Uchambuzi wa Shairi la Tausi kama ilivyo ghaniwa na Mbosso na Mrisho Mpoto

Uchambuzi wa Shairi la Tausi kama ilivyo ghaniwa na Mbosso na Mrisho Mpoto

init

Senior Member
Joined
Mar 22, 2021
Posts
115
Reaction score
109
Aawali ya yote ninapenda kuwashukuru kwa kubahatika kunusa uzi huu. Ifuatayo ni Tafakuri fupi ya uchambuzi Inayotokana na shairi la Tausi lililo ghaniwa na Mpoto akiwa na Mbosso.

Tausi wewe
Tausi wetu
Karibu Tausi uipambe nyumba yetu

Awali Mshairi ana mkaribisha Tausi, hivyo Tausi ni Mgeni katika nyumba yetu.
Tausi wewe
Tausi wetu
Mpendwa tausi mwayangu mwana kwetu
Chanua mbawa zako Tausi
Waione rangi yako Tausi
Mshairi anmsihi Tausi kuchanua mbawa zake kwani ameonekana ni mpole. Pia Tausi ameficha rangi zake.
Mpole sauti hiyo ndio sifa yako Tausi
Chanua mbawa zako Tausi
waione rangi yako Tausi
Mshariri anmsifu Tausi kwa upole wake, Tausi ni mpole na anasifika kwa hilo.
Jichunge Tausi
wasinyofoe nyoya lako
Pia Mshairi an msihi Tausi awe makini kwani wapo watu hawana nia njema dhidi yake na wanaweza Nyofoa nyoya lake.
Karibu Tausi
karibu Sana Tausi
mchezo uliotukuta nao ni wasandakalawe Amina mwenye kupata kapata mwenye kukosa akose
Mshairi ana dhihirisha kuwa Tausi Ameikuta hali ya kugombaniana 'Mchezo wa Sandakalawe Amina'
Kipapatio Cha kuku ugali mweusi
Analiaje kwiu kwiu
Mpaka Lin mwenye kupata apate
mpaka Lin mwenye kukosa akose
Asante Tausi
Umeukataa mlio wa kwiu kwiu
Na rangi ya kuku kugawana
Mshairi anauliza hali hii mpaka lini na kuonyesha matumaini kwa Tausi kuwa Atafanya kitu.
Tausi
Harufu unayoisikia ni yachakula walicho kula
Wameamua tu kujisaidia nyuma ya nyumba ili harufu irudi ndani kumchefua mpishi
Usishtuke ndivyo ilivyo kwa watu wenye shibe
Mshairi anamtaarifu Tausi kuwa watu wenye shibe wameamua kujisaidi Nje jirani na nyumba aliyokaribishwa ili wamchefue mpishi. Pia anamsihi Tausi asishtushwe nao.
Tausi
tumbo lenye kukataa huleta tu mawe mawe
Unapo taka kuwatambulisha watoto wako kwa wageni tumia idadi yetu na sio majina
Maana baadhi ya wanao wanatumia A.K.A siku hizi watakuvuruga
kumbuka vita la kumbi ni fungate lililo fungwa kwa mkazo halipaswi kumuumiza mbebaji
  • Hapa sijaelewa bado
Karibu Tausi
Tausi wewe
Tausi wetu
Karibu Tausi uipambe nyumba yetu
Tausi wewe
Tausi wetu
Mpendwa tausi mwayangu mwana kwetu
Chanua mbawa zako Tausi
Waione rangi yako Tausi
Mpole sauti hiyo ndio sifa yako Tausi
Chanua mbawa zako Tausi
waione rangi yako Tausi
Jichunge Tausi
wasinyofoe nyoya lako
Tausi Mimi mwanao baada ya kutoka jandoni
Nilidhani mm ni mkubwa sasa
Naambiwa ooooh hicho kilicho tolewa ni kipande Cha ngozi tu
Hakina mahusiano na kukua kwako
  • Hapa sijaelewa bado
kwel inamaana Kila anaye ingiza kidole puani anamashaka na alicho nusa
Hapa sasa Mshairi anamuuliza Tausi, Kwani Tausi ameonekana kuwa na Mtizamo kwamba kila aingizaye kidole puani anamashaka na alichonusa (Hii ikiwa ni siku Mbili baada ya Kujiuzulu kwa Spika )
Uliwahi kusema wewe mwenyewe
Mnyonge hapigani kwa fedha
Na tulifanya makosa kuchagua silaha
Silaha tuliyo ichagua itatutia unyonge
Na kuondoa unyonge kwa kutumia silaha za wenye nguvu ambazo sisi hatuna unazid kupoteza muda
Muda upi wasisi kukua au nyakati
Mshairi anamuuliza Tausi pia kama alivyo sema awali kwamba hapo awali tulichagua silaha ambayo ni pesa ambayo sisi hatuna na hivyo tutazidi kupoteza muda , je muda huo ni wa taifa kukua au nyakati tu ?
Tausi nimeamini asiyeona anapotumia torch sio kwaajili yake anawamuoikia wanao ona ili wasimkanyage
na ili iyote Tausi lazima ioze Kila mwenye zamu yake asiache kumwagilia
  • Natamani niifahamu
aaaahaaaaaahaaahaaaaa
viriboto kupe huretaga virusi Tausi
ukuta mweupe wausiufanye mweusi Tausi
Tausi wewe
Tausi wetu
Karibu Tausi uipambe nyumba yetu
Tausi wewe
Tausi wetu
Mpendwa tausi mwayangu mwana kwetu
Chanua mbawa zako Tausi
Waione rangi yako Tausi
Mpole sauti hiyo ndio sifa yako Tausi
Chanua mbawa zako Tausi
waione rangi yako Tausi
Jichunge Tausi
wasinyofoe nyoya lako




