ENANTIOMER
JF-Expert Member
- Sep 22, 2014
- 1,419
- 804
kama mwalimu mzoefu wa somo la kiingereza, hususani kwenye kipengele cha fasihi, siwashauri waalimu kutegemea solely uchambuzi wa watu wengine.
Jambo hili linasababisha uvivu na kukosa ubunifu katika ufundishaji. kama mwalimu, unatakiwa kukiaoma kitabu husika na kuandaa uchambuzi wako ukishirikiana na wanafunzi wako.
Wanafunzi wengi wanafeli maswali ya literature kwa sababu nao hawasomi vitabu bali wanakariri chambuzi, matokeo yake swali lolote watakolopewa watajibu themes mfano, Fgm, corruption, position of women, trad and customs kwa upande wa novella hii ya conteh.
Tafadhali ndugu walimu, tubadilishe mtazamo huu kwa mistakabili wa ufaulu wa watoto wetu katika somo hili.
hawa walimu wavivu ndio wanaosababisha ufaulu wa masomo yenye walimu wa kutosha kua sawa na ule wa masomo yanye uhaba wa walimu.