kitabu cha Mbowe na maalim seif maana huwa tunaambiwa ni askari kanzu
Umesoma vitabu vingapi vya viongozi hadi sasa? And do you think vitabu vya akina Maalim Seif, Mbowe au Lissu na ukweli watakaosema vitaruhusiwa kuuzwa madukani? Tshirt tu za kumwombea Lissu mnaziogopa, sembuse kitabu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…