Kufuatia vizingiti hivyo elekezi ufuatao ni uchambuzi( Angalizo: Sito chambua vipande vyote).
Fani
  1. Muundo: Mchambuzi ametumia lugha ya picha inayo sadifu mandhari ya kazi yake ya fasihi.
  2. Mandhari: Jamiii ya Kitanzania
Maudhui
Yafuatayo ni maudhui ya mshairi
  1. Kumkaribisha Tausi (Mh SSH)
  2. Kumpogeza Tausi
  3. Kumsihi Tausi jinsi jamii ilivyo na mategemeo makubwa juu ya ujio wake nyumbani.
  4. Kumtahadharisha Tausi juu ya yanayoendelea.
  5. Kutilia shaka baadhi ya mawazo ya Tausi.
DHAMIRA KUU YA MSHAIRI NI KUMKARIBISHa TAUSI
Mshairi amegusia maswala ya fuatayo:
  • Uongozi
  • Fitna
  • Uchumi

Ninaomba kuhitimisha kwa kuribisha mawazo zaidi katika shairi hili hususani katika vipengele ambavyo sija vieleza vyenye wino wa kijani.
 
Aawali ya yote ninapenda kuwashukuru kwa kubahatika kunusa uzi huu. Ifuatayo ni Tafakuri fupi ya uchambuzi Inayotokana na shairi la Tausi lililo ghaniwa na Mpoto akiwa na Mbosso...
✍️
 
Unapo taka kuwatambulisha watoto wako kwa wageni tumia idadi yetu na sio majina

Hapa nahisi amemaanisha anapoteua viongozi aangalie makabila yote (kanda zote) sio ukusini kusini au ukaskazini kaskazini
 
Tausi kuna kupe huko wasiifanye nyumba nyeupe( ikulu) kuwa nyeusi( ya kumwaga damu).

Fasihi na mimi nilisoma bwana.
 
Asante mleta mada. Moderators( hivi tafsiri ya neno moderators ni nini kwa kiswahili?) uzi upelekwe jukwaa la Lugha.
 
Back
Top Bottom